Tafuta

Vatican News
Ni miaka 25 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo inashukiwa watu lakini nane waliuwawa kinyama 1994! Ni miaka 25 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo inashukiwa watu lakini nane waliuwawa kinyama 1994!  (ANSA)

Ni miaka 25 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda

Jumapili tarehe 7 nchini Rwanda wanafanya kumbukumbu za miaka 25 ya mauaji ya kimbari.Inasemekana watu lakini nane,wengi wao wakiwa watutsi waliuwawa kwa kipindi cha siku mia moja tu.Licha ya miaka hii,lakini janga hili halijasahulika maana limeacha jeraha ndani ya roho za watu!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kila tarehe 7 ya  mwezi Aprili  ni  siku kumbukumbu ya mauaji  ya kimbari iliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda, ambapo kila mwaka Rais Paul Kagame huwasha mwenge wa kumbukumbu katika  Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari kwenye mji mkuu wa Kigali katika eneo linaloaminika kuwa zaidi ya waathirika 250,000 walizikwa hapo. Siku hii ndiyo mwanzo wa madhimisho ya kumbukumbu hizo na mabzo zinakuwa na  matukio kadhaa yanayo dumu kwa siku mia moja zijazo, na ambazo zilitengwa kwa makusudi ya maombolezo ya nchi nzima.

Tukio la mauaji ya kimbari yalianzishwa na  na kikundi cha watutsi waliokuwa wamekimbia nchi yao kwa  kuunda vuguvugu waliloliita RPF ambalo lilivamia Rwanda mwaka 1990, na huku vita vikiendelea hadi mwaka 1993 ambapo makubaliano ya amani yalifikiwa. Lakini usiku wa terehe 6 Aprili mwaka 1994, ndege iliyokuwa imewabeba hayati Rais Juvenal Habyarmana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira ilitumbuliwa. Kila mtu aliyekuwa katika ndege alipoteza maisha , na ndiyo ukaanza vurugu za kusikitisha sana! Japokuwa miaka 25 imepita, lakini yaliyotokea yameacha mabaki na majeraha. Ni tukio ambalo halitasahulika nchini Rwanda, kwa walio guswa na mkasa, baba, kaka, mama, ndugu, jamaa, marafiki na kwa ujumla nchini Rwanda hakuna familia hata moja iliyobaki bila kuguswa na mkasa huu.

Hii ni wazi kwamba wengi wanaendelea kuishi na kuhisi matokeo ya mauaji ya kimbari ambapo unakuta baadhi ya watu wametengwa na familia zao au labda hata hawana familia, japokuwa na kuanzisha michakati ya kina ya upatanisho. Wahalifu, waathirika, hata wale ambao hawakuwa wamezaliwa wakati huo, kwa pamoja wote wanakabiliwa na matokeo hayo sawa, maaha ni hisotria ya nchi na imegusa  jamii ya kibinadamu na kuacha majeraha makubwa. Licha ya hayo mauaji haya yalisababisha hata kukaibuka wimbi la wakimbizi  kukimbilia katika nchi za jirani zaidi ya milioni tatu waliotaka kusalimisha maisha yao na zaidi ya watu laki moja na ishirini kuwekwa gerezani wakisubiri kesi zao ziweze kusikilizwa na hatimaye kutolewa uamuzi. Lakini cha kusikitisha pia ni wale ambao walikuwa tayari wana hata uraia nchi za karibu, kwa Mfano Tanzania, na ambao waliweza kuingia nchini mwao, na kwa bahati mbaya nao wakabaki ni waathirika pia. Ni historia ya kutia mbayo haitasahulika kamwe.

Hata hivyo Kanisa Katoliki bado limeendelea kuwa mstari wa mbele katika mchakato wa upatanisho, haki na amani kwa kutumia Tume za Haki na Amani. kama ilivyo hata nchi jirani ya Burundi, Kanisa pia linaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuwa ni chombo cha upatanisho, haki na amani. Hii ni dhamana endelevu inayopaswa kusimikwa katika majiundo ya dhamiri nyofu, uwekezaji katika maisha ya vijana kwa njia ya elimu na fursa za ajira ili waweze kujitegemea pamoja na kuhamasisha mwingiliano wa vijana katika nchi mbali mbali ili kujenga umoja na mshikamano. Ni lazima katika nchi kuwafikiria vijana wa sas ana endelevu ili kweli waweze kudumisha utu, kwa kupinga vikali tabia za kibaguzi, kikabila na hali halisi ya utamaduni wa nchi mahalia. Hata hivyo katika  kipindi  cha miaka 25 bada ya mauaji ya kimbari  nchini Rwanda imebadilika tangu. Kwa sasa Rais Paul Kagame ndiye anayesifiwa kwa kusimamia maendeleo ya haraka ya kiuchumi baada ya mauaji kumalizika. Mafanikio yake yamempatia umaarufu kama kiongozi wa kuigwa katika bara la Afrika, hata kama bado kuna badhi ya kupinga misimamo mingine ya kwake, lakini kwa hakika Rwanda kwa sasa ni moja ya nchi zinazoongoza hata katika ngazi ya Teknolojia ya Habari na sera ya uwekezaji ya maendeleo ya kidijitali nchini.

Kunako mwaka 2017 Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) lilita Rwanda kama moja ya mifano ya mafanikio ya maendeleo katika Intaneti barani Afrika. Wakati wa Kongamano la Kiuchumi Duniani lililofanyika mjini Davos, nchini Uswisi, kuanzia tarehe 17 - 20 Januari, 2017, Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu Sayansi na Utamaduni (Unesco) aliitaja Rwanda kama moja ya mifano ya mafanikio katika maendeleo ya intaneti duniani. Kiongozi huyo alitolea wito nchi nyingi ambazo bado zina kiwango cha chini kwa matumizi ya Intaneti kuiga mfano wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa kuungana na kuboresha mazingira ya maisha ya watu bilioni 3.9 ambao bado hawafajafikia hatua hii.

Vile vile ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya ngazi zote za serikali umeiweka pazuri nchini Rwanda. Hayo yalithibitishwa na mwakilishi wa Rwanda Bi Emma Rubagumya mbunge na  mwanakamati wa Kamati ya masuala ya jinsia katika Bunge la Rwanda  akiwa anaiwakilisha nchi yake kwenye mkutano wa  63 wa Kamisheni ya hali ya wanawake CSW mjini New York, Marekani. Akihojiana na mwandishi wa habari alisema:  “Sisi kama wanawake tunapokuwa wengi katika ngazi za kufanya maamuzi,  inakuwa rahisi kwetu kwamba kila maamuzi yanayofanywa serikalini basi huwa wanawake wameweka mchango   wao ambao unatoka kwenye kujua matatizo hasa  yanayowakabili wanawake”.

06 April 2019, 14:03