Tafuta

Vatican News
Kuna ongezeko la wasiwasi juu ya ukosefu wa vyakula katika mataifa duniani kwa mujibu wa FAO na WFP Kuna ongezeko la wasiwasi juu ya ukosefu wa vyakula katika mataifa duniani kwa mujibu wa FAO na WFP 

Amani na maendeleo vinahitajika kusaidia zaidi ya watu milioni 100 wathirika wa njaa

Fao,Wfp na Umoja wa nchi za Ulaya wamewakilisha Ripoti kamili huko Bruxelles juu ya kipeo cha vyakula.Milioni 113 ya watu katika nchi 53,wameteseka mwaka 2018 kwa njaa ya kukithiri,migogoro ya kukithiri,ukosefu wa msimamo kijamii na mabadiliko ya tabianchi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Ongezeko kubwa la watu wanaoteseka kwa njaa duniani inaendelea kupewa nafasi ya kwanza katika magazeti mengi duniani, lakini pia majibu ya yanatafutwa ili kutoa suluhisho mbadala katika hatua za mchakato wa kambi za jumuiya ya kimataifa. Katika mkutano tarehe 4 Aprili njini Bruxelles wameunganika wawakilishi 400 kutoka katika serikali, mashirika ya kitaifa na kimaitafa, mashirika yasiyo ya serikali, vyama vya wakulima pamoja na sekta binafsi ikiwemo wataalam wa dunia kwenye mkutano unaongozwa na tema “chakula na kilimo katika kipindi cha kipeo”. Tukio hili limekaribishwa katika makao makuu ya Tume ya Ulaya na kuandaliwa na Mtandao wa dunia dhidi ya kipeo cha vyakula,ambao unajihusisha na mashirika ya kibinadamu na maendeleo na  kati yake ikiwemo Umoja wa Ulaya, FAO na WFP, mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yanayo jikita kupambana dhidi ya njaa duniani.

Migogoro ni sababu msingi wa ukosefu wa chakula

Katika fursa hiyo wamewakilisha Ripoti kamili kuhusu kipeo cha vyakula  ambapo ripoti inaonesha wasiwasi mkubwa juu ya ukosefu wa usalama wa vyakula unowakumba hadi leo hii, milioni ya 821 ya watu katika sayari nzima. Hii  ni ripoti ya Fao, kuanzia mwezi Septemba 2018 ambayo inathibitisha kwamba, milioni 143 ya watu katika nchi 42 wako chini ya kiwango cha njaa ya kukithiri na ambapo ipo hatari za maisha na watu, na milioni 113 ni wale ambao wameshambuliwa na kipeo kibaya cha vyakula katika nchi 53, ukilinganisha na milioni 124 za watu kwa mwaka 2017 ijapokuwa hali hii imebaki bila mabadiliko au ongezeko katika mataifa 17 duniani.

Aidha katika Ripoti inaonesha kwamba, 2/3 ya watu waliokumbwa na njaa ya kukithiri ni nchi 8 katika bara la Afrika na Asia: Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, Nigeria, Sudan Kusini, Sudan, Siria na Yemen. Na karibu milioni 30 ya watu waenye njaa kali ni kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi na majanga ya asili. Ripoti hata hivyo inaonesha  nchi  nyingine 13 na kati ya hizo, kuna  Korea ya Kaskazini na Venezuela wenye kipeo kibaya cha vyakula, ambao wameweza kutoa taarifa zinazohusu nchi zao. Ripoti inasisitiza juu ya kuwekeza na kwa ajili ya amani ya kudumu na ndiyo wito mkuu wa jumuiya za Kimataifa ili kuweza kushirikishana jitihada zote, kuzuia na kutoa jibu la lazima katika dharura, aidha kutoa sababu, lakini yote hiyo inahitiji uwekezaji mkubwa katika kupinga migogoro kwa ajili ya  amani endelevu.

05 April 2019, 15:50