Tafuta

 Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia kwa mujibu wa shrika la Afya duniani na Unicef Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia kwa mujibu wa shrika la Afya duniani na Unicef 

Unicef/Who:Mtoto 1kati ya 7 duniani anazaliwa na uzito mdogo!

Ripoti iliyotolewa tarehe 16 Mei 2019 kutoka Chuo Kikuu cha London kwa mujibu wa watafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa WHO na UNICEF,wanathibitisha kuwa mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia ambapo takribani asilimia 75 ya watoto hao walizaliwa katika nchi za Asia ya Kusini na zile za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia ambapo takribani asilimia 75 ya watoto hao walizaliwa katika nchi za Asia ya Kusini na    zile za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. Ni takwimu mpya zilizotolewa tarehe 16 Mei 2019 na watafiti kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa na Chuo cha tiba za kitropiki na afya cha London, Uingereza (ambao ni watafiti wanaojumuisha shirika la afya duniani,WHO, shirika la kuhudumia watoto UNICEF) ambazo zimeonyesha kuwa mwaka 2015 zaidi ya watoto milioni 20 walizaliwa duniani kote wakiwa na uzito wa chini kupindukia, ambao ni chini ya kilo mbili na nusu au pauni 5.5.

Nchi za Ulaya,Amerika ya Kaskazini, Australia na New Zealand wana uzito wa juu

Katika ripoti yao wanasema licha ya tatizo la watoto kuzaliwa na uzito mdogo katika nchi hizo lakini kwa hakika ni la juu kwenye nchi za kipato cha juu barani Ulaya, Amerika Kaskazini, Australia na New Zealand. Katika maeneo ya wanaozaliwa na uzito mdogo wamesema kuwa katika maeneo hayo hakuna hatua madhubuti zimechukuliwa tangu mwaka 2000 kupunguza tatizo la watoto kuzaliwa na uzito mdogo, wakizingatia utafiti wao uliohusisha mataifa 148 na vizazi hai milioni 281,  kwa mujibu wa utafiti ambao umechapishwa katika jarida la masuala ya afya la Lancet. Hatua hizo hazijachukuliwa, ingawa kwamba mwaka 2012, mataifa yote 195 wanachama wa WHO waliazimia kupunguza kwa asilimia 30 idadi ya watoto wanaozaliwa na uzito mdogo ifikapo mwaka 2025 wakilinganisha na viwango vya mwaka 2012.

Bora kuchukua hatua za kukabili vichocheo vya watotokuzaliwa na uzito mdogo

Watafiti hao wanasema kwa kuzingatia takwimu za sasa ni vyema kuchukua hatua kukabili vichocheo vya watoto kuzaliwa na uzito mdogo. Vichocheo hivyo ni mwanamke kubeba ujauzito akiwa na umri mkubwa, kubeba ujauzito mfululizo, magonjwa ya shinikizo la damu wakati wa ujauzito, maambukizi kama magonjwa ya malaria, lishe duni, mjamzito kukumbwa na uchafuzi wa hali ya hewa, matumizi ya tumbaku na madawa ya kulevya.

Pamoja na hatua za kudhibiti vichochezi, watafiti hao wanataka kila serikali itimize ahadi hasa ile ya kuhakikisha kuwa kila mtoto anayezaliwa anapimwa uzito na huduma za kliniki zinaimarishwa. “Kila mtoto mchanga anayezaliwa anapaswa kupimwa uzito, lakini duniani hatuna takwimu za uzito kwa takribani theluthi moja ya watoto wachanga,” amesema hayo Julia Krasevec, mtaalamu wa takwimu na ufuatiliaji kutoka UNICEF. Pia ameongeza kusema kuwa “hatuwezi kusaidia watoto waliozaliwa na uzito mdogo bila kuboresha wigo na usahihi wa takwimu tunazokusanya.”

Inahitaji mfumo bora wa kukusanya data  ili kuwa na uzito sahihi

Akiendelea na ufufanuzi pia amesema kuwa iwapo kutakuwepo na mifumo bora ya kukusanya data, wanaweza kuwa na uzito sahihi wa mtoto wakiwemo wale wanaozaliwa majumbani na hivyo kutoa huduma bora zaidi kwa watoto wachanga na mama zao. Zaidi ya asilimia 80 ya watoto milioni 2.5 duniani wanaofariki dunia kila mwaka wanakuwa wamezaliwa na uzito mdogo kwasababu wanakuwa wamezaliwa kabla ya wakati.Watafiti hao wamesema mtoto anayezaliwa na uzito mdogo ambao wanaishi wana hatari kubwa ya kudumaa au kupata matatizo ya kukua kimwili na kupata magonjwa kama vile kisukari na moyo iwapo hawatapata matunzo bora.

16 May 2019, 13:53