Tafuta

Mtazamo kwa ujumla wa kuonesha uharibifu baada ya Kimbunga Idai huko Beira,Msumbiji Mtazamo kwa ujumla wa kuonesha uharibifu baada ya Kimbunga Idai huko Beira,Msumbiji  

Msumbiji-Kimbunga cha Idai:ni maafa makubwa kwa jengo la Afya huko Beira

Kimbunga kiitwacho Idai kilichoikumba nchi ya Msumbiji,Zimbabwe na Malawi, inasemekana kimeacha madhara makubwa sana,yakiwemo vituo vya afya,shule na makazi ya watu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kati ya watu waliopoteza maisha  mashariki mwa nchi ya Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga kiitwacho Idai  ni katika shule mbili ambapo tufani hiyo iliwakumba usiku wa manane wakiwa wamelala. Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu wa miundo mbinu katika jimbo la Manicaland karibu na mpaka wa Zimbabwe na Msumbiji. Jitihada za uokoaji zinaendelea hadi sasa huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani waliko, hali inayohofiwa kwamba huenda inaweza ongeza idadi ya waliopoteza maisha.

Rais Emmerson Mnangagwa alialazimika kusitisha ziara yake huko Mashariki ya Kati na kurejea nchini mwake kutokana na janga hili. Hata hivyo, kimbunga hicho kimesababisha madhara makubwa huku takribani watu 200 wakiwa hawajulikani walipo. Bado familia nyingi zinasubiri kupatiwa msaada baada ya nyumba zao kubomolewa na maji japokuwa uharibifu wa miundo mbinu zikiwemo barabara, unaongeza ugumu wa kuwafikia watu hao na kuwasaidia.

Raia wa Zimbabwe wameungana pamoja na kuendelea kuchanga fedha, mablanketi na chakula kwa ajili ya wahanga wa janga hilo. Nchini Msumbiji na Malawi kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 120. Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga hicho kilicho yakumba maeneo hayo kikiwa na mwendo wa kasi, kilomita 177 kwa saa. Sehemu kubwa ya maeneo yaliyokumbwa ni masikini, miji mingi iko hatari ya mlipuko wa kipindupindu. Ni lazima kuhakikisha inapatikana huduma ya afya licha ya janga hili kubwa.

Ni zaidi ya milioni moja na nusu ya watu waliokumbwa na karibia waathirika 150 wa kimbunga cha Idai ambacho kimeikumba kwa siku hizi chi za Musumbiji, Malawi na Zimbabwe kwa mujibu wa data za Umoja wa Mataifa na vyanzo habari rasmi za serikali. Mji uliopatwa hasara zaidi nchini Msumbiji ni Beira. Kwa dhati ni janga kubwa kusikiliza hata simulizi za watu wa kujitolea  wakisimumulia nchini Musumbiji.

Hapakuwapo hata mawasiliano siku ya Ijumaa na Jumamosi ambapo ilikuwa hata vigumu kuwasiliana na madakari wa Beira, anasimulia Giovanna De Meneghi, mkurugenzi wa mipango ya huduma ya Madaktari na Aafrika Cuamm katika nchi hiyo. Mji umeharibika kabisa, na nyumba zote za mabati kusambaratika kila sehemu kufuatia na upepo mkali sana ambao ulikuwa kasi kubwa kuwahi kutokea katika nchi hzi. Hospitali ya kati mjini Beira, iko katika hali ngumu sana ikiwa hata kituo cha wazazi huko (Berçario). Jengo la dharura limeondolewa paa lake na hakuna maji wala umeme, sakafu imejaa matope tu na maji.

Na wakati huo huo wanazidi kumiminika watu walio jeruhiwa, japokuwa  hospitali inatoa msaada kwa kadiri inavyoweza, hadi masaa 24 kwa 24. Taarifa pia inasema, hata paa la jengo la  Chuo Kikuu Katoliki Msumbiji, limepeperushwa na kimbunga hicho. Mawasiliano na mji Mkuu Maputo ni shida, mahalia ambapo ndipo kuna kituo cha Mipango cha CUAMM na Beira mahali ambapo kwa miaka mingi wametumia kuandalia mipango yao mingi  kwa ajili ya afya ya mama na mtoto na mapambao na UKIMWI.

19 March 2019, 14:38