Tafuta

Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amezindua ujenzi wa bwawa la kufua umeme utakaosaidia mchakato wa ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini Tanzania. Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amezindua ujenzi wa bwawa la kufua umeme utakaosaidia mchakato wa ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini Tanzania. 

Rais Magufuli: Ujenzi wa bwana la kufua umeme muhimu kwa uchumi wa viwanda Tanzania

Mradi huo wenye megawati 2,115 unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 6.5 ni moja ya maono ya Mwalimu Julius Nyerere aliyetaka maporomoko hayo yatumike kufua umeme maono ambayo Rais Magufuli ameyatekeleza kwa kuweka jiwe la msingi. Rais Magufuli anasema mradi huo hautaathiri mazingira na badala yake utaimarisha ukuaji wa uchumi kupitia ujenzi wa viwanda.

Na mwandishi maalum - Morogoro

Rais John  Pombe Magufuli wa Tanzania  Ijumaa, tarehe 26 Julai 2019 amezindua ujenzi wa bwawa la kufua umeme katika mbuga ya wanyama ya Selou na kukamilika kwa mradi huu kutashusha bei ya umeme na kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini Tanzania. Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi la mradi wakufua umeme wa maji katika mto Rufiji mpakani mwa mikoa ya Pwani na Morogoro, Rais Magufuli amesema uhaba wa umeme unasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa viwandani na huduma za kijamii. Mradi huo wenye megawati 2,115 unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi trilioni 6.5 ni moja ya maono ya Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitaka maporomoko hayo yatumike kufua umeme maono ambayo Rais John Magufuli ameyatekeleza kwa kuweka jiwe la msingi.

Rais Magufuli amesisitiza kwamba mradi huo hautaathiri mazingira na badala yake utaimarisha ukuaji wa uchumi kupitia ujenzi wa viwanda. Amesema asilimia tatu pekee ya sehemu hiyo ya mbuga ya wanyama, yenye ukubwa wa kilomita 50,000 mraba, itatumika kwa ujenzi huo. Shirika la Umeme nchini Tanesco linazalisha megawati 1601 ambapo kukamilika kwa mradi wa kufua umeme wa maji rufiji itawezesha Tanzania kuwa na Megawat 3716 huku mahitaji ya ndani ya kiwa ni chini ya megawat 2000. Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni unasema mradi huo wa umeme utaathiri maisha ya watu 200,000 ikiwemo wakulima na wavuvi katika mto Rufiji.

Tangu mwaka 1982, Selou ilitangazwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuwa ni eneo la Urithi wa Ulimwengu, lenye thamani kwa ulimwengu chini ya Mkataba wa UNESCO uliyosainiwa na nchi 193.  Kujenga bwawa la kuzalisha umeme lenye urefu wa kilomita 100 na kilomita 25 kwa upana itakuwa ndiyo mwanzo wa kuiua hifadhi hiyo ya Selous ambayo ni sehemu ya kipekee ya maisha salama kwa wanyama. Katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli amemwagiza Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala kugawa pori la Selou kuwa mbuga ya Taifa ili kudhibiti shughuli za uwindaji wa wanyama unaofanyika katika pori hilo na hivyo kuendelea kulikosesha taifa mapato halisi ya shughuli za uwindaji zinazofanywa katika pori hili. Kamwe watanzania wasikubali tena “kulaliwa” na wajanja wachache kwa mafao yao binafsi.

29 July 2019, 09:15