HAITI:Ujumbe wa maaskofu kuhusu kesi ya Petrocaribe ni kupambana na rushwa na kushtaki wafisadi!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Mamia elfu ya watu wa Haiti wameshuka kuandamana katika bararaba ya mji Mkuu tarehe 9 Juni 2019 wakiomba Rais wa Haiti Jovenel Moïse ajiuzuru. Kwa mujibu ripoti za Mahakama Kuu kitengo cha Wakaguzi na Utawala wa Madai kuhusu mahesabu yeye ni mhusika wa matumizi mabaya ya fedha na kupotea kwa fedha za PetroCaribe siku chache zilizopita. Kuhusiana na mahesabu, Mahakama Kuu imetoa ripoti yenye zaidi ya kurasa 600 juu ya uendeshaji wa Petrocaribe, ambao ni mpango wa maendeleo unaofadhiliwa na Venezuela, kwa kutoa ufafanuzi ulio wazi kuhusu idadi kubwa ya kesi za undeshaji kiholela wa fedha na rushwa zenye kufikia maelfu na maelfu ya dola za kimarekani. Kufuatia na suala hili, Baraza la Maaskofu wa Haiti (CEH) katika ujumbe wao uliotiwa sahini na Askofu Launay Saturné, wa Jimbo Katoliki la Jacmel na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Haiti (CEH) pamoja na maaskofu wote wa (CEH) wamejibu kwa sauti kali mbele ya kesi hii mpya ya matumizi mabaya ya fedha. Maaskofu wanasema: “Tumesoma kwa uangalifu na kuwa na mtazamo wa taarifa mbili za ukaguzi zilizo tolewa na Mahakama Kuu ya Wakaguzi na Utawala wa Madai (CSC/CA) juu ya usimamizi wa mipango iliyo fadhiliwa na fedha za PetroCaribe”.
Ukubwa na ubaya wa rushwa
Maaskofu wa Haiti, wanasema, mpango huu ni mwanga ulio wazi na mkubwa juu ya jambo kubwa na la kushangaza kuhusiana na ubaya wa rushwa katika njia zake mbalimbali hasa za kisiasa na za uendeshaji. Rushwa iliyojumuishwa inageuka kuwa ubaya wa mwisho kiukweli uliosababisha na wizi uliopangwa. “Imekuwa ni janga la kweli la kijamii ambalo linasumbua taasisi zetu na kwa hiyo linadhoofisha sana wote kutokana na mtazamo wa kimaadili na kiuchumi na maendeleo ya nchi yetu. Wanasema maaskofu: watu wa Haiti wanatarajia taarifa hizi mbili za udhibiti zilizotolewa na CSC / CA kufuatiliwa. Katika ghadhabu na kashfa kubwa ya rushwa inayofikia au kubomoa kilele cha serikali, wanaomba kesi ya PetroCaribe itiliwe maanani. Vile vile Maaskofu wa Haiti wanabainisha kuwa nchi yao imekuwa na mfumo maskini zaidi kutokana na tamaa za viongozi walaruaji na ambao hawana uwezo wa kutazama hali halisi ya watu na matatizo yao. Viongozi hao hawasaidii maendeleo ya nchi. Watu wako wanateseka na matokeo hayo …na madhara ya matendo hayo… kwa sababu ya ukosefu wa msimamo wa kisiasa na wakati huo huo kugeuka nyakati za ulevi wa mauaji bila kikomo. Kwa hakika wanateseka katika sekta zote za maisha kitaifa na zaidi ghasia zinamkumba kila mmoja, wanaandika.
Ni wakati wa kuwajibika
Hata hivyo katika ujumbe wao, Maaskofu wa Haiti wanakumbusha kuwa haisadii kuhesabu yote hayo, badala yake kinacho takiwa ni uwajibikaji. Muda umetimia sasa wa kufanya mabadiliko, hasa mbadiliko ya kina… wanaomba wazalendo wajaribu kubainisha wale ambao kweli wanajaribu kutafuta wema wao. Hiyo ni kutokana na kwamba mambo yanabadilika; ni ya lazima na kwa ngazi zote za utawala, katika maofisi, wanawake na wanaume wapya katika akili yao na katika dhamiri yao ya kitaaluma na uwezo wao. Hilo ndiyo lengo ambalo wameamua kuingilia katika ili viongozi wa kisiasa wawe mstari wa mbele katika uwajibikaji wao. Wanawashauri waweze kutafuta namna ya kurudisha haki kijamii na kujiwakilisha katika haki ya nchi na mbayo ni gharama kubwa kurudisha maadili ya utawala katika Serikali na viongozi wake!