Tafuta

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuendeleza mema waliyotenda wakati mwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuendeleza mema waliyotenda wakati mwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Siku kuu ya Eid 2019: Endelezeni mema ya Mfungo wa Ramadhani

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema, wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwa waislam na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote. “Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.”

Na Mwandishi maalum Ofisi ya Waziri Mkuu – Dar Es Salaam.

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka waamini wote wa dini ya Kiislam nchini Tanzania kutumia Siku kuu ya Eid el Fitr kwa kutenda matendo mema pamoja na kuwakumbuka yatima na wajane. “Leo ni siku kubwa na muhimu Waislamu wanahitimisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, hivyo tuendeleze matendo mema.” Waziri Mkuu ameyasema hayo Jumatano, Juni 5, 2019 wakati aliposhiriki swala ya Eid El Fitr katika msikiti wa Anwar uliopo Msasani jinini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema, wakati huu ni mzuri kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwa waislam na madhehebu mengine, hivyo hakikisheni mnayaendeleza mambo mema yote. “Tumeona utulivu uliojitokeza katika mwezi mtukufu, na jambo hili limesisitizwa na viongozi wa dini. Tuendelee kuwa wamoja, tuimarishe mshikamano na tuvumiliane.” Pia, Waziri Mkuu amewakumbusha wazazi na walezi kuwaongoza watoto kwa kuwapa mafundisho ya dini yatakayowawezesha kumjua Mwenyezi Mungu na kuwa raia wema.

Awali, Imamu wa msikiti huo, Sheikh Mhina alisema waislamu wanatakiwa kuitumia siku ya leo kwa kuhamasisha Amani pamoja na kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo. Pia amewasisitiza wayaendeleze mema yote waliyoyafanya katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu na kuwajali wazazi wao.

 

05 June 2019, 11:01