Cerca

Vatican News
Kukua kwa utandawazi kumesababish alugha nyingi kuwa hatarini kupotea na iwapo lugha inapotea basi utofauti wa utamaduni unapotea na kuathiri kiungo muhimu cha jamii Kukua kwa utandawazi kumesababish alugha nyingi kuwa hatarini kupotea na iwapo lugha inapotea basi utofauti wa utamaduni unapotea na kuathiri kiungo muhimu cha jamii  

Kukua kwa utandawazi ni hatari ya kupotea kwa lugha mama

Umoja wa Mataifaifa unasema asilimia 43 ya lugha 6000 ambazo zinazungumzwa duniani leo hii ziko hatarini kutoweka.Imesema hayo wakati wa kuadhimisha Siku ya Lugha ya mama duniani tarehe 21 Februari ambapo ni mamia kadhaa tu ya lugha ambazo zimepewa nafasi katika mifumo ya elimu na kutumika kwa umma

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuadhimisha  siku ya kimatifa ya lugha ya mama, Umoja wa Mataifai unasema asilimia 43 ya lugha 6000 ambazo zinazungumzwa leo duniani ziko hatarini kutoweka. Na kwamba ni mamia kadhaa tu ya lugha ambazo zimepewa nafasi katika mifumo ya elimu na kutumika kwa umma na ni chini ya lugha 100 ambazo zinatumika katika mtandao wa kidijitali. Licha ya hali hii lakini kuna baadhi ya jamii ambazo zinajivunia lugha ya mama na ni kawaida kusikia matangazo ya lugha za mama mbali mbali kupitia radio na hata televisheni.

Katika kuadhimisha siku ya lugha ya mama duniani tarehe 21 Februari Umoja wa Mataifa unahamasisha zaidi juu ya matumizi ya lugha ya mama katika mifumo yote ya maisha iwe elimu, biashara kwa lengo la kuimarisha amani, ustawi na ushirikiano miongoni mwa watu wenye makabila, lugha na tamaduni tofauti. Licha ya umuhimu wa lugha katika kumtambulisha mtu na hata utamaduni wake, Umoja wa Mataifa una hofu kuwa kutokana na mchakato wa utandawazi lugha mama zinapotea na kila baada ya wiki mbili lugha moja inatoweka kwenye ulimwenguni huu ambamo lugha 600 za mama ziko hatarini kutoweka.

Bangladesh imechukua hatua ya kutunza na kuhifadhi lugha za mama: Bangladesh ambayo ni miongoni mwa mataifa yaliyokuwa mstari wa mbele kupitishwa kwa azimio la siku ya lugha ya mama mwaka 1999, kwa kupitia mwakilishi wake wa kudumu kwenye Umoja wa Mataifa Masud Bin Momen anasema nchi  imechukua hatua kulinda lugha hizo. Nchini Bangladesh walianzisha kituo cha kimataifa cha lugha za mama kutafiti lugha ambazo zinatoweka na jinsi gani ya kuzitunza. Na nchini kwao wana jamii ndogo za asili na mfumo wao wa elimu umeanzisha mfumo mpya ili watoto wa makabila haya madogo waweze kutumia lugha ya mama wanapoanza masomo kwa mara ya kwanza sambamba na lugha ya taifa Bengali na kiingereza ambacho kinafundishwa shuleni. Balozi Momen akizungumzia umuhimu wa kuhifadhi lugha hata zile za makabila madogo kwenye visiwa vidogo amesema, idadi kubwa ya nchi hizo za visiwa vidogo jamii zina idadi ndogo ya watu kama maelfu tu, na wanaweza kuhamishiwa kwenye nchi nyingine. La hasha! Jamii ya kimataifa na wakazi wa mataifa haya ya visiwa hivyo  ni watu ambao wanajivunia visiwa vyao na wanajitambulisha kwa lugha yao

Siku ya lugha ya mama imekuwa ikiadhimishwa tangu mwezi Februari mwaka 2000 ili kuhamasishwa kwa utofauti wa lugha, tamaduni na lugha mbalimbali kwa kuzingatia kuwa lugha ni chombo thabiti katika kuhifadhi na kuendeleza kudumu kwa tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Kwa kusisitiza zaidi umuhimu wa siku hii  ya kimataifa  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay katika ujumbe wake wa siku ya lugha ya mama duniani amethibitisha kuwa kila wiki mbili zinapopita, lugha moja ya asili inayotumika duniani inatoweka. Akitoa mfano zaidi ameweza kutoa mfano wa wamasai walioweza kutumbuiza katika moja ya burudani kupitia lugha yao ya mama! UNESCO inasema kuwa lugha ya mama ni msingi wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kwani matumizi ya lugha ya mama yanawezesha mtu kupokea maarifa mapya kwa urahisi kuliko kupitia lugha ya mapokeo au lugha ya kigeni.  Ikumbukwe kwamba kukua kwa utandawazi kumesababisha lugha nyingi kuwa hatarini kupotea na iwapo lugha inapotea basi utofauti wa utamaduni unapotea,hivyo kuathiri kiungo muhimu cha jamii hizo.

 

22 February 2019, 14:50