Tafuta

Vatican News
Siku ya Muungano wa Afrika (AU) ni moja ya maonesho ya nini maana ya Ubuntu,utamaduni na mshikamano wa Afrika.Lazima kuipenda Afrika na kuungana kwa dhati Siku ya Muungano wa Afrika (AU) ni moja ya maonesho ya nini maana ya Ubuntu,utamaduni na mshikamano wa Afrika.Lazima kuipenda Afrika na kuungana kwa dhati  

Siku ya Afrika 2019:Nguvu za vijana zipewe kipaumbele katika enzi mpya ya maendeleo!

Katika kuadhimisha Siku ya Umoja wa Afrika AU mwaka 2019,nguvu za vijana wa bara hilo zipewe kipaumbele zaidi kwani zinaweza kuendeleza bara katika enzi mpya ya maendeleo endelevu.Ni kwa mujibu wa hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Guterres wakati wa kilele cha kutimiza miaka 56 tangu kuanzishhwa kwa Umoja huo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ilikuwa ni tarehe 25 Mei 1963 ambapo Afrika iliunda historia na msingi wa Shirika la Umoja wa Afrika wakati huo (OAU) ambayo baadaye kupewa  jina la Umoja wa Afrika (AU). Siku ya Afrika inalenga kusherehekea na kutambua mafanikio ya Shirika la Umoja wa Afrika (OAU ikiwa ya sasa AU), tangu kuundwa kwake ndani ya mapambano dhidi ya  ukoloni na ubaguzi wa rangi, pamoja na maendeleo ambayo Afrika imefanya hadi sasa. Hata hivyo pia ni kuonesha hata changamoto zake ambazo bara hili inakabiliana na suala ya Mazingira kwa ujumla katika dunia. Vile vile Siku ya Muungano wa Afrika (AU) ni moja ya maonesho ya nini maana ya Ubuntu, nini maana utamaduni na mshikamano wake wa Afrika kama asili. Kutokana na hilo ni lazima kuipenda Afrika na kuungana kwa dhati katika kuonesha kweli nini mzizi halisi wa Afrika. Kila mwaka katika maadhimisho hayo huongozwa  na kauli mbiu, kwa maana hiyo mwaka  2019  inaongozwa na kauli  ni “Afya Bora Inarefusha maisha".

Kauli mbiu ya mwaka 2019 ni kuamasiha juhudi ya pamoja katika maendeleo

Kauli mbiu hii inataka kuhamasisha pamoja na juhudi za maendeleo, katika kuboresha kila aina ya rasilimali za kibinadamu, kuanzis kilimo na utunzaji wa mazingira, kuwawezesha vijana kizazi kilichopo na kijacho cha  bara zima  la afrika kuendelea kulitazama bara kwa kina, kulipenda na kuelimika hasa kwa kuchukua majumu thabiti ya kuongoza mustakabali ya bara la Afrika! Vile vile maadhimisho haya ni pamoja na kuendelea kuimarisha mchango wa mwanamke mwafrika kama chombo muhimu kwa jamii zake na nguzo kwa mageuzi yake ya kiuchumi na utulivu wake, pamoja na  kuunganisha mielekeo ya kiutamaduni na kistaarabu kati ya nchi zote barani Afrika. Na zaidi kuuthibitisha utambulisho wa waafrika katika kuongeza misingi ya mshikamano wa kiafrika.

Nguvu za vijana wa bara la Afrika, zinaendeleza bara hilo kuelekea enzi mpya za maendeleo endelevu

Katika kuadhimisha kilele hiki cha maadhimisho ya Siku ya Umoja wa  Afrika naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres tarehe 25 Mei 2019 ametoa hotuba yake kwamba, nguvu na matumaini ya vijana isiyo na mipaka ya vijana wa kiafrika vinaimarisha bara hilo kuelekea katika nyakati mpya za maendeleo endelevu, sambamba na ushirikiano mpya kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU.

Hata hivyo mapema mwaka huu, Bwana Guterres alikuwa mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ambapo alitumia fursa ya  kukaa na wasichana wanafunzi kutoka katika mataifa 34 ya Afrika ambao wanajifunza masuala ya program za komputa. Bwana Guterres kwa kukumbuka wasichana hao amesema: “Hawakuwa wanaendeleza tu ujuzi wao; walikuwa wanatoa changamoto na kwa ubaguzi wa kijinsia na wanahamasisha ushirikishwaji katika teknolijia ya kidijitali ambayo itakuwa muhimu katika kulipeleka bara la Afrika katika mstakabali stahimilivu na wenye hewa kidogo ya ukaa.”

Siku ya Afrika inatimiza miaka 56

Siku ya Afrika inaadhimishwa ikiwa inatimiza miaka 56 ya kuanzishwa kwa Umoja wa nchi huru za kiafrika ambao hivi sasa ni Muungano wa Afrika yaani AU. Bwana Guterres aidha amesema, “tangu nilipotwaa madaraka mwaka 2017, nimeweka kipaumbele kwenye ushirikiano wa kimakakati kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika. Ninajivunia kusema kumekuwa na wingi wa ushirikiano wetu kuanzia katika kuimarisha kitaasoisi mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika hadi kwenyempango kazi mpya kati ya pande hizi mbili katika masuala ya amani, usalama na maendeleo endelevu, pamoja na maazimio ya pamoja ya ushirikiano katika operesheni za amani. Tunasaidia jitihada za AU katika kuzuia machafuko na pia katika maafikiano ikiwemo kunyamazisha bunduki ifikapo mwaka 2020.”

Kwa kutumia malengo ya pamoja ya kutokomeza umaskini

Kwa kutumia malengo ya pamoja ya kutokomeza umaskini, Katibu Mkuu amesema, Umoja wa Mataifa na AU wanafanya kazi pamoja katika kuimarisha Agenda ya mwaka 2030 na Agenda ya mwaka 2063 katika mipango ya maendeleo na kushirikiana katika kufungua fursa mpya kutoka katika eneo huru la biashara la Afrika. Amehitimisha kwa kusema ushirikiano wa kimkakati kati ya Umoja wa Mataifa na AU tayari umeanza kuleta matokeo na kwa hiyo: “hebu tujenge katika misingi hii imara ili kufanya ushirikiano wetu uwe na ufanisi zaidi, kupitia kuheshimiana na kutegemeana.”

27 May 2019, 12:07