Tafuta

Vatican News
Unicef inasemamaelfu ya watoto wenye ulemavu katika kanda za Ulaya Mashariki wanabaki katika shule maalum ambazo zimetengwa kwa ajili yao tofauti na wenzao na jumuiya zao Unicef inasemamaelfu ya watoto wenye ulemavu katika kanda za Ulaya Mashariki wanabaki katika shule maalum ambazo zimetengwa kwa ajili yao tofauti na wenzao na jumuiya zao 

Asilimia 75 ya watoto bara la Ulaya ya kati,Asia mashariki hawapati mafunzo bora!

Tamko la Shirika la Kimataifa la kusaidia watoto UNICEF katika taarifa yake tarehe 7 Machi 2019 iliyotolewa mjini Geneva inasema kuwa japokuwa na ukosefu wa takwimu kamili, lakini inaonesha ni kwa jinsi gani kuna milioni ya watoto wenye ulemavu ambao hawajawahi kwenda shule katika Bara la Ulaya ya kati, Mashariki na Asia Mashariki

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Zaidi ya asilimia 75 ambayo ni karibia milioni 51 ya watoto wanaishi na ulemavu katika Bara la Ulaya ya Kati na Mashariki ya Ulaya na wakati huo ni watoto ambao wamebaguliwa na mafunzo kamili na ubora. Ni tamko la Shirika la Kimataifa la kusaidia watoto UNICEF katika taarifa yake tarehe 7 Machi 2019 iliyotolewa mjini Geneva.

Unicef inasema kwamba japokuwa na ukosefu wa takwimu kamili, lakini inaonesha ni kwa jinsi gani kuna milioni ya watoto wenye ulemavu ambao hawajawahi kwenda shule. Na wale ambao wameandikishwa, UNICEF inabainisha kuwa upo uwezekano mdogo wa kuendelea na mafunzo ya elimu ya msingi au Sekondari  na wakati huo huo maelfu na maelfu ya watoto wenye ulemavu katika kanda wanabaki katika shule maalum ambazo zimetengwa kwa ajili yao tofauti na wenzao na jumuiya zao.

Kwa maana hiyo kuna hali halisi isiyoelekezeka kwa watoto hawa na familia zao, uchumi kitaifa na kijamii anaeleza Afshan Khan, Mkurugennzi wa UNICEF kanda ya Ulaya na Asia ya Kati. Leo hii Unicef imewekeza ili kuwawezesha kuwa na  ubora na upatikanaji wa wa zana za kiteknolojia ya kuwasadia kwa maana kuna ongozeko la idadi ya watoto ambao hawawezi kwenda shule na wakati ni haki yao msingi wa kupata mafunzo.

Teknolojia ya kuwasaidia ni kama vyombo maalum vya kusoma na tablet, viti vyene magurudumu vya kukalia ili wasome na ambavyo kwa hakika vinauzwa bei ghari na hata vile vya teknolojia vya kutumia computer ya ubongo, vyote hivyo ni vifaa ambavyo vinaweza kuwasaidia watoto wenye ulemavu ili waweza kujitegemea na kuudhuria masomo , hya maisha ya kawaida katika jumuiya. Na katika nchi zenye kiwango cha chini, inaonesha kuwa watoto ambao hawakuweza kwenda shule ni kuanzia asilimia 5-15%.

08 March 2019, 16:27