Tafuta

Vatican News
Ripoti mpya ya Shirika la Afya duniani,inaonesha juu ya dharura ya magonjwa sugu ya madawa.Kwa hiyo ni dharura kwa maana kufikia mwaka 2050 watu milioni 10 watakufa Ripoti mpya ya Shirika la Afya duniani,inaonesha juu ya dharura ya magonjwa sugu ya madawa.Kwa hiyo ni dharura kwa maana kufikia mwaka 2050 watu milioni 10 watakufa 

Ripoti ya Umoja Umoja wa Mataifa na WHO kuhusu magonjwa sugu ya madawa!

Imetolewa ripoti ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu Magonjwa sugu ya madawa ambayo inaonesha dharura kufikia mwaka 2050 kwa maana kila mwaka kutakuwa na vifo vya watu milioni 10.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Magonjwa sugu dhidi ya dawa yanaweza kusababisha vifo milioni 10 kila mwaka kufikia mwaka 2050. Na matokeo ya uharibifu wa uchumi huo unaweza kufikia viwango vya hatari, sawa na yale yaliyosababishwa na mgogoro wa kifedha wa mwaka miaka miwili ya 2008-2009. Hata hivyo usugu wa chanjo za baktareia unaweza kupunguzwa kufikia mwaka 2030 katika  kutibu watu milioni 24  walio katika  hali ya umaskini uliokithiri. Ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu Magonjwa sugu dhidi ya madawa ambayo inaonesha dharura! Katika mtazamio wa dharura hiyo iliyomo katika ripoti yenye kauli mbiu “hakuna muda wa kusubiri: hakikisha usalama wa baadaye kutokana na maambukizi ya magonjwa sugu dhidi ya dawa”, imetarishwa na kuwasilishwa  Mei Mosi  na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu usugu wa chanjo, Kikundi shirikishi cha Shirika la Afya duniani (WHO), Shirika la chakula na kilimo, FAO pamoja na shirika la kimataifa la afya ya wanyama, (OIE).

Magonjwa sugu dhidi ya madawa husababisha vifo dunia laki saba kila mwaka

Kwa mujibu wa taarifa yao wanathibitisha kwamba inabidi kuzingatia kuwa  magonjwa sugu dhida ya madawa yanasababisha vifo dunia 700,000 kila mwaka na zaidi yaliyofanyiwa utafiti na maono katika ripoti  juu ya kuongezeka kwa kiwango cha usugu wa chanjo  na ambao unaonesha kwa dhati matatizo makubwa ya baadaye katika  kufikia malengo ya maendeleo elendelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa hasa kufikia hali halisi ya afya kwa wote; chakula salama na kupambana na utapiamlo; mifumo ya kilimo endelevu; maji safi na salama kwa wote, mifumo yote ya  usafi na  usafi wa mazingira. Ili kuweza kuepuka uwezekano mkubwa,  kama mgogoro wa usugu wa madawa, mashirika haya ya kimataifa, kwa kutambua uhusiano kati ya afya ya binadamu na ile ya wanyama, chakula na mazingira, wameazimia kuwa na lengo moja, liinaloitwa “Afya moja”.

Na ili kuweza kufikia hilo inahitajika hatua mpya ya kuzingatia na  matendo ya haraka tofauti. Vilevile wanasema kuwa usugu wa chanjo ni moja ya vitishio vikubwa  ambavyo tunapaswa kukabiliana navyo kwa pamoja kama  jumuiya ya kimataifa. Ripoti hii pia inatafakari kwa kina na upeo wa majibu yanayotakiwa ili kuweza kuzuia kuongezeka kwake na kulinda maendeleo kwa karne  katika kambi ya  afya. Haya yote yamesemawa na  Amina Mohammed, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na rais wa shirikisho la Kikundi hiki (IACG), ambapo wakati wa uwasilishaji wa Hati hiyo, ameonyesha wazi ni kwa jinsi gani hakuna muda wa kupoteza na kama ripoti inavyo hamasisha sehemu zote za wadau kuchukua hatua kulingana na ushauri unaotolewa, kufanya kazi kwa dharura ili  kulinda watu na sayari na kuhakikisha  wakati endelevu kwa wote” .

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kimataifa la  Afya ya wanyama (OIE) Bi Monique Eloit

Dhana ya “afya moja” imerudiwa kuchuliwa na Monique Eloit, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kimataifa la  Afya ya wanyama (OIE), ambaye ameelezea kwa jinsi gani ya utelekezaji wake ni lazima uhusishe jitihada za dhati na  ujasiri kwa  muda mrefu kwa upande wa  serikali na wadau wengine. Eloit pia amewaaalikwa mashirika yanayohusika kuwa sehemu yao ili kuhakikisha upatikanaji wa baadaye na ufanisi wa madawa haya muhimu.

José Graziano da Silva, Mkurugenzi mkuu wa FAO anasisitiza juu ya mapendekezo ya ripoti

Naye José Graziano da Silva, Mkurugenzi mkuu wa FAO, amejikita kuelezea  baadhi ya mapendekezo ya ripoti kuhusu matumizi  wajibishi ya chanjo katika sekta zote, huku akisisitiza majukumu muhimu katika kulinda uzalishaji wa chakula, usalama wa afya usafi  na biashara na kama ilivyo pamoja na afya ya binadamu na wanyama. Aidha Bwana Da Silva ameongeza kusema kuwa: “Nchi zinapaswa kutia moyo na kuhamasisha mifumo ya chakula endelevu na mazoezi ya kilimo ambayo hupunguza hatari ya usugu wa madawa kwa kufanya kazi pamoja ili kukuza njia mbadala kwa ajili ya matumizi ya madawa kama ilivyoelezwa katika mapendekezo ya ripoti.

Shirika la Kimataifa la Afya ya wanyama kwa upande wake, tangu mwaka 2016 ilikuwa tayari imeanza kukabiliana na tatizo. Ilikuwa amejiwekea miongozo ya matumizi sahihi ya chanjo iliyokuwa imechukuliwa kuwa muhimu ili mwishowe kulinda ustawi wa afya na binadamu na ustawi wa afya ya wanyama. Shirika lilikuwa linathibitisha wakati huo kuwa matumizi makubwa au yasiyofaa yanaweza kusababisha kuonekana kwa bakteria sugu katika matibabu na chanjo za kuzuia. Matukio hayo yanaweka kwa hakika hatari ya kudhibiti magonjwa duniani kote.

03 May 2019, 14:44