Tafuta

Vatican News
Vyombo vya Habari kwa ajili ya Demokrasia:Uandishi wa Habari katika nyakati za kugushi,ndiyo kauli mbiu inayoongoza Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 Vyombo vya Habari kwa ajili ya Demokrasia:Uandishi wa Habari katika nyakati za kugushi,ndiyo kauli mbiu inayoongoza Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019 

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019,kwa ajili ya Demokrasia:Uandishi wa habari katika nyakati za kughushi!

Vyombo vya Habari kwa ajili ya Demokrasia:Uandishi wa Habari katika nyakati za kugushi,ndiyo kauli mbiu inayoongoza Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2019,itakayofikia kilele chake tarehe 3 Mei.Siku hii ilianzishwa kunako mwaka 1993 na mwaka huu nchini Ethiopia inakaribisha Siku hii Kimataifa!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 3 Mei 2019 Jumuiya ya Kimataifa,inaadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ikiongozwa na kauli mbiu: "Vyombo vya Habari kwa ajili ya  Demokrasia:Uandishi wa habari katika nyakati za utoaji habari za kughushi." Siku hii ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1993. Na wakati wa uwasilishaji wa siku hiyo mjini Paris tarehe 30 Aprili kwa waandishi wa habari wanasema:Uhusiano kati ya vyombo vya habari na demokrasia vitakuwa ni mada kuu katika toleo la mwaka huu 2019, kuhusu Uhuru wa vyombo vya habari kunako tarehe 3 Mei, siku iliyo andaliwa na UNESCO pamoja na  serikali ya Ethiopia na Tume ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa nchini Ethiopia, kuanzia 1 hadi 3 Mei 2019. Matukio zaidi ya mia moja yanatarajiwa kufanyika katika ulimwenguni pote katika fursa ya siku hii.

Uandishi wa habari unawezaje kugusa hisia dhidi ya habari za kugushi?

Je uandishi wa habari unawezaje kugusa hisia dhidi ya habari za kugushi wakati wa uchaguzi? Ni nini kinachopaswa kufanyika ili kukabiliana na mazungumzo ya kudhalilisha waandishi wa habari? Kwa kiasi gani kanuni za uchaguzi zinapaswa kutumika kwenye mtandao? Katika fursa ya Siku ya Uhuru wa Waandishi wa Habari kwa Mwaka huu,inayoongozwa na  kauli hii mbiu, “Vyombo vya Habari kwa ajili ya  Demokrasia, Uandishi wa Habari katika nyakati za kugushi ” itakuwa ni fursa ya kutafakari kwa kina mantiki hizi. Mkutano wa kitaaluma umefanyika Mei Mosi,  na  ambao umewasilisha utafiti mpya juu ya usalama wa waandishi wa habari. Huo unalenga kukuza mazungumzo kati ya watafiti na watendaji wa kisiasa wanaofanya masomo ya kawaida. Mkutano huo utazingatia usalama wa waandishi wa habari wa kike pamoja na wale wanaojikita katika masuala ya uchaguzi. Mpango huo pia unajumuisha Meza za miduara  inayojikita katika  majadiliano ya uandishi wa habari mtandaoni na pia suala la kusumbuliwa kwa waandishi wa kike na  tofauti vya kimantiki, hasa kwenye vyombo vya habari na uchaguzi katika Afrika na mageuzi ya vyombo vya habari nchini Ethiopia.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bwana Audrey Azoulay atafungua tukio kubwa la kuadhimisha sherehe pamoja na Rais wa Ethiopia 

Tarehe 2, Mei Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bwana Audrey Azoulay, atafungua tukio kubwa la kuadhimisha sherehe pamoja na Rais wa Ethiopia, Bwana Sahle-Work Zewde, Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika, Bi Vera Songwe  na Naibu Mwenyekiti  wa Tume ya Umoja wa Afrika, Amb Kwesi Quartey. Kwa jumla, zaido ya washiriki elfu moja wanatarajiwa, ikiwa ni pamoja na wawakilishi kutoka jamii ya kiraia, vyombo vya habari, vyama vya kitaalamu, vyuo vikuu na sekta ya haki. Sambamba na Vikao vinavyojihusisha  katika kuimarisha jukumu la vyombo vya habari na demokrasia na uchaguzi vitafanyika pamoja katika  mkutano huo. Miongoni mwa mambo muhimu yatakayofanywa na sherehe hizo ni kutoa Tuzo ya Uhuru wa vyombo habari na UNESCO / Guillermo Cano  jioni ya tarehe  2 Mei 2019. Watakapewa mbele ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, Audrey Azoulay na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Amb. Kwesi Quartey ni Waandishi wa habari wa Myanmar Kyaw Soe Oo na Wa Lone.

Wataalam wa habari, wanafunzi waandishi watakuwa na chumba maalum

Katika mkutano huo,chumba cha habari kitapatikana duniani kote kwa wataalam, vijana na wanafunzi waandishi wa kutoa ripoti juu ya shughuli za kila siku, na  duniani kote kutoa fursa kwa kizazi kijacho cha waandishi wa habari ili kukutana na wenzao kila kona ya dunia. Mwaka huu, UNESCO ilizindua Kampeni ya Kutetea Uandishi wa Habari ambayo inahimiza ushirikiano wake kwa vyombo vya habari ili kuwa na ruhusa ya kujieleza kupiti matumizi ya mabango na majukwaa ya digital. Ikumbukwe kuwa Siku ya Uhuru wa Waandishi wa Habari ulimwenguni ilitangazwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1993, kufuatia mapendekezo ya kikao cha 26 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO mwaka wa 1991. Siku hii inaadhimisha kanuni msingi za uhuru, inachunguza hali ya uhuru duniani kote, inalinda vyombo vya habari dhidi ya kujitegemea na hulipa kodi kwa waandishi wa habari ambao wamepoteza maisha yao wakiwa kazini.

01 May 2019, 15:25