Tafuta

Vatican News
Ni jukumu la watu wote kuchukua hatua ili kuzuia uonevu na ukatili mtandaoni wakati wa kuadhimisha Siku ya Usalama wa Mtandao wa Intaneti Ni jukumu la watu wote kuchukua hatua ili kuzuia uonevu na ukatili mtandaoni wakati wa kuadhimisha Siku ya Usalama wa Mtandao wa Intaneti  (AFP or licensors)

UNICEF:Hatua zichukuliwe dhidi ya uonevu wa watoto katika mtandao!

Katika kilele cha kuadhimisha Siku ya Usalama wa Mtandao wa Intaneti,tarehe 5 Januari,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa wito wa kuchukua hatua dhidi ya uonevu na ukatili mtandaoni ambao unawakumba zaidi ya asilimia 70 ya vijana duniani kote

Na Sr.Angela Rwezaula -Vatican

Katika kuadhimisha siku ya usalama wa mtandao wa intaneti tarehe 5 Januari 2019, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kuzuia uonevu na ukatili mtandaoni kwa zaidi ya asilimia 70 ya vijana duniani kote. Katika taarifa yake UNICEF imeonya kuhusu hatari zitokanazo na uonevu na ukatili huo kwa watoto wadogo na vijana ambaoi  asilimia 70.6 wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 duniani na kuongeza kusema kwamba ikiwa ni miaka 30 baada ya kupitishwa mkataba kuhusu haki za mtoto ni wakati sasa wa kuelekeza nguvu kwenye haki za kidijitali za watoto.

Vijana, wazazi na walimu kutunga sera za kuwalinda

Wito huo uliotolewa katika Siku ya usalama mtandaoni https://www.unicef.org/online-safety/?utm_campaign=safer-internet umekuja kufuatia na  utafiti uliofanywa na UNICEF kwa kuhusisha vijana na kupokea majibu zaidi ya milioni moja katika kipindi cha wiki tano kutoka nchi zaidi ya 160 na mapendekezo kutoka kwenye mfululizo wa majadiliano ya vijana yajulikanayo kama #ENDviolence yaliyofanyika dunia nzima. Katika utafiti huo vijana wametoa majibu ya kina kuhusu nini wao na wazazi wao, walimu na watunga sera wanaweza kufanya ili kuwalinda na suala la kutenda wema lilijitokeza kama moja ya hatua yenye nguvu na muhimu katika kuzuia uonevu na uonevu mtandaaoni. Akizungunmzia hilo mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Bi Henrietta Fore amesema kwamba wamesikia kutoka kwa watoto na vijana kote ulimwenguni na wanachokisema kiko bayana. Mtandao wa intaneti umekuwa jangwa jema na ndio sababu katika siku hii ya usalama wa mtandao wa intaneti, UNICEF inamkaribisha kila mmoja, vijana na wazee kuwa wema mtandaoni na kutoa wito wa hatua madhubuti wa kufanya mtandao wa intaneti uwe mahali pa salama kwa kila mtu.

Matumizi ya mtandao kwa watoto wadogo na zaidi wasichana

Bi Fore ameongeza akiendelea na ufafanuzi zaidi amesema kuwa mtandao wa intaneti umekuwa ni sehemu ya maisha ya vijana licha ya kiwango cha uchumi walichonacho. Kwa mujibu wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU, wakati asilimia 94 ya vijana wa umri wa kati ya miaka 15-24 katika nchi zilizoendelea wako mtandaoni, zaidi ya asilimia 65 ya vijana katika nchi zinazoendelea wako mtandaoni. Hii ni zaidi ya kasi ya matumizi ya mtandao wa intaneti kwa idadi nyingine ya watu. Na duniani kote, nusu ya watu wote bila kujali umri wako mtandaoni. Hata hivyo hatua hii ya UNICEF inasema inakuja na ongezeko la hatari, kwani kwa mujibu wa takwimu za shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, kiwango cha waathirika wa uonevu mtandaoni kwa watoto na vijana wadogo katika nchi za kipacho cha juu ni kati ya asilimia 5 hadi 21, huku wasichana wakionekana kuwa wahanga zaidi ya wavulana.

Athari za uonevu mtandaoni ni kubwa kwa watu wengi

Uonevu mtandaoni unaweza kusababisha athari kubwa kwani unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na unaweza kusalia mtandaoni milele na kuwa jinamizi kwa waathirika katika maisha yao yote. Uonevu na uonevu wa mtandao havitengamani na ni chachu ya tabia haribifu. Waathirika wa uonevu mtandaoni mara nyingi wanaweza kutumia pombe na mihadarati na kukwepa shule kuliko wanafunzi wengine. Na pia wanauwezekano mkubwa wa kupata alama za chini shuleni, kutojiamini na kupata matatizo ya kiafya. Na katika mazingira mengine ya hatari zaidi uonevu mtandaoni umesababisha watu kujiua hasa katika mataifa ya Ulaya na Amerika, matukio yamekwisha thibitishwa. Kutokana na mambo hayo katika kilele hiki UNICEF inamkumbusha kila mtu kwamba, wema  kwenye mtandao na nje ya mtandao ni wajibu ambao unaanza kwa kila mmoja wetu!

Je UNICEF inafanya nini katika kuenzi miaka 30 ya kupitishwa haki za mtoto?

Na katika kuenzi miaka 30 ya kupitishwa kwa mkataba kuhusu haki za mtoto UNICEF pia inatoa wito wa kufufua haraka ushirikiano wa kuziweka haki za mtoto katika msitari wa mbele kwenye juhudi za masuala ya kidijitali. Na kama sehemu ya hili, UNICEF inatejieleza katika mipango ya kutimiza ahadi ya kuunganisha watu na mtandao wa intaneti na elimu kwa niaba ya Watoto wa dunia hii, ikisisitiza kwamba:Ni wakati kwa serikali,familia,vyuo  na sekta binafsi kuwaweka watoto na vijana katika kitovu cha sera za masuala ya kidijitali, kuwalinda na madhala yatokanayo na mtandao wa intaneti na zaidi ili kupanua wigo wa fursa nzuri na kwa mambo mazuri.

05 February 2019, 15:34