Siku ya Kimataifa ya Familia inaadhimishwa tarehe 15 Mei ya kila mwaka:ni fursa ya kuchagiza uelewa wa masuala yanayoathiri familia ikiwemo kijamii kiuchumi na kidemografia Siku ya Kimataifa ya Familia inaadhimishwa tarehe 15 Mei ya kila mwaka:ni fursa ya kuchagiza uelewa wa masuala yanayoathiri familia ikiwemo kijamii kiuchumi na kidemografia 

Siku ya Kimataifa ya Familia:Msingi mkuu wa jamii ni Familia!

Tangu tarehe 15 Mei 1989 hadi 15 Mei 2019 ni miaka 20 tangu Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipoweka Siku ya Kimataifa ya Familia.Umoja wa Mataifa unasema licha ya kwamba muundo wa familia unabadilika ulimwenguni kote kufuatia mienendo ya kimataifa na mabadiliko ya demografia lakini bado Umoja huo unatambua familia kama kundi msingi katika jamii.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 15 Mei ya kila mwala ni Siku ya kimataifa ya Familia, ambayo ilizinduliwa rasmi na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1989 kwa lengo la kutoa kipaumbele juu ya masuala yote yanayohusu familia na jamii. Umoja wa Mataifa umetenga siku hii kwa ajili ya kutoa fursa ya kuchagiza uelewa wa masuala yanayoathiri familia ikiwemo kijamii kiuchumi na kidemografia. Siku ya  familia  inatoa fursa pia ya kujadili haki za kila mwanafamilia bila kujali hali yake ikiwemo watoto wenye  ulemavu wakila haina  hata wa ngozi ambao katika sehemu nyingi hasa barani afrika wamekuwa waathirika kiasi cha kupindukia kutokana na kasumba mbaya za ushirikina.

Mada kuhusu umuhimu wa familia leo hii ni muhimu sana

Je kwa miaka hii 20 tangu kuazaishwa kwa Siku hii ni jambo gani limebadilika ndani yake juu ya misingi ya familia? Mada kuhusu umuhimu wa familia leo na kama ilivyo asili na ina maana ya kusema kwamba ni familia ndogo na iliyo kubwa yenye kuwa na  matatizo, furaha na uchungu. Dunia ya Familia ndogo  ni mahali ambapo mtoto anazaliwa, anakua na mahali ambapo ni kuaandaa kukabiliana na dunia iliyo kubwa, yaani ile ya maisha na ile ya kijamii. Lakini katika familia tayari ni mahali ambamo kila mmoja yumo, anapata mambo ya kweli zaidi na msingi na mawazo ambayo yanastahili na ili si katika kuishi pekee ndani maisha yake mwenyewe bali kwa pamoja.

Ni vigumu na siyo rahisi kulipokea kuhusu mzazi anaye muuza mtoto ili auwawe

Hata hivyo kwa dhati ni vigumu kufikiria kama mtu, mwanaume, kijana  mwanamke, msichana anayependa kuishi pekee yake yaani kuibagua  kujifunga maana hali hiyo ni kuishi kama mtumwa, mwenye huzuni ndani ya sayari inayozunguka mtu. Na katika familia inayochanua na kutoa maisha ni pamoja na kutoa joto ndani ya familia yake na kuilisha wakati huo huo inalinda na kukuza. Ni vigumu kufikiria familia ambayo baba anamua kumuuza mtoto na ili auwawe kwa sababu ya kutaka fedha mbili, au familia ya baba na mama kushirikiana kwa pamoja kwa kumtelekeza mtoto wao kwa shilingi mia ili waweze kupata paa la nyumba, wakati hawajuhi mtoto huyo amekwenda kuishia wapi, kama biashara haramu, ukhaba, wizi na uhalifu… Siyo rahisi kufikiria  jambo hili linatendekea ndani ya familia, na wakati kumbe ndiyo habari inayosikika katika vyombo vya habari na kuripitiwa na Mamlaka ya Polisi kuhusiana na wazazi kuhusika katika mauzo na mauaji ya watoto wao!

Familia ndimi tunajifunaza kuanza kukaa,kutembea hadi kujifunza kupenda na kuteseka

Licha ya masuala ya tabia ya familia ya kisasa kujiingiza katika masuala machafu sana ya mauaji na uhalifu wa kila aina na kumbe katika familia ndimo tunapojifunza kutembea ndani ya umbu lenyewe la familia, mahali ambapo tunajifunza hata ya kwamba ya kukaa, kuzungumza, kutembea, kupenda na kuteseka. Na siyo mambo yote tunaweza kujifunza darasani kwa ajili ya kutambua  nini maana ya familia  kwa asili yake  lakini kwa urahisi kila familia kwa hakika ndicho kituo cha mapendo, maelewano, cha matatizo ya pamoja na namna ya kuyatatua kwa pamoja, ikiwa na maana ya kishirikishana kwa pamoja katika familia, kushindwa, kuanguka lakini pia kuinuka na kuteseka kwa pamoja. Na kama ndiyo hivyo basi ni  “ole” wake/wao anayemtupia mzigo mwingine licha ya tamaduni na kasumba za makabila fulani katika mabara, na ambamo kwa hakika yanaonesha udhaifu wa nini maana ya familia. Au au uhusiano kati ya watoto na wazazi wazazi wao, wakati mwishingie  kuishi bila kuheshimiana na wazazi wao, kaka na dada kwa pamoja, na wakati huo kuonesha hata matatizo kati yao, lakini ambayo kwa hakika kama  familia iliyo jengwa katika misingi ya kiutumaduni, kuna nyenzo kubwa ya msamaha ili kuweza kurudi katika msingi asili wa familia ya upendo, kiota cha upendo kama kuku awakusanyavyo watoto wake na kuwalinda.

Ndani ya famili ni mahali pa kukutana na watu wa kweli

Ni ndani ya familia mahali ambamo  unakutana na watu wa kweli wenye kuwa na moyo wa upendo, ukarimu na mshikamano,japokuwa na udhaifu wa kila mtu kwa maana sisi si wakamilifu lakini wanaojitahidi kuamka kila wanapoanguka, upendo unapokosa ndani ya familia, ndiyo majanga ya baadaye kwa ajili ya watoto, ndiyo mateso makubwa zaidi ndani ya familia lakini pia hata uhusiano wa jamii, kwa maana familia ni msingi, ni kiunganisha cha familia ya kinadamu na jamii yake inayozunguka. Katika ushirikiano wa pamoja  ndani ya familia ndiyo maana ya kukua katika matokeo mema ya mshikamano na kiungo kizima kinachounda familia, ile ya ukawaida, ya kazi , ya matumaini yanayotambua ndugu na si katika kutofauti kwa mtazamo wa udugo bali wa furaha kindugu. Katika familia ndimo chimbuko la maadili na namna ya kutofautisha kati ya mema na yaliyo mabaya kwa kadili ya misingi ya asili ya familia. Ndani ya familia ndimo pa kujifunza kupokea msamaha na kusamehe, kukarimu na kukaribisha, kunyosha mikono ya kusaidia na kukimbilia wengine…. Wema, fadhila, maadili vyote vinatokana na familia, mahali ambamo kweli wanaishi misingi halisi ya familia.

Siku ya kimataifa ya familia inatoa fursa ya kukumbuka misingi halisi

Katika fursa ya  siku ya kimataifa ya familia ni mwafaka katika  matukio ya kila namna hasa uwezekano wa kuhamasisha uwelewa wa matatizo na rasilimali zinazohusiana na mada hii nyeti na kubwa kwa kiasi chake. Kuhamasisha changamoto ambazo zimekumba familia kwa ujumla, kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, utandawazi na mitandao ya kijamii. Umoja wa Mataifa unafikiria Familia kama msingi wa kikundi cha kijamii na mazingira ya asili ya maendeleo na ustawi wa wote kwa maana ya kua kiungo kizima cha familia ambacho kinaweka katikati mtoto. Kati mada muhimu ambazo zimeweza kugusiwa kwa miaka 20 sasa tunakumbuka ile ya mshikamano kati ya familia, familia na kipeo cha uchumi, kipeo cha wanandoa, udhaifu wa wazazi katika kukuza watoto na mada nyingine ambazo zinaangazia familia kwa karibu. Nafasi kubwa pia inajionesha hasa umuhimu wa mababa katika kujikita ndani ya kiungo cha familia, nafsi ambayo kwa dhati inahitaji uwajibikaji mkuu na zaidi katika changamoto za kila siku. Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Siku hii ya Kimataifa ya familia,inpaswa kuwa tukio muhimu la kutambua na kutafakari kwa kina nafasi msingi ambayo familia inajikita ndani ya jamii ya kisasa na mzunguko wake wote katika syari. Lengo kwa maana hiyo ni kutaka kuweka chachu zaidi na kuona nafasi kuu ya familia katika mandeleo ya binadamu kamili na ili kutafuta namna ya upyaisho wa kutafakari kuhusu kushirikishana na siasa na suluhisho la matatizo kwa namna ya pekee ya familia ya leo hii.

Inasikitisha kuona kuwa hadi karne hii bado kuna ukatili dhidi ya wanawake

Kwa mtazamo wa familia kwa ujumla,kwa hakika inasikitisha kuona kuwa hadi kufikia karne hii pamoja na maendeleo ya mambo mengine bado kuna  ukatili wa kupindukia dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, ukatili unaoendelea kushika kasi kwenye baadhi ya maeneo mengi katika mabara  ya  sayari. Hivi karibuni imefanyika Siku ya wanawake duniani yaani tarehe 8 Machi na kwa mwaka huu Umoja wa Mataifa umengazia kuhusu uwezeshaji wanawake na usawa jinsia vitu ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya dunia kwa kuongozwa na kauli mbiu 2019 “fikra sawa, jenga kwa ufanisi na kuwa mbunifu kwa mabadiliko.  Lakini kuna umuhimu wa kujiuliza, mabadiliko hayawezi kuwapo kama hakuna jitihada. Wazazi na walezi hasa wanaume kuwajibika kikamilifu kwa kushirikiana na akina mama katika malezi bora ya watoto wao. Tunatambua kuwa katika taratibu za maisha ya jamii zilizo nyingi hasa kwa upande wa Afrika na kwingineko wanaume wana nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko, lakini zaidi pia ni wanawake kwa pamoja na  hivyo kama wanaume wana wajibu mkubwa sana katika kutokomeza ukatili unaokuwapo ndani ya familia.

Kuwajibika bila kutelekeza familia na watoto:mikakati ya maendeleo

Hadi leo hii bado kuna familia ambazo zina idadi kubwa ya watoto kiasi kwamba, kutokana na hali halisi kwa sasa wanashindwa hata kumudu gharama za kuwahudumia vyema watoto wao, kama vile kwenda shule  hali ambayo inafisha harakati za maboresho ya hali ya maisha ya familia nyingi. Tatizo jingine linaloendelea kujitokeza ni ndoa na talaka, zinazopelekea familia kuwa tenge, yaani, familia zinaoongozwa na mzazi wa upande mmoja, hali ambayo kimsingi imelta myumbo mkubwa kwa makuzi ya watoto , maadili na adhabu. Ubaguzi na ukosefu wa fursa sawa ni kasoro inayoendelea kujitokeza katika maisha ya familia nyingi, kiasi kwamba familia nyingi zinashindwa kukabiliana na kishindo cha maisha kwa kujiwekea mikakati ya maendeleo endelevu; ukosefu wa fursa za ajira, ukubwa wa familia, malezi tenge, ukata, magonjwa, ulemavu; ni kati ya mambo yanayoendelea kuathiri maendeleo ya familia nyingi duniani; kwa misingi ya kijinsia hasa kwa watu wanaoishi vijijini na makazi duni mijini. Familia za wageni na wahamiaji nazo zinakabiliwa na changamoto mbali mbali; hali ambayo inayojionesha pia katika familia zinazoishi kwenye migogoro ya kivita na kinzani za kijamii na kisiasa.

Wito kwa serikali zinazotunga sera za kisheria

Inatakiwa kwa kiasi kikubwa Serikali mbali mbali zijitahidi kutunga sera za makusudi kabisa kwa ajili ya kuzisaidia familia na kukabiliana na changamoto zake kwa kuzipatia ruzuku, hifadhi ya kijamii pamoja na kutoa kipaumbele cha kwanza kwa watoto wa kike katika masuala ya elimu na maendeleo yao. Aidha sera hizo zote kwa hakika ziweze kupania kuboresha maisha ya kifamilia, makuzi na elimu ya watoto, kama sehemu ya mchakato wa mapambano dhidi ya  umaskini wa kukithiri ambao unawaanda mamilioni ya watu duniani. Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kutoa changamoto kwa Serikali na wadau mbali mbali ili waweze  kuweka mikakati na sera zitakazoboresha maisha ya familia na ili familia hizi ziweze kuwajibika barabara katika malezi na makuzi ya watoto wao; kwa kuwasaidia wazee, ili kujenga jamii inayosimikwa mizizi katika uvumilivu, maadili  bora na heshima kwa utu wa mwanadamu. Hakuna nchi yoyote inaweza kuendelea bila kuwa na mambo hayo msingi ndani ya familia. Na familia ya kweli itayumba tu iwapo itakwenda kinyume na maadili asili na kadiri ya matakwa ya Mungu alivyoiumba!

15 May 2019, 15:27