Tafuta

Vatican News
Licha ya mashambulio dhidi ya raia kupungua kwa kiasi kikubwa tangu kutiwa saini makubaliano ya amani lakini ukatili wa kingono unaendelea kutekelezwa Sudan Kusini Licha ya mashambulio dhidi ya raia kupungua kwa kiasi kikubwa tangu kutiwa saini makubaliano ya amani lakini ukatili wa kingono unaendelea kutekelezwa Sudan Kusini  (AFP or licensors)

Sudan Kusini:Wanawake na wasichana ni waathirika wa kingono

Kuna ongezeko la ukatili wa kingono katika jimbo la kaskazini mwa Sudan Kusini, ambapo wanawake 134 na wasichana wamebakwa na wengine 41 kukumbwa na aina nyingine za ukatili wa kingono kati ya mwezi Septemba na Desemba 2018

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 15 Februtari 2019 imetolewa Ripoti ya Umoja wa Mataifa huku ikonesha ongezeko la ukatili wa kingono katika jimbo la kaskazini mwa Sudan Kusini, kwa kutaja kuwa wanawake 134 na wasichana wamebakwa na wengine 41 wamekumbwa na aina nyingine za ukatili wa kingono kati ya Septemba na Disemba 2018.

Miongoni mwa waathirikia ni kuanzia umri wa miaka nane

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu,OHCHR,  Rupert Colville amesema, miongoni mwa manusura ni watoto wa umri wa miaka nane, huku idadi kamili ya visa hivyo ikitarajiwa kuwa juu zaidi ya visa vilivyoripotiwa. Ripoti hiyo iliyotolewa kwa pamoja na OHCHR na Ujumbe wa Umoja huo nchini Sudan Kusini, UNMISS inaonya kuwa licha ya mashambulio dhidi ya raia kupungua kwa kiasi kikubwa tangu kutiwa saini makubaliano ya amani lakini ukatili wa kingono unaendelea kutekelezwa katika jimbo la Kaskazini.

Bwana Rupert Collive anasema:“Asilimia 87 ya wanawake na wasichana walibakwa na zaidi ya mtu mmoja  kwa saa nyingi. Miongoni mwa watu waliobakwa, 50 walikuwa ni watoto huku mtoto mmoja akiwa na umri wa miaka nane, wanawake wajawazito na wanawake wanaonyonyesha pia walilengwa. Katika kisa kimoja Disemba 17 mwaka jana, kijiji cha Langa kaskazini mwa Bentiu, wanawake watano walibakwa ambapo wanne kati yao walikuwa na uja uzito mmoja akiwa karibu miezi tisa na mwingine miezi saba.” Ofisi ya haki za binadamu imesema uchunguzi umeonyesha kuwa kuna mambo mbali mbali yamechangia hali hiyo ikiwemo idadi kubwa ya wapiganaji wanaosubiri utekelezaji wa makubaliano ya amani, uwepo wa idadi kubwa ya vijana wa makundi yaliyojihami na ukosefu wa uwajibishwaji katika matukio ya ukatili wa kingono hapo awali.

Wito kwa mamlaka ya Sudan Kusini ili kuchukua hatua madhubuti

Bwana Collive akiondelea kuelezea  ameongeza kusemakuwa:“Kamishna mkuu Michelle Bachelet ametoa wito kwa mamlaka nchini Sudan Kusini kuchukua hatua ikiwemo zilizoorodheshwa kwenye makabaliano ya amani, lkulinda wanawake na wasichana, kuchunugza kwa haraka madai ya ukatili wa kingonoi na kuwawajibisha washukiwa kwa njia ya kisheria.” Kufuatia ongezeko la ripoti za ukatili wa kingono, UNMISS iliwasiliana na serikali na kuongeza doria na kuweka mahakama ya muda katika maeneo ya hatari ikiwemo Bentiu na Malakal.

18 February 2019, 13:52