Utapiamlo wa kukithiri nchini Yemen Utapiamlo wa kukithiri nchini Yemen 

Papa:Baba utupe mkate kwa ajili ya watoto wa Yemen,Siria na Sudan Kusini!

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko,Jumatano 27 Machi 2019 wazo lake limewaendea watoto wengi wenye njaa,mahali ambapo wanakosa mkate. Amewaomba waamini wote kuungana katika sala wakisema Baba utupatie mkate wa kila siku!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko,Jumatano 27 Machi 2019 wazo lake limewaendea watoto wengi wenye njaa mahali ambapo wanakosa mkate. Amewaomba waamini wote kuungana kwa sala wakisema Baba utupatie mkate wa kila siku. Baba Mtakatifu anasema mkate ambao mkristo anaomba katika sala siyo mkate wangu, hivyo lazima kuwa na umakini huo, Baba Mtakatifu ametoa angalisho. Kwa sababu, ni mkate wetu na ndiyo Yesu anapenda hivyo. Yeye anatufundisha kuomba, si kwa ajili yetu binafsi, bali kwa ajili ya ndugu wote duniani. Iwapo hatusali kwa namna hiyo, yaani  Baba Yetu, hakuna sala ya mkristo anathibitisha Baba Mtakatifu. Akendelea na tafakari anasema: Iwapo Mungu ni  Baba Yetu, tunawezaje kujiwakilisha kwake bila kushikana mkono sisi sote? Je  iwapo mkate ambao yeye anatujalia tunauiba kati yetu, tunawezaje kusema sisi ni watoto wake?

Kifikiria watoto hawa na kusali kwa sauti ya juu “utupe leo mkate wetu wa kila siku

Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anafafanua kwamba, sala hii ina ina tabia ya mtazamo wa huruma, na tabia ya mshikamano! Ni  kihisi njaa yangu kama njaa ya wengine, basi nitasali kwa Mungu ili hata maombi yao yaweze kusikilizwa. Na ndiyo jinsi ambavyo Yesu anaelimisha jumuiya yake, Kanisa lake ili kupeleka kwa Mungu mahitaji ya wote kuwa: “ sisi ni wana wako, au Baba utuhurumie”. Kwa maana hiyo anathibitisha kuwa, itakuwa vema kusimama na kufikiria watoto wenye njaa. Kufikiria watoto ambao wanaishi katika nchi zenye migogoro ya kivita; watoto wenye njaa nchini Yemen, watoto wenye njaa Siria na watoto wenye njaa katika nchi ambazo hakuna mkate kama vile Sudan ya Kusini.

Kwa kufikiria watoto hao, Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa pamoja ni kusali sala kwa sauti ya kuu; "Baba utupe leo mkate wa kila siku"…. Wote wamerudia sala hiyo ….. Mkate  tunaoomba kwa Bwana katika sala ndiyo mkate huo ambao kila siku unatuhukumu. Na Bwana  anatukaripia kutokana na ukawaida wa kukosa kuumega mkate kwa yule aliye karibu na ukawaida wa kukosa kushirikishana. Ni mkate ulitolewa bure kwa binadamu, na badala yake umeliwa na mmoja tu. Upendo hauwezi kuvumilia hili.

Mzozo wa Yemen unaingia mwaka wa tano

Wakati mzozo wa Yemen ukiingia mwaka wa tano, maeneo ambako kuna mahitaji zaidi hayafikiki kwa ajili ya kuwasilisha msaada limesema Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi msemaji wa WFP Herve Verhoosel amesema WFP inahitaji kufikia watu walioko hatarini kwa uhuru bila vizuizi vyovyote ili kuhakikisha hali ya njaa haiwi mbaya zaidi.

Hata hivyo katika kipeo hiki cha Yemen tarehe 25 Machi WFP imeelezea wasiwasi wake kufuatia ripoti za kuongezeka kwa uhasama katika maeneo kadhaa ya mji wa Hodeidah ikiwemo katika mtaa wa Sana’a uwanja wa ndege wa Hodeidah, chuo na Kilo na maeneo mengine. WFP imeongeza kuwa usalama ni lazima ili kuhakikisha uwasilishaji wa misaada inayotolewa na WFP na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa. Bwana Verhoosel ametolea mfano jimbo la Hajjah moja ya maeneo kunakoshuhudiwa uhaba wa chakula, ongezeko la ukatili unahatarisha maelfu ya watu kukabiliwa na njaa kubwa ambapo katika kipindi cha miezi sita, idadi ya watu walioondoka  kutokana na ongezeko la ukatili imeongezeka sana kutoka 203,000 hadi watu takriban 420,000.

Kwa mujibu wa shirika hilo kaya 11,000 wametoka katika jimbo la Hajjah tangu kuzuka kwa mapigano mapema mwezi machi 2019 na shirika hilo limetoa mgao wa chakula kwa familia 5,000 na bado mgao wa chakula unaendelea. WFP na wadau wake hawajaweza kufikia wilaya nne karibu na mpaka wa Saudia kwa sababu ya ongezeko la machafuko hususan wilaya ya Harad, Mustaba, Midi na Hayran ambako kuna takriban watu 50,000 walio katika hatari ya kufariki kutokana na njaa.

Kipeo cha watoto Yemen

Hali  ya watoto nchini Yemen kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema tangu 2015 watoto karibia milioni 85 wamekua kwa sababu ya utapiamlo na magonjwa. Kwa mujibu wa shirika la Save the Children , zaidi ya watoto milioni 10 hawawezi kufikia matibabu ya kutosha.Mwaka huu kwa mujibu wa Takwimu ya Umoja wa Mataifa karibia milioni 2 za watoto watahitahi matibabu dhidi ya utapiamlo wa kukithiri. Maisha ya watoto wadogo milioni 11,3 kwa mujibu wa Unicef yanategemea na nguvu za msaada wa kibinadamu. Bila kuwa na oparesheni za haraka maisha ya watoto hao yako hatarini.

 

27 March 2019, 13:25