Tafuta

Vatican News
Akofu Mkuu Dieudonné Nzapalainga wakati akizungumzia kuhusu matendo maovu ya kikundi kipya cha uhasi kwa waandishi wa habari anashurumu ukatili na mauaji yanatendeka nchini mwake Akofu Mkuu Dieudonné Nzapalainga wakati akizungumzia kuhusu matendo maovu ya kikundi kipya cha uhasi kwa waandishi wa habari anashurumu ukatili na mauaji yanatendeka nchini mwake 

Askofu Mkuu Nzapalainga:Siyo silaha itakayo komboa Jamhuri ya Afrika ya Kati!

Ni wakati sasa wa kuzika maovu ya kasi za vita zitokanazo na kikundi cha kihasi kitokanacho na kikundi cha Rassemblement patriotique pour le renouveau de la Centrafrique ambacho pia ni moja kati ya watia sahini ya mkataba wa amani huko Khartoum na serikali ya Bangui.Siyo silaha iatakomboa Jumhuri ya Afrika ya Kati.Ni maneno ya Kardinali Dieudonné Nzapalainga wakati akizungumzia na waadhishi wa Habari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali Dieudonné Nzapalainga wakati akizungumzia juu ya matendo maovu ya kikundi kipya cha uhasi nchini humo amesema : “Siyo kwa kutumia makundi ya silaha  yatakayo weza kuikomboa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na matatizo yake ya kijamii. Ni wakati sasa  wa  kuzika kasi za vita zitokanazo na kikundi cha kihasi kitokanacho na kikundi kiitwacho Rassemblement patriotique pour le renouveau de la Centrafrique ambacho pia ni moja kati ya watia sahini ya mkataba wa amani huko Khartoum na serikali ya Bangui.

Matatizo ni pamoja na barabara mbovu,ukosefu wa walimu bora na mfumo mbaya wa afya

Kardinali Nzapalainga akitaja baadhi ya matatizo mengi nchini Afrika ya Kanisa amethibitisha kuwa: “matatizo ya kweli ni barabara ambazo ziko katika hali ya kutisha, mashule yasiyokuwa na walimu bora, elimu ya chini nchini ambayo ni dhaifu sana na kama ilivyo hata mifumo wa afya”. “Ameongeza kusema: katika vituo vya afya, hakuna madaktari, labda mkunga mmoja tu. Leo kumi na tano, kesho kumi na sita na kumi na saba. Hawa wametia sahini ya mkataba hivi karibuni wa amani huko Khartoum na makundi ya kisilaha 14. Je mnapenda kufanya mkutano wa pili kwa ajili ya kutia mkataba wa makubaliano mengine? Ameuliza hayo katika mazungumzo na vyombo vya habari.

Pamoja na mkataba wa amani, hakuna kinacho endelea katika matendo

Pamoja na kuwa na  makubaliano ya amani mwezi februari, lakini bado kuna  ucheleweshaji wa kujikita katika matendo na hii inajionesha na matukio yasiyo simama ya mashambulizi na mauaji ya hovyo hata hivi karibuni. Tarehe 21 Mei wameuwawa raia 34 huko Kaskazini Magharibi ya nchi. Janga hili limetendeka katika vijiji viwili karibu kilometa 50 kutoka huko Paoua. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni kwamba baadhi ya makundi wenye silaha waliandaa mkutano na watu wa vijiji na watu walipofika makundi yenye silaha yalifyatua moto wa risasi na kuwaua watu. “Watu wakatili hawa hawatafakari juu ya watu wao wa Afrika ya Kati ambao wanataka amani” amethibisha Kardinali Nzapalainga na kutoa wito kwa serikali ili haki kwa hakika iweze kutendeka: “hakuna aliye juu ya sheria na lazima kuwajibishwa katika haki ya waathirika na wale waliotenda uhalifu huo lazima wajibu”.

12 June 2019, 11:41