Tafuta

21 Machi ni siku ya kimataifa dhidi ya ubaguzi 21 Machi ni siku ya kimataifa dhidi ya ubaguzi  

Tarehe 21 Machi ni siku ya kimataifa dhidi ya ubaguzi

Tarehe 21 Machi ni siku ya kimatafia dhidi ya ubaguzi,ambapo Umoja wa Mataifa na Unesco wanatoa mwaliko kwa mataifa yote kupambana na itikadi kali zinazo hamasisha ubaguzi na uchochezi ili kwa pamoja kusema hapana ubaguzi kutokana na kwamba tatzio hili linaenea kwa kasi duniani na linahitaji mpango wa kivitendo na siyo ya kinadharia

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika masuala ya haki za binaadamu kinachosimama usoni kabisa ni haki na usawa kwa kila binaadamu. Ubaguzi si jambo geni, kwani umekuweko wakati wa ukoloni barani ulaya na hata wakati wa enzi ya biashara ya utumwa, walipovushwa na kupelekwa bara la Amerika. Kuna hali ya ubaguzi katika jamii ya nchi zote kuanzaia magharibi, masharikia, kusini na kaskazini kutokana wakati mwingine na  udhaifu wa mkakati wa kisiasa na sheria katika vita dhidi ya ubaguzi katika nchi husika. Ukitazama suala la kuhusu umuhimu wa kulishughulikia tatizo hilo waandishi wengi, na watu maarufu sana wakiwa wa kidini au wanasisasa hai wameweze kuelezea hali halisi. Lakini suala hili la ubaguzi limekuwa kweli gumu sana. Kwa kukumbuka Kongamano la kimataifa dhidi ya ubaguzi lililofanyika katika mji wa bandari wa Durban nchini Afrika kusini kunako mwaka 2001, ilisisitiza kwamba ili kupambana na ubaguzi ambalo limegeuka tatizo la dunia nzima, panahitajika mpango wa kivitendo wa pamoja duniani na siyo wa kinadharia.

Fikiria tangu miaka mwaka 2001 hadi leo hii je ni kitu gani kimeweza kufanyika? Katika bara la Afrika ambako miaka iliyopita imeshuhudia vita katika nchi kadhaa barani humo, ikiwa chanzo cha baadhi ya migogoro ni tafauti za kikabila. Huko Zimbabwe kwa mfano kumekuweko na hisia za kibaguzi dhidi ya wakulima wakizungu kutokana na umasikini na ukosefu wa ardhi kwa waafrika walio wengi, hadi  kufikia ya Afrika kusini kugeuka kuwa mhanga wa ubaguzi wa wachache dhidi ya walio wengi, na zaidi pia wahamiaji. Kwa kuthibitisha mfano huo wa kibaguzi ni wiki iliyopita,Askofu Mkuu wa Johnanessburg katika ujumbe wake wa Kwaresima 2019 amesema: “Mji wa Johannesburg ni mama gani? Je hupaswi kuwa kama mama ambaye hukusanya watoto wake wote? kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake!” (Mathayo 23:37). Kwa maana hiyo ni mantiki inayotazama moja kwa moja ishara za kiubaguzi, licha ya wahamiajia na wakimbizi, lakini hata wazalendo ambao wanakimbilia miji na kukosa mahala pa kulala na kutengeneza mtaa wa mabanda, ambamo maisha ya watu hao ni mabaya sana yasiyo na hadhi ya kibinadamu.

Mara nyingi taasisi ya haki za binadamu, imekuwa ikizungumza sana, hasa juu ya chuki dhidi ya wageni ambayo kwa kiasi chake imepindukia, watu wageni wanabaguliwa sana. Hiyo pia ni kutokana na sura tofauti, rangi za ngozi au jina la lugha nyengine, kwa hakika wageni wanabuguliwa. Miongoni mwa wanadamu hata katika nchi nyingine ambazo huwezi kufikiria wanabaguliwa, wakati mwingine siyo tu kwa kwa kuwa ni wahamiaji wenye utamaduni tafauti, bali kuna ubaguzi wa aina nyengine kwa mfano katika kupata nyumba au ajira, lugha au hata katika viwanja vya kandanda.

Kwa kutazama hali halisi hiyo ni  kweli unaona umuhimu kabisa wa siku ya Kimataifa ya kupinga ubaguzi ambayo inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 21 Machi. Kwa kutazama mifano hai, tunaona nchi nyingi zikitengeneza hata mikakati ya kitaifa ya kupiga vita ubaguzi, kama inavyotakiwa, lakini mara nyingi mikatati hiyo ni kama inaishia hewani, maana hata viongozi wengine wa kisiasa ndiyo wako mstari wa mbele kuchoche chuku. Kwa maana  hiyo tunaweza kukiri kabia kwamba ubaguzi ni tatizo la dunia nzima. Ubaguzi huo pia unashamiri sana katika bara la Asia na Mashariki ya kati jambo ambalo linatishia maisha ya binadamu,kuanzia lugha, kabila dini na rangi. Mwisho wa ubaguzi huu utaishia wapi, kwa maana upo ubaguzi wa kichini chini na adharani! Ni swali la kila mmoja katika siku ya leo ya kimataifa ya kuupiga vita ubaguzi.  Ni kujaribu kutazama kwa pamoja namna ya kuhamasisha maelewano, usawa kidugu, hasa kwa kizazi kipya. Siku hii inakumbusha juu ya haja ya kutekelezwa mpango wa hatua za pamoja za kimataifa kama ilivyopendekezwa katika kongamano nyigi za kimataifa. Shuhuda mbalimbali tukiwa ndani ya mabasi, treni au kutembea barabarani inatishia kusikia maneno mabaya yanayotolewa na watu wazima, hadi kuona vijana wengine wanakaripia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO): Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linasema kwamba “wanadamu wote ni jamii moja na wametokana na familia moja kwa mjibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Jamii na Ubaguzi wa Kijamii, mwaka 1978. Hata hivyo katika maeneo mengi ya dunia, vitendo vya ubaguzi bado vimeenea, ikiwemo ubaguzi wa rangi, makabila, dini, utaifa na uchochezi wa chuki. Ni  mamia ya mamilioni ya watu wanaendelea kuumia kutokana na ubaguzi wa rangi, upendeleo, chuki dhidi ya wageni, na kutengwa na jamii.  Hata hivyo kwa mujibu wa wa ripoti ya UNESCO dhidi ya Ubaguzi, inasema huenda elimu ikawa njia muhimu ya kupambana na aina mpya za ubaguzi wa rangi, upendeleo, na kuwatenga watu wa jamii nyingine. Kadhalika shirika hili linathibitisha kuwa licha ya kuongezeka kwa ushirikiano kati ya mataifa, inaonekana ubaguzi wa rangi na wa kijamii “unazidi katika sehemu nyingi ulimwenguni.

Katika suala hili la ubaguzi, inasahulika kanuni ya dhahabu isemayo kila binadamu anayo haki ya kupata haki za binadamu bila ya ubaguzi. Haki za usawa na kutobaguliwa ni suala muhimu katika sheria za haki za binadamu.  Kuwabagua watu kwa misingi ya rangi na makabila kunaelezwa kama utegemezi wa utekelezaji wa sheria, ulinzi na udhibiti wa mtu katika mipaka kwa kuzingatia rangi, ukabila, asili ya taifa au ukabila kama misingi ya  kuwaingiza watu na utafutaji wa kina, utambulisho na uchunguzi, au kwa ajili ya kuamua iwapo mtu fulani anashiriki  katika shughuli za uhalifu.

Wakimbizi pamoja na wahamiaji ndio haswa walengwa katika ubaguzi wa rangi na uchochezi wa chuki: Katika azimio la wakimbizi na wahamiaji la jijini New York lililopitishwa mwezi Septe mba 2016 wanachama wa Umoja wa Mataifa walikemea vikali vitendo na dalili za ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na vitendo vingine vinavyohusiana na hayo kwa wakimbizi na wahamiaji na kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na mitazamo na tabia kama hizo hasa kuhusu uhalifu wa chuki, kauli za kichochezi na vurugu za kibaguzi. Mkutano wa kilele wa wakimbizi na wahamiaji wa mwezi Septemba 2016, pia ulikuja na kampeni ya “pamoja”, ikiwa ni hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha heshima, usalama na utu kwa wakimbizi na wahamiaji.  Kampeni hiyo ya kidunia ilikuwa inalenga kubadili fikra hasi na mitazamo hasi dhidi ya kundi hilo, kwa kushirikiana na nchi wanachama, asasi za kiraia na sekta binafsi. Kila mara Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiwataka watu duniani kusimama na kutetea haki za watu hii leo.  Je ni kwa jinsi gani ya kuweza kweli kuhamasisha na kuunga mkono matendo ya kila siku katika maisha ya mwanadamu ya kutetea haki za binadamu kwa ajili ya wengine? Popote tulipo,tunaweza kuleta mabadiliko kwa sababu inaanza na sisi sote. Je ni kwa namna gani wewe unatetea haki za binadamu?

Kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa katika siku ya kupinga ubaguzi: Tarehe 21 Machi kwa hakika  Umoja wa Mataifa unawaalika  mataifa kutafakari juu ya dharura hii na kuandaa mipango ya kuelimisha. Kwenye jamvi hili kuna ukuaji wa harakati za sera za kisiasa na za kitaifa ambazo, kama maelezo ya Umoja wa Mataifa, zinaeneza ulimwenguni kote, huchochezi  wa ubaguzi wa rangi, kutovumilia na mara nyingi huelekezwa dhidi ya wahamiaji na wakimbizi  hasa kwa watu  asili ya Afrika! Kwa sababu hii, azimio la tarehe 15 Januari 2019 ambalo lina lengo la kuondoa kabisa ubaguzi wa rangi, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliona haja ya kuthibitisha kwamba wanadamu wote wanazaliwa huru na sawa katika heshima na haki na kwamba wana uwezo sawa  wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo na ustawi wa jamii. Azimio hilo linasisitiza kwamba mafundisho yoyote yanayounga mkono ubora wa rangi ni ya uongo,inapaswa kushutumiwa na siyo ya kijamii, siyo ya haki ni  hatari.

Hata hivyo Tendayi Achiume, mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu mitindo ya sasa ya ubaguzi wa rangi, katika ripoti yake ya hivi karibuni ambayo ilikuwa inabainisha  juu ya tishio linaliwakimba watu wa mataifa, linawakilisha kweli kanuni za usawa na zisizo za ubaguzi. Kupungua  kwa maadili ya wanadamu na mikakati ya kitaifa, anasema, inawakilisha tishio kubwa kwa ajili ya  usawa na kuhamasisha ubaguzi, kutoelewana na kuundwa kwa taasisi na miundo inayohamasisha kutengwa kwa jamii. Kwa hiyo ripoti hiyo inakataa hali hiyo makundi hayo ya kitaifa na hambayo yanapendelea sera zisizozingatia au za kupingwa  makundi ya watu  ambao wanafuata misingi yao na ukabila wao wa kitaifa au wa kidini. Ripoti  pia inatazama juu ya matumizi ya itikadi za kidigitali zenye lengo ka kueneza ubaguzi. Vile vile  maandamamo ya hivi karibuni yanayo tukuza ubaguzi, ripoti inasema  yanachangia kukukuza aina ya kisasa ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa unyanyasaji na kutovumilia.

21 March 2019, 15:47