Tafuta

Vatican News
Baada ya mwezi mmoja wa Kimbunga Idai nchini Msumbiji,Malawi na Zimbabwe, maisha ya watoto yako hatarini kwa mijibu wa UNICEF Baada ya mwezi mmoja wa Kimbunga Idai nchini Msumbiji,Malawi na Zimbabwe, maisha ya watoto yako hatarini kwa mijibu wa UNICEF 

UNICEF:Watoto ni waathirika wakuu baaada ya mwezi tangu kitokee kimbunga Idai

Mara baada ya mwezi mmoja tangu kimbunga Idai kiikumbe nchi za Msumbiji,Malawi na Zimbabwe,waathirika wakubwa ni watoto kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,UNICEF

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baada ya mwezi moja tangu kimbunga Idai kuzikumba nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, (UNICEF), limetoa ombi la dola milioni 1.6 ili kusaidia watoto kutoka na athari zilizosababishwa na kimbunga hicho. Unicef imesema watoto milioni moja nchini Msumbiji, 443,000 nchini Malawi na 130,000 nchini Zimbabwe wana mahitaji makubwa ikiwemo huduma ya afya, lishe, elimu na maji. Tangu kimbunga hicho kupiga Msumbiji, visa vya kipindupindu vimezidi kuongezeka kufikia hadi 4,600 huku visa vya malaria vikiripotiwa kuwa 7,500. Unicef imesema kusitishwa kwa huduma muhimu huenda ikasababisha mlipuko wa magonjwa na ongezeko la utapiamlo ambapo watoto wako hatarini.

Watoto wanaoishi katika makazi yaliyojaa watu wako hatari ya magonjwa

Akizungumza kuhusu hali ya watoto baada ya kimbunga hicho mkurugenzi mkuu wa UNICEF, Bi. Henritta Fore ambaye alitembelea  Msumbiji mara  tu baada ya kimbunga hususan katika mji wa Beira amesema, “watoto wanaoishi katika makazi yaliyojaa watu mbali mbali na makazi yao wako hatarini ya magonjwa, kutumikishwa na ukatili.” Na kuhusiana na mantiki ya huduma muhimu Bi. Fore amesema, nia ya  kuelekea kupona, itakuwa ndefu na ni muhimu kwa wadau wote wa kutoa misaada ya kibinadamu wahusike katika kila hatua.”

Takribani nyumba 200,000 nchini Msumbiji zimeharibiwa

Aidha Kwa mujibu wa Unicef, takriban nyumba 200,000 ziliharibiwa nchini Msumbiji tu na kwa sababu kimbunga hicho kilichotokea wiki chache tu kabla ya mavuno, uhakika wa chakula uko hali mbaya. Wakati huo huo, maelfu ya watu wanabaki bado  katika kambi za muda mfupi ambapo Unicef imeelezea wasiwasi wake kuhusu hatma ya watoto takriban 130,000 waliolazimika kuhama nchini Musumbiji na Malawi. Unicef imesisitiza umuhimu wa kusaidia watoto na familia kukabiliana na hali ya sasa na ili kurejeea katika maisha yao hapo baadaye. Unicef imetoa ombi la dola milioni 122 kwa ajili ya kusaidi watoto na familia walioathirika na kimbunga na athari zake nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kwa kipindi cha miezi tisa ijayo.

15 April 2019, 14:28