Tafuta

Vatican News
Zaidi ya familia milioni 5 Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Caribbean kila mwaka hutumia zaidi ya 40% ya gharama zao za familia zisizo za chakula katika huduma za afya kwa  mama wazazi Zaidi ya familia milioni 5 Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na Caribbean kila mwaka hutumia zaidi ya 40% ya gharama zao za familia zisizo za chakula katika huduma za afya kwa mama wazazi  (AFP or licensors)

UNICEF:Watoto 7.000 wanakufa kila siku katika mwezi wa kwanza wa maisha

Tangu mwaka 2010 hadi 2017 kumekuwa na ongezeko kutoka wafanyakazi wa afya 4 hadi 5 kwa watu 10,000 nchini Msumbini na kutoka 2 hadi 9 nchini Ethiopia na wakati kipindi hicho nchini Norway idadi imeongeza kutoka wafanyakazi 213 hadi 228 kwa watu 10,000.Zaidi ya familia milioni 5 Afrika,Asia,Amerika ya Kusini na Caribbean kila mwaka hutumia zaidi ya 40% ya gharama zao katika familia zisizo za chakula katika huduma za afya kwa mama wazazi

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kwa mujibu wa Ripoti mpya ya Shirika la Watoto UNICEF kuhusu afya ya mama, zaidi ya familiia milioni 5 katika Bara la Afrika, Asia, Amerika ya Kusini na  Caribbean kila mwaka hutumia zaidi ya 40% ya gharama zao za familia zisizo za chakula katika huduma za afya kwa  mama wazazi. Karibu theluthi mbili ya familia hizi, au tuseme karibia  milioni 3, ziko Asia, wakati karibu milioni 1.9 ziko Afrika. Kulingana na uchambuzi, gharama za utunzaji wa ujauzito na huduma za kujifungua zinaweza kuzuia wanawake wajawazito kukosa kutafuta huduma za matibabu na kuhatarisha maisha ya mama na watoto wao. Kwa familia nyingi gharama za kujifungua ni janga kubwa na iwapo familia haiwezi kugharamia  matokeo yake ni hatari pia na watoto kwa mujibu wa Bi Henrietta Fore, Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF.

Utafiti kwa ujumla unaonesha kuwa

Utafiti uliofanywa unaonesha kwamba, ingawa maendeleo mengi yamefanywa duniani kote katika kuboresha huduma za wanawake kwa huduma za uzazi, lakini inaonesha kwamba zaidi ya wanawake 800 bado wanakufa kila siku kutokana na matatizo yanayo husiana na ujauzito. Kila siku kuna watoto 7,000 wanaozaliwa wamekufa, nusu yao wakiwa hai wakati wanazaliwa na watoto 7,000 wanakufa  katika mwezi wa kwanza wa maish yao. Hali halisi ni ngumu kwa wanawake masikini zaidi. Karibu  Asia ya Kusini yote  na mara nyingi wanawake matajiri hutazamwa mara nne au zaidi za kujitunza kabla ya kujifungua kuliko wanawake kutoka kwa familia masikini. Linapokuja suala la wanawake wanaozalia katika kituo, pengo kati ya maskini zaidi na tajiri ni zaidi ya mara mbili katika nchi za Afrika Magharibi na Kati.

Mamilioni ya watoto wanazaliwa bila msaada maalum

Madaktari, manesi na wakunga wanajikita katika shughuli yao msingi wa kusaidia mama, lakini ni mamilioni ya watoto wambao wanazaliwa bila msaada maalum. Kwa mujibu wa Ripoti, tangu mwaka 2010 hadi 2017 kumekuwa na ongezeko kutoka wafanyakazi wa afya 4 hadi 5 kwa watu 10,000 nchini Msumbiji na kutoka 2 hadi 9 nchini Ethiopia, na katika kipindi hicho hicho nchini Norway, idadi imeongeza kutoka wafanyakazi 213 hadi 228 kwa watu 10,000. Utafiti huo pia unasema kuwa katika dunia matatizo ya mimba ni sababu kuu ya kifo kati ya wasichana wenye umri wa miaka 15 na 19.  Kwa sababu wasichana bado hawajakomaa na ambao wako katika  hatari kubwa ya matatizo ikiwa wanapata ujamzito. Aidha watoto wao wana hatari zaidi ya kufa kabla ya kuzaliwa na  kabla ya kufikisha miaka mitano. Ripoti pia  inasema kwamba wasichana walio olewa wakiwa wadogo na vijana wadogo wako hatari ya kifo kwa sababu ya kutokupata huduma za afya wakati wa ujauzito au kuzaliwa katika kituo cha afya kuliko wanawake walioolewa na watu wazima.

Kwa ujumla, wasichana walioolewa wakiwa wadogo na vijana wadogo wanaishia kuwa na watoto wengi wa kutunza na mara nyingi zaidi kuliko wanawake wanaolewa wakiwa  watu wazima. Katika nchi ya  Cameroon, Chad na Gambia, zaidi ya 60% ya wasichana wenye umri wa miaka 20 hadi 24 ambao wameolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 15 wana watoto 3 au zaidi, ikilinganishwa  na asilimia 10 ya wanawake wa umri huo ambao wameolewa na watu wazima . "Tunashindwa kutoa msaada wa ubora kwa mama masikini zaidi na walio na mazingira magumu zaidi," amesema Bi Fore. Mama wengi huendelea kuteseka kwa muda usiojulikana, hasa wakati wa kujifungua. Lakini  tunaweza kuzuia mateso haya na kuokoa mamilioni ya watu katika mikono salama, vifaa vya kazi na huduma bora zaidi kabla, wakati na baada ya ujauzito".

03 June 2019, 12:40