Tafuta

Vatican News
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Michelle Bachelet akiwakilisha Ripoti katika Kikao cha 40 cha Baraza la  haki za binadamu mjini Geneva Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Michelle Bachelet akiwakilisha Ripoti katika Kikao cha 40 cha Baraza la haki za binadamu mjini Geneva   (ANSA)

Bachelet:Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu

Ripoti ya kila mwaka ya hali ya Haki za Binadamu Duniani iliyowasilishwa tarehe 6 Machi 2019 mjini Geneva Uswisi na Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Michelle Bachelet katika Kikao cha 40 cha Baraza la haki za binadamu kuhusu kazi uliyofanyika kwa mwaka 2018 inathibitisha kuwa bado ukiukwaji mkubwa wa haki msingi!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea kutamalaki katika sehemu mbalimbali duniani ukichochewa zaidi na changamoto zilizopo hivi sasa ikiwemo tishio la mabadiliko ya tabianchi, maendeleo ya teknolojia, vita vinavyozua wasiwasi kubwa kwa raia, ukosefu wa ajira kwa vijana, mabadiliko ya mifumo, chuki dhidi ya wageni na ongezeko la pengo la usawa. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya hali ya haki za binadamu duniani iliyowasilishwa tarehe 6 Machi  2019 mjini Geneva Uswisi na Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Michelle Bachelet katika Kikao cha 40 cha Baraza la  haki za binadamu kuhusu kazi uliyofanyika kwa mwaka 2018.

Mbele ya wajumbe wa nchi wanachama kwenye Baraza la Haki za binadamu Bi. Bachelet amesema changamoto kubwa zaidi hii leo ni ongezeko la pengo la usawa kwani pengo la usawa katika kipato, mali, rasilimali, fursa ya haki ya kisheria vinaleta changamoto kubwa katika misingi ya usawa, utu na haki za binadamu kwa kila mtu, na vinatokana na uongozi mbovu, ufisadi, kutokuwepo utawala wa sheria, ubaguzi, na taasisi dhoofu au zenye upendeleo. Bi. Bechellet akiendelea kuelezea amefafanua juu ya athari za pengo la usawa katika jamii ambapo anasema pengo hilo katika masuala ya haki za kisiasa, kijamii na kiuchumi ni chachu na linaweza kusambaratisha mihimili ya Umoja wa Mataifa. Na ili kuhakikisha hili halitokei Bi. Bachelet amesema ni muhimu sana kufanyakazi kwa karibu na nchi wanachama na kuzisaidia kuweka mifumo ya usawa na kuhakikisha haki za binadamu zinadumishwa na kusisitiza kwamba, pengo la usawa linaathiri nchi zote hata katika nchi tajiri watu bado wanahisi wanatengwa katika faida za maendeleo na kunyimwa haki za kiuchumi na kijamii na kusababisha hali ya kutengwa, na wakati mwingine machafuko. Pia ameongeza kuwa pengo hilo la usawa ni tishio kubwa la amani na usalama na limewalazimisha mamilioni ya watu kufungasha virago kuzihama nyumba zao na hata nchi zao. Amesisitiza kuwa pengo hilo la usawa limedumaza maendeleo ya kijamii, utulivu wa kiasiasa na kiuchumi.

Kwa upande mwingine amesema kudumisha amani kunajenga matumaini, kunawaleta watu pamoja katika misingi ya kuwa na mustakabali bora tofauti kabisa na ukandamizaji, ubaguzi, uonevu na kutokuwepo kwa usawa. Aidha katika ripoti yake Kamishina Mkuu wa haki za binadamu amezigeukia nchi nchi ambazo zimekuwa na changamoto kubwa ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo suala la usawa kwa kutoa  mfano,wa chini Sudan katika miezi kadhaa iliyopita watu ambao wamekuwa wakiandamana kupinga hali mbaya ya uchumi na utawala mbovu, wametawanywa kwa nguvu na vikosi vya usalama, wakati mwingine kwa kutumia risasi za moto. Matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati mwingine ndani ya hospitali, misikitini  na kwenye vyuo vikuu, watu kuingozwa kwa nguvu rumande kiholela, utesaji na kutangazwa kwa hali ya dharura, hakutasaidia kumaliza dukuduku nyingi na  halisi ambayo waandamanaji wanataka kuyaeleza amethibitisha.

Kwa mantiki hiyo Umoja wa Mataifa umeichagiza Sudan kufanya mabadiliko yenye manufaa ili  kukabiliana na ufisadi uliotawala nchini humo, kufungua fursa za kiraia, kuwezesha majadiliano jumuishi na ushiriki mkubwa wa watu katika ngazi ya maamuzi. Kadhalika  mfano mwingine ni  nchini Zimbabwe ambako changamoto za haki za binadamu zimekuwa kwa miaka nenda rudi  na hivyo ameweka bayana kwamba: maandamano ya kupinga hatua za kukabiliana na kudorora kwa uchumi yalikabiliwa na ghasia zisizokubalika kutoka kwa vikosi vya usalama lakini hatua za serikali za kuzindua mchakato wa majadiliano  katika siku za hivi karibuni zinatia moyo japokukuwa  anahofia ripoti za msako wa nyumba kwa nyumba pamoja na vitisho dhidi ya wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu na wanaowawakilisha watu waliokamatwa!

Ripoti hiyo ya kina, mbali ya kujikita na pengo la usawa imeangazia mada zingine ikiwemo hali mbaya ya kiuchumi, na haki za kisiasa na kiraia kama vile nchini Venezuela, Nicaragua, huku ikisikitishwa na wanayotendewa watetezi wa haki za binadamu kote duniani hususan Saudi Arabia na Uturuki, Haiti, nchini Ufaransa, Nicaragua katika nchi ya Palestina na Yordania, kuanzia China hadi India, kutoka El Salvador hadi Guatemala, Honduras, kutoka Yemen hadi Ethiopia, kutoka Sahel hadi Myanmar, kutoka Uffilippini hadi Libia  kutoka Kashmir hadi Pakistan.Bi Bachelet anatoa wito wa kuwa na mazungumzo ya kujenga, kuheshimu uhuru wa kujieleza na kuzuia ukiukwaji wa kila hadi ya binadamu na  kuwa na usalama wa kulinda watu na  kusaidia binadamu! Haki ya maendeleo na ajenda ya 2030 ya kutomwacha yeyote nyuma pia imegusiwa  kwa maana anasema:ili kufikia malengo ya Agenda 2030, nchi za dunia zinapaswa kuendeleza kushughulikia usawa; usawa wa rasilimali, mapato, nguvu, upatikanaji wa haki na kuheshimu hali msingi ya hadhi ya kibinadamu, lakini ni  wasiwasi wake kuona idadi kubwa ya mauaji ya waathirika wa utetezi wa haki za binadamu duniani kote na mashirikia yasiyo ya kiserikali yanayoshirikiana nao. Pia jicho likielekezwa kwa nchi ya China ili kuhakikisha safari hiyo inamjumuisha kila mmoja na hata jamii za walio wachache mfano nchini India.

Nguvu thidi ya wanawake inaendelea kuendea kwa maana mwanamke mmoja kati ya 5 anakufa: Kuhusu suala la mauajia dhidi ya wanawake limekuwa kero katika sehemu nyingi duniani ambapo Bi Bachellet anasema katika sehemu nyingi za dunia, wanawake wanashambuliwa, hutumiwa, unyanyaswa na kunyamazishwa waibiwa hadhi yao na haki zao. Vurugu za kijinsia zinaendelea kuenea katika hali ya migogoro, na waathirika wengi walengwa kwa misingi ya kikabila, kidini, kisiasa au ukoo. Hata wanawake wahamiaji na wasichana wana hatari kubwa ya unyanyasaji wa kijinsia. Kati ya nchi 25 zilizo na viwango vya juu zaidi vya mauaji ya kike ulimwenguni, nchi 14 ni za Amerika ya Kusini na Caribbean, wakati mwanamke mmoja kati ya wanawake watano katika nchi za Umoja wa Ulaya amepata nguvu na unyanyasaji wa kimwili au kijinsia kutoka kutoka kwa mpenzi wake  wa sasa au wa zamani.  Lakini pia Bi Bacchelet pia ametoa habari njema zinazotia matumaiani hasa katika ukombozi wa mwanamke katika dunia kwamaba anaendelea kuwa na maendeleo kulingana na uongozi wa mwanamke na usawa wa wanawake.

Kwa kutoa mfano amesema mwakambe ameweza kuchaguliwa kuwa Rai wa nchi ya Ethiopia ambayo ni hatua kubwa na kama ilivyo mwaka jana nchini Tunisia alichaguliwa Meya mwanamke katika kanda ambayo wanawake wana ngazi ya chini sana katika uwakilishi wa sera za kisiasa duniani na pia ongezeko la kukumbuka kwa wanawake ni lile la kuchaguliwa hivi karibuni wabunge wanawake kwenye Bunge la Congress nchini Marekani. Hii imeonesha hatua muhimu ya kuwa na wanawake na maendeleo ya utofauti hasa  mwamake wa kwanza mwislam katika kongress ya Marekani na mzaliwa wa Marekani na kijana aliyewahi kuchaguliwa katika Congress nchini Marekani. Kwa maana hiyo Bi Bachellet amewasalimia wanawake wote walioko katika madaraka dunia kote na kwamba ni mfano ambao unawakilisha kizazi endelevu.

Mada za ugaidi, ukatili wa kingono kwenye migogoro na ongezeko la wimbi la wahamiaji hususan Amerika ya Kati, Marekani, Australia na Muungano wa Ulaya halikupewa kisogo:Suala la wahamiaji ni changamoto ambayo inaweza kukabiliwa kwa pamoja kwa njia ya vipimo vya kidunia vyenye kisimamia hali za binadamu ambazo zinakwenda pamoja na mkataba wa pamoja kuhusu uhamishaji uliotolewa mwezi Desemba  2018 mjini Marrakesh Morocco. Hata hivyo migogoro ya kislaha mara nyingi ndiyo sababu kubwa ya uhamiaji wa ihali. Lakini mara nyingine  kuhama kwa kulazimisha na migogoro ni mambo mawili ambayo yanaongozwa na ukosefu wa usawa ikiwa pia sababu nyingine kama vile  umasikini, ubaguzi, kunyanyaswa, nguvu, ukatili wa utawala, mabadiliko ya tabianchi, ukiukwaji wa kiraia, kisiasa , kiuchumi, kijamii na haki za utamaduni.Hali kadhalika   kwa mujibu wa ripoti suala la ugaidi bado ni mtihani mkubwa dunia nzima ikiwemo katika nchi za Kiarabu, sahel na pembe ya Afrika. Kwa kuzingatia mambo hayo watu na hasa vijana wanaweza kuhisi kuelemewa na kuibiwa haki zao na ndiyo sababu inayopelekea kuhama na mara nyingi kwa kutaka kutafuta maisha bora.

Kwa kutazama matukio hayo ya uhamiaji, Bi Bachelet ameweza kutazama kwa kina hali halisi ya Amerika ya kati na protokali mpya za ulinzi wa wahamiaji ambapo Marekani inatoa vizingiti vya kutoa ruhusa kwa waomba hifadhi na aina nyingine za ulinzi. Na kwa upande mwingine  pia ameweza kupongeza baadhi ya mipango na sheria ambazo nchi za Ulaya wameweza kujiwekea, japokuwa hakukosa kuonesha  wasiwasi mkubwa kwa mantiki nyingine sera za kisiasa kuhusu uhamiaji Ulaya kwa namna ya pekee kwa idadi kubwa ya wathirika katika Bahari ya Meditteranea , mahali ambapo watu 226 wamerekodiwa kufa katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka 2019. Ameomba Umoja wa nchi za Ulaya na nchi wanachama wake kutoa kipaumbele cha maisha na usalama wa wahamiaji ambao wanakatisha bahari ya Meditterranea, kuongeza jitihada za kutafuta na kulimbilia, kuruhusu vikosi vya ukoaji vya meli za mashirika yasiyo ya kiserikali na kupangilia mapokezo yao ya haraka katika forodha na usalama wa binadamu hawa na wakati huohuo wakikabiliana na mizizi ya sababu za uhamiaji huo.

07 March 2019, 15:19