Tafuta

Vatican News
Kila mwaka ni milioni 92 tu ya watoa damu damu, shukrani kwao kwa kuokoa maisha ya wahitaji kwa mujibu wa WHO.Kwa hakika mchango wa kutoa damu ni tendo kubwa la ubinadamu na ustaarabu! Kila mwaka ni milioni 92 tu ya watoa damu damu, shukrani kwao kwa kuokoa maisha ya wahitaji kwa mujibu wa WHO.Kwa hakika mchango wa kutoa damu ni tendo kubwa la ubinadamu na ustaarabu! 

Siku ya Kimataifa ya kuchangia damu 2019:Damu salama kwa wote!

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kuchangia damu duniani 2019,inaongozwa na kaulimbiu “damu salama kwa wote”,Rwanda ndiyo mwenyeji wa maadhimisho ya kimataifa kwa siku hii. Shirika la Afya duniani WHO linashukuru watoa damu katika kuokoa maisha kwa wahitaji.Wanasihi wadau husika kuimarisha mchango wa hiari bila malipo ili kuboresha benki ya damu salama na yenye kutosha kwa ajili ya dharura

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kila tarehe 14 Juni ya kila mwaka nchi zote duniani kote zinaadhimisha siku ya kimaifa ya kuchangia damu. Tukio linataka kuwashukuru watoaji kwa ihari yao  damu katika kusaidia maisha na kuhamasisha umuhimu wa kawaida wa kuhakikisha kwamba ubora, usalama na uwezekano wa damu na kwa watoaji damu kwa ajili ya wagonjwa wenye kuhitaji unapatikana kwa wakati unaohitajika. Lengo la toleo ya siku hii ambayo inafanyika kimataifa katika mji Mkuu wa Kigali ni kuhamasisha wazalendo, serikali na huduma za afya ili ziweze kuchukua hatua nzuri za sera kisiasa katika kuhamasiaha na kulinda zawadi ya kujitolea bila malipo, kwa wakati, ushirikishwaji na uwajibikaji. Vile vile kuwaajibisha wengine wapya ambao wanaweza kujitolea damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wengine.Maadili muhimu ni kuhakikisha damu na bidhaa za damu na viwango vya juu vya ubora na usalama.Kadhalika, ASANTE kwa watoaji damu ambao wametambua kwa kina mahitaji ya yule anayeteseka na kujikita kwa namna ya pekee kutumia muda wa saa moja kwa ajili ya kusaidia na zawadi yao. Kwa mfano kila siku nchini Italia watu wanaishi, shukrani kwa ishara ndogo na rahisi, lakini ambayo ni muimu sana kwa mujibu wa mkuu wa kitengo katika ofisi za kitengo cha Afya duniani. Aidha Kutoa damu inawakilisha tendo kubwa sana la maisha ya mwanadamu ambaye anaweza kufanya kwa ajili ya kusaidia yule hasiyekuwa na fursa na ndiyo maana shirika la Afya duniani linatoa shukrani kubwa na litazidi kushukuru daima kwa kusema ASANTE.

Kila mwaka milioni 92 za watoaji damu: Dk. Karl Landsteiner mvumbuzi wa makundi ya damu ABO

Kila mwaka milioni 92 ni watoa damu. Na karibu asilimia 50 ya watu hawa wanatoka katika Nchi zilizo endelea ambao zinafanya asilimia 15% tu ya watu wote duniani kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Hata hivyo Siku ya watoaji damu duniani, ndiyo siku aliyozaliwa mvumbuzi wa makundi ya damu ABO, ambaye ni raia wa Austria Dk. Karl Landsteiner (Vienna 1868-New York 1943). Daktari huyo alikuwa ni mtafiti huko Vienna  Austria na tangu 1922 akahamia katika taasisi ya Rockefeller ya utafiti wa matibabu huko New York Marekani. Kunako miaka ya 1900, kwa dhati, uhamisho wa damu ulikuwa umefanyika kwa zaidi ya karne mbili bila kufikia matokeo mazuri. Katika miaka hiyo matokeo ya hatari ya kutofautiana na ambayo yalijitokeza kati ya wagonjwa wa makundi tofauti ya damu yalisababishwa bado kutoambuliwa vizuri kwa sababu haya yalikuwa bado hayajulikani. Mageuzi yalianzishwa mwaka 1901, wakati daktari wa Austria, Karl Landsteiner alipopindua ulimwengu wa uhamisho wa damu, kutokana na ugunduzi wa mfumo wa makundi ya  damu ya AB0. Mwaka wa 1930 alipewa Tuzo ya Nobel ya dawa. Aliunganisha jina lake la ugunduzi wa makundi ya damu A B O  na kipengele cha Rh na A. Wiener, 1940; Yeye ni mwandishi wa Ripoti za  utafiti mbalimbali, umuhimu msingi wa majaribio ya magonjwa, juu ya hemoglobinuria baridi, juu ya maambukizi makubwa na majaribio ya tafiti nyingine nyingi kuhusiana na damu.

Kutoa damu daima ni wazo jema hasa kiangazi, mtoaji anaweza kuokoa maisha hadi watu 3

Haiwezekani kuunda damu katika maabara hivyo watoaji damu wa ihali ndiyo njia pekee ya kuwawezesha wote wenye kuwa na mahitaji hayo. Kila mtoaji damu anaweza kusaidia kuokoa maisha hadi ya watu watatu. Ishara hiyo ya upendo ni chanya sana hata katika afya zetu. Watu wenye kuwa na damu nyingi, wanaboresha pia afya yao katika kutoa zawadi hiyo na shukrani kwa vipimo maalum ambapo pia katika utoaji damu unawezekana kugundua pia ugonjwa mapema unaoanza katika mwili wako na kutibiwa mapema. Ni suala la kutengeneza uwezekano wa kutunza afya yetu na kuhisi  zaidi uwajibikaji wa kuchagua mtindo wa maisha yaliyo bora. Pia damu inaweza kufafanuliwa kama dawa ya kweli ya kuokoa . Katika kutoa damu inawekana pia kusaidia kesi nyingi kwa mfano  kutoa damu  kwa dharura, magonjwa ya saratani, hatua za upasuaji,  upasuaji mgumu  wa kasoro za kuzaliwa. Kwa hakika mchango wa kutoa damu ni tendo kubwa la ubinadamu na ustaarabu!

Siku ya kimataifa kuazimisha mjini Kigali Rwanda: Ndege zisizo na rubani kuokoa maisha ya kusafirisha damu Rwanda

Upatikanaji wa damu salama ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la huduma za afya kwa wote lakini pia ni kipengee muhimu katika utendaji kazi wa mifumo ya afya kote duniani kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) katika maadhimsho ya siku ya uchangiaji damu duniani.Siku ya uchangiaji damu duniani ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 14 kwa mujibu wa WHO ni ya kuwashukuru mamilioni ya watu wanaojitolea kwa hiyari zawadi kubwa ya akiba katika maisha yao ambayo ni damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine lakini pia kuelimisha umuhimu wa uchangiaji damu katika jamii ili kuhakikisha watu na jamii zote wanapata fursa ya damu kwa gharama nafuu na kwa wakati. WHO inasema Rwanda imepiga hatua kubwa katika kutumia teknolojia mpya ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu vijijini.

Katika miongo miwili iliyopita Rwanda imeimarisha huduma ya damu

Katika miongo miwili iliyopita Rwanda imeimarisha huduma ya damu nchi nzima na kuongeza mara tatu kiwango cha uchangiaji damu kati ya mwaka 2000 na 20018. Mafanikio haya ya huduma Rwanda WHO inasema yamechangiwa na kutumia teknolojia bunifu kama ndege zisizo na rubani au drone kwa kusafirisha damu haraka kwa wanaohitaji. Huduma ya kuongeza na kuchangia damu ilianza nchini Rwanda kunako mwaka 1975 na tangu mwaka 1985 ilikuwa ni kwa hiyari na bila malipo yoyote. Mauaji ya kimbari ya 1994 yalisambaratisha vibaya miundombinu na mifumo ya afya Rwanda, lakini serikali ilitoa kipaumbele katika kujenga upya huduma ya uongezaji damu kwa kutambua ni jinsi gani ilivyo muhimu kuwa na fursa ya upatikanaji wa damu katika kuokoa maisha. Hivyo nchi hiyo ikachukua hatua mbalimbali ya kuimarisha usalama na upatikanaji wa damu nchi nzima njia ambazo WHO inasema zimesaidia kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili kati ya mwaka 2000 na 2015 na vifo vya kina mama  wajawazito kwa robo tatu.

Tarehe 14 Juni siku ya kutoa damu ya kutosha na salama kwa wagonjwa wote wanaohitaji

Kutokana na juhudi hizo tarehe 14 Juni 2019  kituo cha taifa cha uongezaji damu (NCBT) kinatoa damu ya kutosha na salama kwa wagonjwa wote wanaoihitaji. Na lengo hili limefikiwa kupitia vituo 541 vya kudumu vya ukusanyaji damu na vituo 5 vya kikanda vya usambazaji damu ambavyo vinahudumia vituo vya afya 66 vya uongezaji damu. Na moja ya changamoto kubwa iliyokuwa ikiikumba Rwanda katika kufikisha damu kwa wanaohitaji hususani vijijini ni miundombinu kwani ni taifa la milima na barabara mbovu. Lakini sasa inatumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani au drones ziitwazo “zipline” ambazo zinakata muda wa kusafirisha damu hiyo kutoka saa 4 hadi dakika 15 kwa baadhi ya maeneo. Akizungumzia umuhimu wa hatua hivyo waziri wa afya wa Rwanda Dk. Diane Gashumba amesema :“kila sekunde unayoongeza katika kuokoa maisha ni muhimu sana, tulipotambua kwamba zipline zitakuwa suluhu hatukusita.”

Teknolojia ya drones bila wachangiaji damu haina maana

Hata hivyo katika ufafanuzi zaidi ni kwamba teknolojia kama hizo bila wachangiaji damu inayohitajika hazina maana. Tangu 1985 sera ya Rwanda ni kwamba uchangiaji damu ni wa hiyari bila malipo na inatolewa kwa wagonjwa wanaoihitaji bure bila malipo. Hata hivyo shirika la WHO limesema fursa ya kupata damu salama sio utamaduni kwa kila nchi, katika siku hii ya uchangiaji damu linatoa wito wa upatikanaji wa damu salama kwa wote kwa kusema kuwa Rwanda ni mfano ambao unapaswa kuigwa endapo dunia itahitaji kuwa na damu salama ya kutosha na bidhaa zingine za damu kwa ajili ya kila anayehitaji , ikiwaasa watu kujitolea damu leo ili kuokoa maisha. Aidha WHO inasema janga kubwa la kibinadamu la hivi sasa limeweka dhahiri upungufu mkubwa wa mfumo wa afya barani humo, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa damu kwa wakati muafaka na kwa usalama. Hivyo katika maadhimisho haya WHO imesihi wadau husika kuimarisha mchango wa hiari, bila malipo, ili kuboresha benki ya damu salama na yenye kutosha kwa ajili ya dharura. Hivyo, ipo haja ya kuchangia damu kwa wale wenye uwezo wa kufanya hivyo, jambo ambalo litawasaidia wale wenye mahitaji maalumu ya dharura. Pia si kwa usaidizi wa watu tu lakini hadi kwa Mwenyezimungu watu wanaochangia damu watapata ujira kutoka kwake.

Zanzibar na maadhimisho ya siku ya kuchangia damu kimataifa

Zanzibar kama sehemu nyingine imeadhimisha siku ya kimataifa ya kuchangia damu kwa  kufanya hafla ya uchangiaji damu katika eneo la Mwanakwerekwe Unguja na maeneo mengine ya nje ya mji. “Kama zilivyo nchi nyengine lakini na Zanzibar ina mahitaji makubwa ya huduma za damu hasa kwa watoto, wazazi na wahanga wa ajali hivyo uwepo wa damu katika hospitali zetu utasaidia sana kuokoa makundi hayo”. Ni maneno ya waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed hivi karibuni  akiwataka wananchi kuendelea kuchangia damu kwa hiari kwani mahitaji ya damu salama nchini yamekuwa makubwa, kufuatia na siku hii. Kadhalika amesema  mahitaji ya damu kwa mwezi ni wastani wa chupa 1,550 kwa matumizi ya kawaida na watumiaji wakubwa ni mama wajawazito, watoto, wahanga wa ajali na wagonjwa wa upasuaji. Waziri Hamad amesema kutokana na wananchi wengi kuhamasika kutumia hospitali na vituo vya afya mahitaji ya damu yanaongezeka kwa kiasi. Hata hivyo, alizipongeza taasisi na vikundi vya hiari vinavyojitokeza kuchangia damu kwa hiari katika mabonanza yanayoandaliwa na kitengo cha damu salama ambapo imekuwa msaada mkubwa katika hospitali na vituo vya afya. Ameahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi za kijamii na vikundi mbali mbali vinavyojitolea kuchangia damu ili kuondosha tatizo la damu na kuokoa maisha ya wananchi.

14 June 2019, 11:25