Tafuta

Vatican News
Afrika imepongezwa kwa ukarimu wake hasa wa kupokea mamilioni ya watu wanaotafuta usalama wakikimbia vita na mateso hasa katika sehemu za migogoro ya kivita Afrika imepongezwa kwa ukarimu wake hasa wa kupokea mamilioni ya watu wanaotafuta usalama wakikimbia vita na mateso hasa katika sehemu za migogoro ya kivita  (AFP or licensors)

Afrika:Kuelekea katika suluhisho la kudumu kwa watu waliolazimika kutawanyika barani Afrika

Kuelekea katika suluhisho la kudumu kwa watu waliolazimika kutawanyika barani Afrika ndiyo kauli mbiu ya Mkutano maalum wa majadiliano ya Afrika kwa mwaka 2019 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York,uliofunguliwa tarehe 21-23 Mei 2019.Hata hivyo bara la Afrika linapongezwa kwa jitihada za ukarimu kama vile Uganda,Kenya,Tanzania na Ethiopia.

Afrika imepongezwa kwa ukarimu wake hasa wa kupokea mamilioni ya watu wanaotafuta usalama wakikimbia vita na mateso mengi hasa katika maeneo yenye mizozo na migogoro ya kivita. Hata hivyo idadi ya watu wanaotawanywa na kulazimika kukimbia makwao hadi kufikia mwisho kwa mwaka 2017 ilikuwa milioni 24.2  na kulibebesha  bara hilo mzigo mkubwa wa kiuchumi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 21 Mei 2019  na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya mshauri maalum kwa ajili ya Afrika UNOSAA, amesema nchi kama Uganda, Kenya, Tanzania na Ethiopia zimekuwa zikifungua milango yake kwa kiasi kikubwa kupokea wakimbizi, lakini ongezeko la jumla ya wakimbizi milioni 4.6 lililoshuhudiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2017 limeifanya Afrika kubeba mzigo isioweza  na siyo tu kwa upande wa kiuchumi bali pia kwa mazingira na mfumo wa maisha hasa kwa jamii zinazowahifadhi.

Kusaidia watu wasikimbie makwao kwa njia ya kutatua vyanzo vya umasikini na vita

Katika ufunguzi wa mkutano maalum wa majadiliano ya Afrika kwa mwaka 2019 ulioanza tarehe 21 Mei 2019  kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa kuongozwa na kauli mbiu “kuelekea suluhisho la kudumu kwa watu waliolazimika kutawanywa barani Afrika”. Naye  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema,“njia bora ya kuwalinda wakimbizi na wakimbizi wa ndani ni kuzuia wao wasikimbie makwao, na hii inamaanisha kwamba kushughulikia vyanzo ambavyo ni umasikini, vita, ubaguzi na ubaguzi wa aina zote.  Ufadhili wa fedha ni muhimu sana katika nchi zote hususan zilizoendelea ni lazima zitimize ahadi walizotoa ahadi kwenye mpango wa hatua wa Addis Ababa.” Mkutano ulioandaliwa na UNOSAA, Muungano wa Afrika (AU), shirika la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wengine unatoa fursa hiyo ya jukwaa la kujadili njia bunifu za ufadhili wa kutoka msaada wa kibinadamu kuelekea kwenye maendeleo katika nchi za Afrika zinazohifadhi wakimbizi na wakimbizi wa ndani. Mkutano huu pia unalenga kuchagiza msaada kutoka kwa viongozi wa Afrika katika kuhakikisha uridhiaji na upitishaji wa mikakati muhimu ya Afrika na kimataifa ikiwemo mkataba wa Kampala.

Hali ya watu kulazimika kukimbia makwao ni tishio la maendeleo endelevu

Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa Bience Gawanas akizungumza katika mjadala huo amesisitiza kwamba, “hali ya watu kulazimika kukimbia makwao Afrika ni inaleta tishio kubwa kwa maendeleo endelevu SDGs , na pia kufikia ajenda ya Muungano wa Afrika ya 2063. “Hatuwezi kufikia lengo la kutomuacha yeyote nyuma endapo hatutotafuta suluhisho la changamoto ya watu kulazimika kukimbia makwao. Nchi zinazohifadhi watu waliolazimika kukimbia zinabeba mzigo mkubwa na zinatoa fundisho katika dunia somo la kuwa na huruma na ukarimu.” Majadiliano hayo ya siku tatu yatakunja  jamvi  tarehe 23 Mei 2019 ambayo  yameweza kuwaleta pamoja viongozi mbalimbali na wawakilishi kutoka barani Afrika, Umoja wa Mataifa, Muungano wa afrika, mashirika ya kimataifa likiwemo shirika la UNHCR, asasi za kiraia, wakimbizi na wadau wengine wa misaada.

Mkataba wa Kampala 2009 wa Muungano wa Afrika (AU)

Hata hivyo katika hali halisi kuhusu wakimbizi, Afrika ndilo bara pekee duniani lililopitisha mkataba wa 2009 wa muungano wa Afrika (AU) kuhusu ulinzi wa wakimbizi wa ndani barani Afrika ujulikanao kama: “Mkataba wa Kampala” ambao unashughulikia tatizo la ukimbizi wa ndani unaosababishwa na vita, majanga ya asili na miradi mikubwa ya maendeleo Afrika. Hadi sasa nchi 27 za Afrika zimeridhia mkataba huo. Na katika  kusisitiza mtazamo wake kuhusu suala la watu waliolazimika kutawanywa,kunako  Julai2018 AU ilitangaza kuwa mwaka 2019 utakuwa “mwaka wa wakimbizi, watu wanaorejea makwao na wakimbizi wa ndani” ikiwa  chini ya kaulimbiu ya majadiliano ya mwaka huu. Na katika kuzingatia utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, lengo la Afrika ni katika kutafuta kwa namna moja au nyingine suluhisho  kwa ajili ya watu wanaotawanywa na wakati huohuo ikitafuta namna ya kuweza kuzuia migogoro na changamoto kubwa dhdi ya majanga ya asili.

21 May 2019, 14:43