Tafuta

Vatican News
Itachukua muda mrefu kukarabati mji wa Beira nchini Msumbiji ulioharibiwa na kimbunga Idai na hivyo mshikamano wa dhati unahitajika Itachukua muda mrefu kukarabati mji wa Beira nchini Msumbiji ulioharibiwa na kimbunga Idai na hivyo mshikamano wa dhati unahitajika  (AFP or licensors)

Kimbunga Idai Msumbiji:Caritas Italia na msaada wake wa dharura

Taarifa kutoka ofisi ya Caritas nchini Italia katika kitengo cha Afrika wanasema,baada ya mwezi mmoja wa tukio la kimbunga Idai nchini Msumbiji,Zimbabwa na Malawi,hali halisi ya ukarabati bado ni ngumu.Inatakiwa mshikamano wa kuendelea na ambao tayari utazame leo,kesho na kesho kutwa!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya mwezi mmoja wa kimbunga kilicho ikumba eneo kati ya Msumbiji, Zimbabwe na Malawi, takwimu za majanga hayo japokuwa ni za muda, kwa bahati mbaya bado zinaonesha kuwa na hali mbaya sana. Ni uthibitisho wa taarifa kutoka Ofisi ya Caritas nchini Italia katika kitengo cha Afrika, kwamba mfano Msumbiji tu, karibia milioni moja ya watu wamekufa na bado mamia kupotea, nyumba 240,000  kuharibiwa na  hekali 500,000 za ardhi kusombwa na maji. Caritas ya Baraza la Maaskofu nchini Italia ilitoa mara moja mchango wa Euro milioni moja ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi fulani cha dharura katika jitihada za kukarabati na kuweka sawa baadhi ya miji haribifu.

Utakuwa vigumu kurudisha hali halisi mapema na kwa haraka

Kimbunga Idai kilikumba maeneo hayo ya nchi za Afrika na kwa namna ya pekee katika mji wa Beira, mji  mkubwa wa pili katika nchi ya  Musumbiji, anasema Fabrizio Cavalletti Mhusika wa  Ofisi ya Caritas Nchini Italia, katika kitengo cha Afrika. Asilimia 90 ya makazi ya watu na majengo yao katika forodha ya mji huo yameharibika sana na mengine kusombwa na maji. Kwa hakika ni kusema, itakuwa ni vigumu kuweza kurudisha hali halisi mapema, hivyo ni kazi ngumu ya kuweza kukarabati mji huo. Na hiyo ni kutokana na kwamba hadi sasa maji bado yanaendelea  kukauka kwa taratibu sana, hasa katika ardhi tambarare na maji mengi yametuhama. Hali hii imekuwa pia hatari sana kutokana na mlipuko wa kipindupindu  kilichosababishwa na hali hizi za ukosefu wa usafi kwa njia ya mafuriko, hata kuongezeka kesi za malaria.

Inahitaji mshikamano wa kuendelea na wa dhati

Akiendelea kufafanua juu ya janga hili anasema, suala ambalo liko ndani ya moyo wao kama mratibu wa ofisi wa kitengo cha Afrika katika Caritas Italia ni kutafuta msaada, ili kusaidia Caritas mahalia na hali halisi nyingine ambazo zinahitaji msaada wa haraka zaidi. Dharura hiyo ni kama vile ugawaji na usambazaji wa turubali  zisizo pitisha maji, makao ya dharura, vifaa vya afya na  vifaa vya matibabu, msaada kwa watu waliorundikana  na chakula. Lakini kuna pia haja kubwa ya kuhitaji mshikamano unaopaswa uendelee wakati huu na ambao tayari utazamie leo hii, kesho na kesho kutwa. Kimbunga kwa hakika kimesababisha madhara makubwa mno ambayo itachukua muda mrefu kukarabati. Na zaidi mazao yameharibiwa, kwani ilikuwa ni kipindi cha mavuno, miundombinu imeharibiwa na nyumba zimeharibiwa. Kwa namna hiyo  kutakuwa na haja ya jitihada kubwa za ujenzi na ukarabati, pia kwa sababu, jamuiya hizi tatu katika nchi tatu, zilikuwa tayari zimeathiriwa  sana na umasikini. Kadhalika amefafanua kuwa hiki siyo kimbunga tulichozoea kuona katika nchi za Korea, Italia, Ulaya au Marekani, lakini ni nchi ambazo kwa hakika, tayari zilikuwa na hali ngumu ya umasikini, kuongezeka hii inazidisha wasiwasi mkubwa, anasema kwa uchungu Mratibu wa Caritas nchini Italia.

Mazingira kuharibika mara mbili

Hatuwezi kuficha lolote anaongeza kusema, japokuwa na uwajibikaji wetu. Ni wazi kwamba vimbunga hivi haviwezi kuwa vimejitokeza kutokana tu na mabadiliko ya tabia nchi, bila kuwapo na mkono wa mwanadamu  na ambapo matokeo mabaya ni kwa nchi masikini sana na ambao kwa hakika hawakuchangia hata upashaji wa dunia joto! Ni suala lisilo la haki na ambalo lingeweza kufikiriwa zaidi hasa wanapozungumza juu ya majanga haya kwa wadau wa kutetea mazingira. Ni mazingira ambayo yameharibiwa mara mbili, umasikini na majanga ya asili.

20 April 2019, 09:48