Tafuta

Bwana Michel Sidibé  amenukuliwa akisema  kuwa kwamba kupata tiba ya Virusi vya ukimwi ni ndoto ya mwisho.Ingawa hatua hii bado ni ngumu na kazi kubwa zaidi inahitajika Bwana Michel Sidibé amenukuliwa akisema kuwa kwamba kupata tiba ya Virusi vya ukimwi ni ndoto ya mwisho.Ingawa hatua hii bado ni ngumu na kazi kubwa zaidi inahitajika 

Utafiti mpya wa kisayansi kuhusiana na uwezekano wa tiba ya ukimwi!

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya virusi vya ukimwi,UNAIDS lionesha kutiwa moyo na ripoti iliyochapishwa tarehe 5 Machi 2019 mjini Seattle Marekani na Geneva Uswisi ya mgonjwa aliyekuwa na ukimwi kuponywa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya virusi vya ukimwi,UNAIDS  limethibitisha  kutiwa  moyo na ripoti iliyochapishwa tarehe 5 Machi 2019  mjini Seattle Marekani na Geneva Uswisi ya mgonjwa aliyekuwa na ukimwi kuponywa. Kwa mujibu wa UNAIDS mwanaume huyo alikuwa akipewa tiba tangu mwaka 2016 na wataalamu katika Chuo Kikuu cha London na Chuo Kikuu cha Imperial kinachohusika na magonjwa ya saratani.

Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Bwana Michel Sidibé  amenukuliwa akisema  kuwa kupata tiba ya Virusi vya ukimwi ni ndoto ya mwisho. Ingawa hatua hii bado ni ngumu na kazi kubwa zaidi inahitajika, inatupa matumaini makubwa kwa siku za usoni tunaweza kuumaliza ukimwi kwa njia za sayansi kupitia chanjo au tiba. Hata hivyo inatuonesha ni kiasi gani bado tuko mbali kufikia hapo, pia umuhimu wa kuendelea lijikita katika juhudi za kuzuia virusi vya ukimwi na kutibu.

Taarifa ya UNAIDS ikifafanua kuhusu hatua ya sasa, imesema upandikizaji wa seli ni jambo gumu, tete la gharama na lenye athari zitokanazo na tiba hiyo kiasi cha kutokuwa njia inayoweza kuwatibu watu wengi walio na virusi vya ukimwi. Hata hivyo inaelezwa kuwa matokeo ya sasa yanatoa mwelekeo mzuri kwa watafiti wanaoshughulika na virusi vya ukimwi na pia kuonesha umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika utafiti wa kisayansi dhidi ya Virusi hivyo.

Matokeo haya yametangazwa katika kongamano lililofanyika mjini Seattle Marekani linalohusu virusi vyenye tabia ya kujibadilisha ndani ya mwili ili kijifananisha na hali halisi ya mwilini ili viweze kuzaliana na kushambulia viungo vya asili kama seli. Matokeo ya mgonjwa ya kwanza kabla ya haya ya sasa, yalikuwa ya Timothy Ray Brown ambaye alipokea matibabu ya saratani mwaka 2007.

Hata hivyo tarifa ya UNAIDS imesisitiza kuwa ulimwengu ni lazima utambue kuwa hivi sasa bado hakuna tiba ya Virusi vya ukimwi. UNAIDS inafanya kazi kuhakikisha watu wote wanaoishi na walioathirika na virusi vya ukimwi wanapata huduma za dawa za kurefusha maisha na matibabu. Takwimu zinaonesha mwaka 2017 kulikuwa na watu milioni 36.9 waliokuwa wakiishi na virusi vya ukimwi  na watu milioni 1.8 walipata maambukizi mapya huku katika mwaka huo huo takribani watu milioni 1 walikufa kutokana na magonjwa yaliyohusiana moja kwa moja na Ukimwi.

06 March 2019, 14:26