Tafuta

Vatican News
Tangu tarehe 3 Juni watu zaidi 160 wamekufa kufuatia na ghasia zinazoendelea nchini humo, wakati huo huo hospitali hazina chochote. Tangu tarehe 3 Juni watu zaidi 160 wamekufa kufuatia na ghasia zinazoendelea nchini humo, wakati huo huo hospitali hazina chochote.  (AFP or licensors)

Sudan:Tangu tarehe 3 Juni zaidi ya watu 160 wamekufa wakiwemo watoto na wanawake

Tangu tarehe 3 Juni zaidi ya watu 160 wamekufa miongoni wao ni wanawake 50 na watoto 30 na zaidi ya majeruhi 1500.Kwa sasa hospitali hazina kitu chochote,kwa mujibu wa shirika la Amsi na Co-mai.Kwa sasa wanajeshi wameonesha hawataki kutoa madaraka kwa watu na wanataka kuendelea kuongoza hasa makamu rais.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 9 Juni kumekuwa na mgomo wa raia katika mji wa Sudan na vifo vya watu 160 na  wakati  hu wanawake  50 na watoto 30. Foad Aodi ni mwanzilishi wa Amsi ambalo ni Shirikisho la Madaktari wenye asili ya kigeni nchini Italia na Co-mai ambayo ni Jumuiya ya dunia ya kiarabu nchini Italia aliyetoa taarifa juu ya picha halisi ya kipeo cha madaktari mahalia huko  Sudan kwamba ni ya kute wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kuongezeka  ghasia na idadi ya vifo vya watu ambavyo havitajwi kwa maana wanatupa miili ikiwa imefungiwa na uzito fulani ili isiweze kuelea. Ni hali ya kutisha ya ukatili.

Wanajeshi hawataki kuacha madaraka

Hadi sasa wanajeshi wamejionesha hawataki kutoa madaraka kwa watu na wanataka kuendelea kuongoza hasa makamu rais ambaye ni kiongozi wa kikundi cha kijeshi kiitwacho Aldam Alsaree na ambaye ni mhusika wa suala la ukosefu wa usalama, kufuatia na mauaji tangu tarehe 3 Juni. Kwa mujibu wa taarifa mahalia inasema ni zaidi ya watu 160 na zaidi wanawake 50 na watoto 30 na wengi wao wametupwa katika mto Nile wakiwa wamefungiwa uzito fulani ili miili isiweze kuelea juu, japokuwa wanabainisha kwamba, kila siku wanaokota miili ya watu. Aidha wanasema, wamekuta wanawake wawili wamechomwa ndani ya hema lao huko Sit-In. Hadi sasa ni zaidi ya watu 1500 waliojeruhiwa na ambao wanajeshi wanazuia wasiende katika hospitali na kulazimisha madaktari wasiwatibu katika baadhi ya mahospitali.

Kuzuia maduka yasifunguliwe na mazoezi mengine 

Tarehe 9 wameanza na mgomo wa raia katika mji wa Sudan na kufunga mazoezi ya shughuli za kawaida na maduka kwa  kuwazuia watu wasiende kufanya kazi hadi wanaangusha utawala lakini hofu na wasiwasi ni  mkubwa kwa mujibu wa taarifa za madaktari. Lengo la serikali ni kuua watu kwa wingi hasa katika misikiti wakati wanasali na aina nyingine za kutumia nguvu na kuua kwa wingi; na katika siku ya  kwanza ya maandamano makuu watu 6 walikufa na 50 kujeruhiwa.

11 June 2019, 15:09