Tafuta

Vatican News
Migogoro nchini Sudan Kusini inaendelea kutishia uzalishaji wa vyakula,kudhoofika hata wanyanya na vizingiti vya kuweza kufikia vyanzo vya vyakula mbadala Migogoro nchini Sudan Kusini inaendelea kutishia uzalishaji wa vyakula,kudhoofika hata wanyanya na vizingiti vya kuweza kufikia vyanzo vya vyakula mbadala   (Albert Gonzalez Farran / AFP)

Sudan Kusini:Milioni 7 ya watu wako hatari ya ukosefu wa chakula

Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yaani FAO,UNICEF na WFP wametangaza dharura la baa la njaa katika nchi ya Sudan kusini,ambapo ripoti inasema kuwa karibia watu milioni 7 wako hatari ya ukosefu wa vyakula na miongoni mwao watoto 860 wanakosa lishe bora

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

FAO; UNICEF na WFP, ambayo ni mashirika ya Umoja wa mataifa yametoa tangazo la dharura kuwa ni karibia watu milioni 7 nchini Sudan ya Kusini wataweza kukabiliana na ukosefu wa vyakula katika kipindi cha ukame ( kuanzia mwezi Mei na Julai) kwa maana hiyo wanaomba kuongezewa msaada ili kuweza kukidhi  msaada wa kibinadamu. Ripoti iliyotolewa tarehe 22 Februari 2019 mjini Juba na Serikali ya Sudan ya Kusini kwa ushirikiano wa Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa, idadi ya watu wenye wasiwasi kwa mtazamo wa vyakula tayari imeongezea kwa asilimia 13% tangu Januari mwaka 2018

Kati ya  watu 30,000 wanaishi tayari na uzoefu wa ukosefu wa uhakika wa kutisha wa vyakula. Migogoro inayoendelea kuitishia uzalishaji wa vyakula, kudhoofika hata wanyanya na vizingiti vya kuweza kufikia vyanzo vya vyakula mbadala ni sababu pia . Vipindi virefu vya ukame, mafuriko na magonjwa ya kilimo na upulizaji wa dawa za mimea umeleta madhara makubwa ya uzalishaji wa kilimo na mbao ndiyo  unategemewa kwa kiasi kikubwa. Kuna dharura ya mahitaji ya kifedha ili kuongeza msaada wa kibinadamu, hatimaye kuweza kuwasaidia maisha ya binadamu na kuwalinda kwa zana muhimu.

Pamoja na ripoti ya mashirika hayo kuhusu baa la njaa bado matatizo ni mengi nchini Sudani kwani,wakati maelfu ya watu kwa mara nyingine wakifukuzwa makwao kwa sababu ya machafuko nchini Sudan kusini , tume ya haki za binadamu kwa ajili ya Sudan Kusini imeitaka serikali ya nchi hiyo na pande zote katika mzozo kuheshimu mkataba wa usitishaji uhasama na kutekeleza mkataba huo mpaya wa amani uliotiwa saini miezi mitano iliyopita. Wito huo upo katika ripoti ya tatu ya tume hiyo iliyotolewa tarehe 20 Februari 2019 ambayo imebaini kwamba machafuko yanayoendelea na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo vitendo vya ubakaji na ukatili wa kingono vinaweza kuwa ni uhalifu wa kivita.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo ya haki za binadamu kwa ajili ya Sudan kusini, Bi Yasmina Sooka anasema kuwa,  tangu mwaka 2017 hadi sasa hali ya ukatili wa kingono imekubwa mbaya zaidi na kwamba kuna uthibitisho wa mwenendo wa jinsi gani wapiganaji wanavyoshambulia vijiji, kupora nyumba, kuwachukua wanawake kama watumwa wa ngono na kisha kuchoma nyumba na mara nyingi watu wakiwa  ndani yake. Aidha amsema kuwa ubakaji, na ubakaji wa magenge, utekeji na utumwa wa ngono pamoja na mauaji vimekuwa kama ada Sudan Kusini. Bi. Sooka amesema bila shaka uhalifu huu unaendelea kwa sababu ya ukwepaji sheria ambao unasababisha kila taratibu kuvunjwa.

Hata hivyo Ripoti pia imesisitiza kuwa  amani ya kudumu inahitaji uwajibikaji na haki ambayo inahitajika kwa maelfu ya watu wa Sudan Kusini . Kadhalika Ripoti inasisitiza kuwa tume inatiwa hofu kwa kuzorota kuanzishwa kwa mkakati wa haki na sheria hususani mahakama maalumu, tume ya ukweli na upatanishi na mamlaka ya ulipaji fidia. Na ripoti hiyo itawasilishwa kwenye Baraza la haki za binadamu mwezi Machi mwaka huu.

 

 

23 February 2019, 15:35