Tafuta

Kila tarehe 29 Mei ya kila mwaka ni Siku ya Walinda Amani duniani. Kuheshimu mashujaa wetu ndiyo mada ya iliyo chaguliwa kwa 2019 Kila tarehe 29 Mei ya kila mwaka ni Siku ya Walinda Amani duniani. Kuheshimu mashujaa wetu ndiyo mada ya iliyo chaguliwa kwa 2019 

Kuwaheshimu mashujaa wetu ndiyo mada ya Siku ya Walinda Amani duniani 2019!

Tarehe 29 Mei ni Siku ya Walinda Amani duniani.“Tunawaheshimu mashujaa wetu” ndiyo mada iliyochaguliwa mwaka huu 2019 katika fursa ya kusherehekea siku hiyo.Kunako tarehe 29 Mei 1948,Baraza la Usalama kwa Azimio n.50 iliomba kukomesha vita nchini Palestina na kuamua wanajeshi wanasimamiwa na wapatanishi wa Umoja wa Mataifa waliosaidiwa na kikundi cha kijeshi.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican News

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Azimio 57/129 la mwaka 2003 ulichagua tarehe 29 Mei  kusherehekea Siku ya Kimataifa ya walinda amani duniani. Ilikuwa ni siku kama hiyo  hiyo, kunako 1948, lianzishwa operesheni ya ulinzi wa amani ya kwanza ya Umoja wa Mataifa kwa kuipya jina la Shirika la Usimamizi wa Umoja wa Mataifa (UNTSO) ambapo ilianza shughuli za ufuatiliaji  wa amani mara moja nchini Palestina mnamo Juni mwaka huo huo. Kunako tarehe 29 Mei  1948, Baraza la Usalama  kwa  Azimio  n. 50 iliomba kukomesha vita nchini Palestina na kuamua kwamba wanajeshi wanasimamiwa na wapatanishi wa Umoja wa Mataifa waliosaidiwa na kikundi cha kijeshi ambacho kilikuwa na jukumu la kuwa na uangalizi kwa  namna ya pekee; na katika muktadha huo UNTSO ndipo ikazaliwa!

Mada ya Siku ya walinda amani 2019 : “kuheshimu washujaa wetu”

“Tunawaheshimu mashujaa wetu” ndiyo mada  iliyochaguliwa mwaka huu 2019 katika fursa ya  kusherehekea Siku ya Walinda Amani duniani. Ni mada ambayo kwa dhati inataka  kuwakumbuka wale wote waliojikita kutoa huduma na  hata sasa wanaendelea kutumikia katika kulinda thamani ya amani ulimwenguni. Na kupitia utume wa Umoja wa  Umoja wa Mataifa tangu kuanza operesheni za vikosi vya Umoja wa Mataifa kunako 1948 hadi leo watu 340,000 (wakiwa ni pamoja na  askari polisi, wanajeshi, maafisa wa utekelezaji wa sheria na raia) wamepoteza maisha yao wakati wa kutoa huduma ya kulinda amani katika nchi mbalimbali zenye mizozo ya kivita na matukio mengine ya asili.

Hata hivyo tangu mwaka wa 1948, operesheni 71 zimefanyika za kulinda amani, kwa sasa shughuli za operesheni ya ulinzi wa amani ni 16 katika mabara 4,  na kati ya operesheni inayo hitaji zana zaidi  na wafanyakazi wa kuajiriwa ni ile ambayo inaendelea katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) (MONUSCO) ambayo ina wasimamizi wa kuwajiriwa 22,492, na  kati yao ni  polisi, wanajeshi  na raia. Zaidi ya asilimia 95% ya utume wa zoezi lake ni kulinda raia na zaidi ya watu 600 katika operesheni 9 za walinzi wa amani wameajiriwa katika kuhamasisha na kulinda haki za binadamu.

Sherehe za Siku ya walinda amani Duniani nchini Italia imeadhimisha Brindisi

Shughuli za kulinda amani zinazohusisha askari wa Italia 1103 ni (MINUSMA) yaani Ujumbe wa Uimarishaji wa Umoja wa Mataifa katika utume nchini Mali na Nguvu ya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL). Nchini Italia, maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani duniani, yamefanyika tarehe 27 Mei 2019 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Brindisi. Tukio hili limewaunganisha baadhi ya Taasisi kuu za mafunzo ambazo wamefanya mitihani kuhusu mafunzo ya amani (BeLIeVE in PEACE). Wanafunzi kupitia kazi za kisanii au audiovisual wamealikwa kuwakilisha mada ya “Kulinda Amani”. Hata hivyo tarehe 19 Mei 2019 katika Makao ya Fao, Waziri wa Ulinzi  Bi Roberta Pinotti na Waziri wa Elimu, Vyuo Vikuu na Utafiti, wametoa tuzo kwa wanafunzi washindi kuhusu mada ya “Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Amani”, ambayo imefanyika katika  mantiki ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Washiriki waliwasilisha mitungo mbalimbali, mada, Video za multimedial, blogs na mitungo ya mashairi kuhusu  mada hiyo. Lengo la ushindani lilikuwa ni kuwafanya  vijana  wadogo na  wakubwa wawe na ufahamu kuhusu mchango mkubwa wa Misaada wanajeshi ambao ni walinda amani na utume wao katika maeneo mengi yenye vipeo vya kivita na hali halisi ngumu ya mazingira.

Nchini DRC kuna polisi 2,000 kutoka nchi mbalimbali ambao wanaunga mkono shughuli za Ujumbe UN

Katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani ambapo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL wanashirikiana na polisi nchini humo, PNC katika kuhakikisha ulinzi wa raia.  Nchini DRC kuna polisi 2,000 kutoka nchi mbalimbali ambao wanaunga mkono shughuli za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO wakifanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi wa raia hii ikiwa ndio wajibu mkuu wa polisi wa Umoja wa Mataifa kama anavyosema kamishna wa polisi, MONUSCO, Jenerali Awale Abdounasir. Askari polisi wa MONUSCO wameweka mikakati kuhusu mbinu za kutekeleza ulinzi wa amani. Wamebuni mbinu za kukabiliana na ukosefu wa usalama sehemu za mizozo  na hili linawawezesha kufanya kazi kwa karibu na vikosi vya polisi la taifa. Wamefanya kazi kwa pamoja kupunguza ukosefu wa usalama katika baadhi ya miji mashariki mwa nchi, ambako kwa pamoja wameanzisha mpango uliopewa jina SOLI ambao ulibuniwa na kutekelezwa na umepata mafanikio tangu mwaka 2018. Amesema Jenerali Awale.

Miji yenye faida na mkakati wa SOLI ni  Oicha,Beni,Goma, Bunia,Uvira,Kalemie na Bukavu

Miji ambayo imepata faida na mkakati wa SOLI ni Oicha, Beni, Goma, Bunia, Uvira, Kalemie na Bukavu. Mpango wa SOLI unatoa taarifa kwa wenyeji kuelewa kuhusu usalama wao na hutoa namba ambayo wanaweza kupiga iwapo kuna hofu ya usalama.  Kwa mantiki hiyo UNPOL na PNC wameweka ofisi katika maeneo mbalimbali kote nchini DRC kwa lengo hilo moja la ulinzi wa raia.  Jenerali Placide Nyembo Ngalusha kamishna wa polisi wa serikali ya DRC jimboni Kivu Kasakzini amesema kwamba hadi kufikia sasa, ushirikiano umekuwa na matokeo chanya kwa sababu katika ushirikiano huo kikosi cha taifa cha polisi kimekuwa ni mnufaika mkubwa. Kuhusu doria za pamoja na MONUSCO mjini Goma na  kwingineko, wamefanya kazi kwa pamoja kufanikisha SOLI katika kitengo cha kuratibu opereshen na katika kutoa mafunzo, na wananufaika na  UNPOL kutokana na ushirikiano na mafunzo yao.

30 May 2019, 10:45