Siku ya kutokomeza ubaguzi ilianzishwa kunako mwaka 2014 na mpango wa Umoja wa Mataifa unao husika na harakati dhidi ya Ukimwi,UNAIDS Siku ya kutokomeza ubaguzi ilianzishwa kunako mwaka 2014 na mpango wa Umoja wa Mataifa unao husika na harakati dhidi ya Ukimwi,UNAIDS 

Siku kutokomeza ubaguzi duniani:Nchi zote zichunguze sheria na siyo kuumiza!

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na harakati dhidi ya Ukimwi,UNAIDS limetaka nchi zote duniani zichunguze sheria na sera baguzi zinazozuia baadhi ya makundi kupata huduma hizo.Imeeleza hayo tarehe 1 Machi 2019 wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi unaokwamisha mtu kupata huduma za afya na nyinginezo

Na Sr.Angela Rwezaula -Vatican

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS limetaka nchi zote duniani zichunguze sheria na sera baguzi zinazozuia baadhi ya makundi kupata  huduma hizo. Imeeleza hayo tarehe 1 Machi 2019 wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi unaokwamisha mtu kupata  huduma za afya na nyinginezo. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS  Bwana Michel Sidibé amesema ukiukwaji wa haki unafanyika kote duniani kwa sababu ya uwepo wa sheria na matendo baguzi na kwamba sheria zinapaswa kulinda na si kuumiza.

Mataifa 20 yameweka aina fulani ya vikwazo vya usafiri kwa watu wenye virus

Katika kusisitizia hilo ametolea mfano kuwa, mataifa 20 yameweka aina fulani ya vikwazo vya usafiri dhidi ya watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi, (VVU), mataifa mengine 29 yameripotiwa kuwa, mwanamke anahitaji ridhaa ya mumewe au mpendwa wake ili aweze kupata huduma za afya ya uzazi. Halikadhalika mataifa 59 yanalazimu makundi fulani ya watu kuchunguza hali yao ya virusi vya ukimwi (VVU) kabla ya ndoa, kuajiriwa au vibali vya kuishi na kama hiyo haitoshi kwenye mataifa yapatao 67, ndoa za jinsia moja zimeharamishwa. Ni kwa kuzingatia sheria na kanuni hizo kandamizi zilizopitishwa mwaka 2018 ambapo Bwana Sidibe anasema kuwa nchi zote lazima zitathmini kwa kina sheria na será zao kuhakikisha usawa na ulinzi kwa watu wote bila ubaguzi wowote. Katika siku ya kutokomeza aina zote za ubaguzi na kila siku amesisitiza kuwa, “hebu na tuchukue hatua pamoja kubadili sheria baguzi.”

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Unaids amepongeza mataifa ambayo mwaka jana yalichukua hatua kubadili sheria baguzi akitolea mfano wa nchi ya India ambayo Mahakama Kuu ilifuta kifungu namba 377 cha Kanuni za makosa ya jinai ambacho kilikuwa kinaharahalisha mahusiano ya jinsia moja. Na nchi ya Ufilippini imeshusha umri wa ridhaa ya mtu kuchunguza virusi vya ukimwi (VVU) bila kuomba ridhaa ya mzazi au mlezi ambapo sasa ni umri wa miaka 15 na wakati huohuo nchini Malawi wameondoa kifungu cha sheria ambacho kingeweza kamtia mtu hatiani iwapo hasingeweza kutangaza bayana kuwa na virusi vya ukimwi.

Siku ya kutokomeza ubaguzi ilianzishwa 2014

Siku ya kutokomeza ubaguzi ilianzishwa kunako mwaka 2014 na mpango wa Umoja wa Mataifa unao husika na harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS ambapo walisisitiza zaidi kwamba tukio hili linapaswa liwaunganisha serikali zote  na raia wote kwa lengo la kutazama kwa upya nia za baguzi, ambazo zinatokana na sababu nyingi, kati ya hizo ni uzee, jinsia, kabila na afya na nyingine nyingi. Wakati wa kutoa tamko la kunza sikhi hiyo  mwaka 2014 Mkurugenzi mkuu wa Mapango wa Umoja wa mataifa katika harakati dhidi ya ukimwi, Bwana Michel Sidibè alitaka serikali na jamii zote duniani kushirikiana  kwa pamoja ili kupinga  kila aina ya mtindo wa kibaguzi.

Maadhimisho ya mwaka jana yalitazama saabu za ujinga wa kibaguzi

Wito wa mwaka jana 2018 ulikuwa unaizingatia kukabiliana na ujinga ambao unasabisha na kutofahamu, kwa maana hiyo UNAIDS iliandika wito wake kuwa   hakuna hata mmoja anapaswa ahisi kubaguliwa kwa sababu ya umri, jinsia, utambulisho wa aina yoyote, uemavu, kabila, rangi, lugha, uhamiaji na kila aina ya sababu. Haki hizi ambazo katika nchi nyingi duniani utafikiri zimehakikishwa, lakini kiukiukweli bado ni sababukubwa ya kukosa ulinzi wake na haki yake. Watu wengi kila siku wanaathirika sana na  matendo ya kibaguzi kuanzia utambulisho wao hadi kufikia matendo yao. Kutokana na hiyo, kuna haja ya kupinga , kunahaja ya kupambana dhidi ya ujinga , imani potofu, ukosefu wa elimu na hofu ambazo zinazidi kuongezeka kati ya watu.

04 March 2019, 15:40