Tafuta

Ziara ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika, Assisi kunako 2016 Ziara ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika, Assisi kunako 2016 

The Economy of Francesco:Wazo la vijana kuhusu dunia lizingatiwe sana!

Kufuatia na mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko kwa wanauchumi vijana na wajasiriamali wote,Profesa Bruni,Mkurugenzi wa Tume ya maandalizi ya Mkutano huo anasema kuwa kilicho kosekana miaka ya ‘900 siyo upendo kwa vijana bali ni heshima na kusikiliza wazo la vijana.Wao wana mtazamo tofauti zaidi ya watu wazima,hivyo lazima wazo lao lizingatiwe kwa kina.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kunzia tarehe 26-28 Machi 2020 katika mji wa Assisi utaongozwa na tukio la “The Economy of Francesco”, Uchumi wa Francis, katika  siku tatu ambazo zitajikita kwa wanauchumi vijana na wajasiriamali kutoka pande zote za dunia ambao wamealikwa moja kwa moja na Baba Mtakatifu Francisko. Kuna wazo kwa vijana hasa juu ya masuala ya mazingira na uchumi ambayo kwa upande wao, wako  mbele zaidi ya mawazo ya watu wazima kwa mujibu wa maelezo ya mwanauchumi Profesa Luigino Bruni aliyo eleza katika Gazeti katoliki la  Sir.  Profesa Bruni amesema kile kilicho kosekana miaka ya '900, siyo upendo kwa vijana, bali ni heshima na kusikiliza mawazo ya vijana. Na hiyo ni kutokana na kwamba,"vijana wanao maono ya hali ya juu ya mambo mengi, tofauti na yale ya watu wazima na kwa maana hiyo, wazo hili ni lazima kulizingatia sana! amesisitiza.

Mwaliko wa kushiriki vijana katika tukio hilo,ndiyo habari mpya inayotoka moja kwa moja kwa  Baba Mtakatifu Francisko kwa barua yake ya hivi karibuni: Profesa  Bruni wa Tume ya maandalizi ya Mkutano wa "The Economy of Francesco",  amesema , wao wamemwalika hata mwenye Tuzo ya Nobel, wataalam na watu wengine maarufu wa dunia  hii ili kuweza kushuhudia tukio hili, lakini lengo kuu hasa ni vijana. Vijana kutoka duniani kote ndiyo wako mstari wa mbele kuhusu mwaliko wa “The Economy of Francesco” amesisitiza. Katika tukio hili pia anasema kuwa litauganisha pamoja na shughuli za pamoja, kama vile tamasha, sanaa na mikutano mingine ya mwaka. Kwa hakika mwaliko wa kushiriki, ndiyo habari mpya  inayotoka kwa Baba Mtakatifu  iliyo tolewa hivi karibuni kwa pendekezo kubwa la kutaka kuwaunganisha vjana wote katika azimio ili kuweza kubadili mazingira ya sasa kiuchumi na kutoa mwamko mpya wa uchumi endelevu, ili uchumi huo uweze kuwa wa haki na zaidi unao unganisha na bila kumwacha mtu yeyote nyuma!

Tukio hili linaandaliwa na Tume ya Jimbo Katoliki la Assisi, Meya ya Assisi, Taasisi Kuu ya Assisi na Muungano wa Uchumi. Kutokana na hiyo Mwanachumi Luigino Bruni ambaye ni  Profesa wa Uchumi wa Siasa katika Chuo Kikuu cha Lumsa na ndiye Mkurugenzi wa Tume ya Kisayansi ya maandalizi amefafanua kwa kina kwamba, mkutano huo badala ya kuwahusisha wakuu wa nchi pekee yake na wakuu wa viwanda na ambao hawabadiliki, Baba Mtakatifu Francisko amependekeza kwa vijana ili awe na azimio la pamoja na kuwauliza, "Je mpo tayari kuwa na jitihada na mimi ili kuweza kubadili uchumi? Katika mkutano huo vijana karibia 500 kutoka duniani kote wataweza kuudhuria. Hawa ni vijana wanafunzi wanao somea au kupata shahada ya uchumi na vijana wajasiriamali. Vile vile wazo la mkutano huo ni kwamba, mara kwa mara vijana wanaweze kukutana na kukua pamoja  huku wakianzisha harakati za chama cha vijana wanauchumi katika ulimwenguni, katika Roho ya Baba Mtakatifu Francisko, lakini pia hata kwa roho ya Mtakatifu Francis wa Assisi. 

Assisi na uchumi, inaonekana ni mchanganyiko wa mambo mawili kwa kuzingatia kwamba Mtakatifu Francis alifanya uchaguzi wa umasikini uliokithiri na kwamba hata leo, tunakabiliwa na dhana hiyo, ambayo hujitokeza kama kupambana na uchumi kwa ajili ya uchumi ulio ubora. Je ni kwa nini uchaguzi huu?  Profesa Bruni akijibu swali hili amesema, kwa sababu Mtakatifu Francis wa Assisi alikuwa ni kitovu cha uchumi mwingine. Wafranciskani walikuwa ni watu wa kwanza kuwa wanauchumi Ulaya. Waliandika masuala mengi ya kwanza kuhusu uchumi wa miaka ya 1200 na 1300. Na kutoka kwa wafranciskani, ndipo kulianzishwa hata  Banki za kwanza za kisasa kwa mfano Benki ya "Monti di Pieta" katikati ya mwaka 1400. Vile vile Profesa anaeleza kuwa, kutokana na uchaguzi wa umasikini, waliweza kutafsiri uchumi kama zawadi na ushirikishwaji. Na zaidi huwezi kusema kuwa wafransiskani siyo wanauchumi. Wao wana njia nyingine ya kuelewa uchumi na ambapo maskini wanapewa kipaumbele, mahali ambapo utajiri ni wa kushirikishwa,hasa mahali ambapo kuna uchumi unao husishwa na mazingira kwa sababu  "Assisi pia ni Wimbo wa Viumbe", amesema.

Ni kwa nini Vijana?  Profesa akiulizwa kwa nini kuhusisha vijana katika suala la uchumi amesema: " Leo hii tunazo harakati kama zile za Greta ambazo zinajikita juu ya masuala makubwa ya mazingira, kuwahusisha vijana kutoka duniani kote na kwa upande mwingine tuna siasa kubwa zinazoshikilia maslahi  ya uchumi wa dunia na kuwa mikononi mwake. Lakini kinacho kosekana ni kiungo cha kati ,ikiwa na maana ya vijana kati ya umri wa miaka 25 na 35, ambao wanaingia katika ulimwengu wa uchumi na wakiwa na matumaini ya kuweza kuwa mstari wa mbele, japokuwa kwa hakika anasema, wamekatwa na wako nje kabisa katika mijadala mkubwa. Badala yake anasema Profesa Bruni, "lipo daraja kati ya Greta na viongozi wa kisiasa na Baba Mtakatifu Francisko anayerudia kutoa pendekezo kwao kwamba: je ninyi ambao mnasoma katika sekta hiyo, tunataka kubadilisha uchumi huu au hapana? Kutokana na hiyo, Profesa Bruni amesema, " wazo la Baba Mtakatifu ni kwamba vijana siyo wa wakati endelevu, bali ni wa wakati wa sasa".

Lakini unafikiria kuwa hii ni nafasi ya mabadiliko katika mfumo wa sasa kiuchumi?  Profesa Bruni anathibitisha uwezekano wa madadiliko  kwa sababu kwamba: "vijana wako ndani ya mabadiliko". Iwapo wangeweza kufikiria kuandaa Mkutano Assisi kwa ajili ya viongozi wakuu wa uchumi, wangeweza kupiga picha nzuri, japokuwa kwa hakika dunia isingeweza kubadilisha lolote, kwa maana viongozi wakuu ni  watu wasiobadilika. Na hilo ndilo jambo jipya ambalo ni maono ya Baba Mtakatifu huko Assisi kwa wanauchumi vijana, yaani kufanya mabadiliko tofauti, kuanzia wao. Ni jambo lenye maana na ishara kubwa kwa sababu Baba Mtakatifu anasema, vijana wanaweza kubadilisha dunia”, amethibitisha Profesa. Hata hivyo iwapo hakuna mabadiliko ya uchumi, wakati endelevu ni kama ule ambao tayari tuna ushuhudia sasa. Wakati endelevu wa sasa unajionesha na ukosefu wa usawa na kuzaliwa kwa aina nyingi za kutotosheka na wakati huo huo kuanzishwa mifumo ya vurugu kama vile yenye ugaidi na uharibifu wa sayari hii. Mambo hayo yote yapo tayari katika wakati uliopo na ndiyo ya wakati endelevu, iwapo hakuna linalofanyika  kudhibiti. Huo ndiyo ujumbe wa kina ambao kijana mdogo Greta anajaribu kueneza; ndiyo ujumbe ule ule ambao hata katika mkutano Assisi wataweza kuwaalika vijana wote, kwamba siyi kuzungumzia wakati endelevu, bali matatizo ambayo yapo tayari na hatuwezi kusubiri ya mbele, badala yake tunapaswa kubadilika kuanzia sasa. Na mabadiliko hayo tayari yanaanzia kwa vijana ambao wanaonesha utayari huo bila kusubiri kesho.

Kutazamia vijana katika uchumi ni wazo jipya ambalo halijawahi kutokea: Lakini zaidi iwapo kwa pamoja tutajikita kuanza mabadiliko hayo, tutaweza kuanzisha vyama vyenye uwezo wa kupokea watu, kujiunga na vyuo vikuu, katika mashirika na makumpuni mbali mbali tukiwa na vijana ambao watageuza na wenye uwezo mkuu wa mabadiliko. Kwa kutazama wazo la vijana hasa katika masuala ya mazingira, ni wazo ambalo liko mbele zaidi ya mawazo ya watu wazima. Kilicho kosekana miaka ya 1900 siyo upendo kwa vijana, bali ni heshima na kusikiliza wazo la vijana. Wao wana mtazamo wa mambo tofauti ya watu wazima, hasa yanayo husu mahesabu kama vile uchumi na mazingira, umasikini na  hadhi ya binadamu, kuheshimu viumbe na maendeleo endelevu. Hayo yote  ni mawazo ambayo lazima yazingatiwe sana kwa maana kipindi kipya kimeingia katika mzunguko wa umma lenye  wazo la vijana. Ni  kama jambo jipya ambalo hadi sasa halikuwahi kuwapo! Amethibitisha Profesa Bruni.

14 May 2019, 13:23