Vatican News
Viongozi mbali mbali wanalaani tendo la kuchomwa moto kituo cha kutibu Ebola kinachoendeshwa na Madaktari wasio kuwa na mipaka huko Katwa nchini DRC Viongozi mbali mbali wanalaani tendo la kuchomwa moto kituo cha kutibu Ebola kinachoendeshwa na Madaktari wasio kuwa na mipaka huko Katwa nchini DRC 

DRC:Zaidi ya watu 800 wameshambuliwa na mlipuko wa ebola na 500 wamekufa

Mkurugenzi mkuu wa Unicefu, Bi H.Fore anathibitisha katika taarifa yake kuwa watu 800 wameshambuliwa na Ebola wakati wa mlipuko wa mwisho,wakati watu 500 wamekufa na robo tatu ya kesi hiyo ni watoto

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Zaidi ya watu 800 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wamekwisha ambukizwa na Ebola wakati wa mlipuko wa mwisho; zaidi ya watu 500 wakufa. Watoto wanawakilisha robo tatu ya kesi ya Ebola zilizo thibitiwa na zaidi ya mlipuko wa nyakati zilizopita. Hayo yamethibitishwa na Bi Henrietta Fore, Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF katika taarifa  ambayo anasema inasitikitisha hata kwa mashambuliza ya mwisho na ya nguvu dhidi ya kituo cha tiba ya ebola kilichokuwa kinaendele kuwatibu watoto na watu wa familia nyingi Mashari ya nchi ya DRC.

Katika mchakato wa mashambulizi ya hivi karibuni wanasema polisi ameuwawa na jengo la Kwatwa kuchomwa moto , kwa maana hiyo  Bi Fore anatoa salam za rambi rambi kwa wanafamilia wote kutokakana na kupteza maisha katika mashambulizi hayo, ikiwa pia ni salam kwa kikundi cha madaktari wasio kuwa na mipaka ambao wanaendelea kutoa huduma yao katika mazingira magumu sana  anasema  Bi Fore. Kila siku, kikundi cha UNICEF na wadau wengine, kati yao wahudumu wa afya katika vituo vya kutibu ebola wanaendelea na jitihada zao  za kijasiri kwa  ajili ya kuokoa  maisha ya watoto na watu wazima ambao wamepata virus vya Ebola. Haiwezekani kueleweka kwa yule anayetaka kuzuia watoto na familia wasipate huduma ambayo inawakilisha kuishi kwao anaonya Bi Fore.

Hata hivyo  kufuatia matukio ya kutiwa moto kwa kituo cha kutibu Ebola cha Katwa na kile cha Butembo kwa kushambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana, vyote jimboni Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeripotiwa kuwa vituo hivyo viwili sasa havifanyi kazi kabisa. Shirika la afya ulimwenguni WHO ambalo limelaani kitendo hicho, sasa linahofu kuwa ugonjwa huo unaweza kusambaa zaidi kutokana na hatua ya baadhi ya mashirika ya kiraia kuondoa wafanyakazi wake kutoka eneo hilo. Martial Papy Mukeba wa Radio Okapi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO anaripoti zaidi. Kituo cha kutibu Ebola cha Katwa kilichomwa moto siku chache zilizopia  na wakati huo  kile cha Butembo kilishambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana siku mbili zilizopita na kabla ya kufungwa zilizikuwa zinasimamiwa na madaktari wasio na mpaka, (MSF) na Wizara ya Afya ya DRC. Kituo pekee cha muda cha kutibu Ebola ambacho kinafanya kazi sasa ni kile kilichopo kwenye hospitali ya Katwa kikiongozwa na ALIMA.

Mashambulizi haya mawili yamechochea Madkatari wasio na Mpaka (MSF) na ALIMA kuondoa wafanyakazi wao wa matibabu kutoka Butembo na Katwa. Daktari Michel Yao, kiongozi wa operesheni za dharura katika WHO barani Afrika anatoa tahadhari juu ya hatari ya kusambazwa kwa ugonjwa wa Ebola kama hakuna kinachofanyika. Anasema kuwa “kuna shirika la madaktari wasio na mipaka ambalo limehamisha wafanyakazi wake, na pia shirika la ALIMA pia limehamisha wafanyakazi wake. Ni kusema vituo vya matibabu vya Ebola vya Katwa na Butembo havifanyi kazi tena. Ni jambo ambalo linakwamisha kazi za kuzuia Ebola.Ikiwa  hakuna kinachofanyika, Ebola itasambaa miongoni mwa wakazi”. Na ifahamike kwamba Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 6 vya Ebola mjini Katwa.

04 March 2019, 15:58