Tafuta

Vatican News
Rais Sergio Mattarella kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Italia anampongeza Papa Francisko kwa kuadhimisha kumbu kumbu ya miaka sita ya utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Rais Sergio Mattarella kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Italia anampongeza Papa Francisko kwa kuadhimisha kumbu kumbu ya miaka sita ya utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.  (ANSA)

Rais Mattarella ampongeza Papa Francisko kwa utume!

Familia ya Mungu nchini Italia, inapenda kumtakia heri na baraka Baba Mtakatifu Francisko anapoadhimisha tarehe 19 Machi 2019, Miaka 6 tangu alipoanza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anamshukuru na kumpongeza kwa kazi kubwa anayoendelea kuitekeleza kwa kujisadaka bila ya kujibakiza, kiasi cha kuwashangaza watu wengi na kuvutwa na mwelekeo huo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Sergio Mattarella kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Italia, anapenda kumtakia heri na baraka Baba Mtakatifu Francisko anapoadhimisha tarehe 19 Machi 2019, Miaka 6 tangu alipoanza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Anamshukuru na kumpongeza kwa kazi kubwa anayoendelea kuitekeleza kwa kujisadaka bila ya kujibakiza, kiasi cha kuwashangaza watu wengi na kuvutwa na mwelekeo huo!

Rais Mattarella anampongeza Baba Mtakatifu kwa hija mbali mbali za kitume ambazo amezifanya katika kipindi cha Mwaka huu na hatimaye kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani huko Panama. Anasema, Baba Mtakatifu Francisko, amekuwa ni Khalifa wa kwanza wa Mtakatifu Petro kutembelea katika Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, ili kukoleza mchakato wa majadiliano ya kidini, ili kujenga udugu wa binadamu! Kila hija iliyofanywa na Baba Mtakatifu, imekuwa ni fursa ya kutoa ujumbe wa matumaini, amani na udugu kwa watu wote bila kujali dini, kabila au tamaduni za watu, kiasi hata cha kuchangamotisha dhamiri za watu kujikita katika mchakato wa majadiliano na maridhiano!

Rais Mattarella anampongeza Baba Mtakatifu kwa huduma anayoitoa kwa familia ya Mungu nchini Italia. Ushuhuda wake unajionesha kwa kufanya hija za kichungaji huko Puglia, Toscana na Sicilia pamoja na kuendelea kuimarisha mshikamano wa Kanisa na maskini pamoja na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Rais Mattarella anakumbuka kwa shukrani kubwa, mara ya mwisho walipokutana ana kwa ana ni wakati alipokuwa anamtangaza Papa Paulo VI kuwa Mtakatifu. Mwishoni, anamtakia kila la heri na baraka katika maisha na utume wake, ili aendelee kuliongoza Kanisa kwa mafundisho yake makini!

Rais Mattarella: Papa
19 March 2019, 16:34