Shirika la Kazi Duniani, ILO linaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwekeza kwa rasilimali watu-wanawake katika uzalishaji, huduma na uongozi wa ngazi ya juu, kwani inalipa! Shirika la Kazi Duniani, ILO linaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwekeza kwa rasilimali watu-wanawake katika uzalishaji, huduma na uongozi wa ngazi ya juu, kwani inalipa! 

ILO: Wekezeni kwa rasilimali-wanawake! Inalipa sana!

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba, uwepo mkamilifu wa wanawake katika shughuli za uzalishaji na huduma ni muhimu sana kwani zinachangia katika tija, ufanisi na ubora wa bidhaa na huduma inayotolewa. Haya yamo katika taarifa ya utafiti uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani kuhusu umuhimu wa kukuza fursa sawa kati ya wanawake na wanaume. T

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirika la Kazi Duniani, ILO linasema, sekta ya kazi haina budi kujikita katika ubunifu ili kuimarisha uchumi fungamani na kusonga mbele katika mchakato wa malengo endelevu ya binadamu! Mabadiliko katika mfumo wa kazi, mahusiano katika maeneo ya kazi pamoja na umuhimu wa mapumziko kwa wafanyakazi ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa, ili kuongeza tija na ufanisi kazini. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba, uwepo mkamilifu wa wanawake katika shughuli za uzalishaji na huduma ni muhimu sana kwani zinachangia katika tija, ufanisi na ubora wa bidhaa na huduma inayotolewa. Haya yamo katika taarifa ya utafiti uliofanywa na Shirika la Kazi Duniani kuhusu umuhimu wa kukuza fursa sawa kati ya wanawake na wanaume.

Takwimu zilizochukuliwa kutoka katika makapuni 13, 000 katika nchi 70 zinaonesha kwamba, asilimia 57% ya jitihada za kuboresha fursa kati ya wanawake na wanaume zimechangia katika maboresho ya uzalishaji wa bidhaa na huduma. Hali hii pia imechangia kwa ongezeko la faida kutoka kutoka asilimia 5% hadi asilimia 20%. Takwimu zinaonesha kwamba, mahali ambapo, wanawake wamepewa nafasi za juu katika uongozi, huduma zimeboreka na faida imeongezeka. Umoja wa Mataifa unasema, bado kuna changamoto kubwa kwa wanawake ili kuweza kufikia kupata nafasi za juu katika uongozi, kumbe, hapa utashi wa kisiasa unahitajika zaidi.

Deborah France-Massin, Mkurugenzi wa Ofisi ya Ajira, Shirika la Kazi Duniani anasema, umefika wakati kwa makapuni kuwekeza kwenye rasilimali watu- yaaniwanawake kama kipaumbele katika mchakato wa kuongeza tija, ubora na faida. Ubaguzi dhidi ya wanawake katika fursa za kazi na ajira, umewafanya kuonekana kuwa si mali kitu na kwamba, wao ni watu wanaoweza kufanya kazi za nyumbani, ikiwa ni pamoja na kulea watoto. Utafiti huu wa Umoja wa Mataifa, uwe ni chachu ya kuboresha nafasi za kazi miongoni mwa wanawake, ili hata wao wapewe nafasi za juu katika uongozi wa makapuni na jamii katika ujumla wake. Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba, wanawake wanawekewa mazingira mazuri ya kazi, ili waweze pia kutekeleza dhamana na wajibu wao kama akina mama.

Takwimu zinaonesha kwamba, wanawake wenye nafasi za juu katika uongozi ni wachache sana. Fursa sawa kati ya wanawake na wanaume kwenye maeneo ya kazi ni muhimu sana ili kuweza kupata mafanikio makubwa katika uzalishaji na huduma.

ILO:Ajira

 

04 June 2019, 11:37