Tafuta

Bado kuna changamoto kubwa ya kutokomeza tendo baya la FGM.Ni karibia milioni 200 ya wanawake na wasichana duniani wamekeketwa Bado kuna changamoto kubwa ya kutokomeza tendo baya la FGM.Ni karibia milioni 200 ya wanawake na wasichana duniani wamekeketwa 

Karibia milioni 200 ya wanawake na wasichana duniani wamekeketwa!

Katika kilele cha Siku ya kutokemeza ukeketejia kila ifikapo tarehe 6 Februari ya kila mwaka UNICEF, UNFPA na UN Women kwa pamoja wameungana katika harakati za kutokomeza ukeketaji au FGM wa viungo vya wanawake ifikapo 2030

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wakati wa kuchukua hatua ili kutokomeza ukeketaji  au FGM, ifikapo mwaka 2030 ni sasa. Huo ni wito wa pamoja umetolewa tarehe 6 Februari 2019 wakati wa fursa ya kuadhimishwa kwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na wakuu  wa mashirika ya Umoja wa Mataifa:Bi Natalia Kanem, Mkurugenzi Mkuu, shirika la idadi ya watu (UNFPA),  Bi Henrietta H. Fore, Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF na Phumzile Mlambo-Ngcuka, Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Wanawake duniania  (UN Women). Wakati wa kutoa hoja zao wametolea mfano wa athari za majanga  hayo potofu ya watu ambapo wamemtaja Mary Oloiparuni ambaye akiwa na  umri wa miaka 13 tu alilazimishwa kupitia kisu cha ngariba kwa uchungu mkali na kutokwa damu kupita kiasi na uchungu umeendelea hadi leo na baadaye ambapo kila alipojifungua watoto wake watano amekuwa na maumivu ambayo hayasemeki. Viongozi hao wanathibitisha kwamba Mary hayuko peke yake,kwani kwa mujibu wa tarifa hiyo ya pamoja takriban wasichana na wanawake milioni 200 walio hai hii leo wamekeketwa na kuwa waathirika wa moja ya ukatili mkubwa kabisa wa kijinsia duniani.

Juhudi zinazohitajika kutekelezwa

Katika maadhimisho ya siku hii, viongozi hao wamesisitiza dhamira yao ya kukomesha ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu ili mamilioni ya wasichana ambao bado wako hatarini kukeketwa ifikapo 2030 kutopitia machungu aliyopitia Mary. “Juhudi hizi ni muhimu kwa sababu ukeketaji una athari za muda mrefu za kimwili, kisaikolojia na kijamii. Unakiuka haki za wanawake za kujamihiana na afya ya uzazi, utu wao, kutobaguliwa na uhuru dhidi ya ukatili au kudharaulika. Pia ukeketaji unakiuka kanuni za kitabibu, na sio salama bila kujali nanani anaufanya au mazingira ni masafi kiasi gani,” wamethibitisha. Aidha wameongeza kusema kwamba,kwa kuwa FGM ni aina mojawapo ya ukatili, lakini hauwezi kushughulikiwa bila kujumisha mifumo mingine ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kama ndoa za utotoni, na kwa maana hiyo wanahimiza kwamba ili kukomesha FGM ni lazima kushughulikia mizizi ya kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia na kuuhakikisha uwezeshaji wa wanawake kijamii na kiuchumi.

Hatua za kuchukua duniani kwa pamoja

Mwaka 2015 viongozi wa dunia kwa pamoja waliunga mkono utokomezaji wa FGM ifikapo mwaka 2030 kupitia ajenda ya maendeleo endelevu SDGs. Umoja wa Mataifa unasema hili ni lengo linalowezekana na ni lazima kuchukua hatua sasa kugeuza utashi wa kisiasa kuwa hatua. Viongozi hao wa Umoja wa Mataifa wakizitaja hatua hizo wamesema, “Katika ngazi ya taifa tunahitaji será mpya na sheria za kulinda haki za wasichana na wanawake ili waishi huru bila ukatili na ubaguzi na kwa nchi ambazo FGM bado inaendelkea kuwe na mipango ya serikali kukomesha vitendo hivyo na mipango ijumuishe bajeti kwa ajili ya elimu, afya ya uzazi, huduma za jamii na msaada wa kisheria.” Kwa kusisitiza zaidi wamesema, “katika ngazi ya kikanda, tunahitaji taasisi na jamii kufanya kazi pamoja kuzuia kitendo cha wanwake na wasichana kuvuka mipaka kwa lengo la kuwapeleka kwenye maeneo ambayo sheria kuhusu ukeketaji si kali sana ili wakafanyiwe ukatili huo.” Katika ngazi ya jamii tunataka viongozi wa dini kukemea dhana kwamba FGM msingi wake ni dini. Kwa sababu shinikizo la kijamii mara nyingi huchagiza vitendo hivyo, hivyo watu na familia zinahitaji kuelimishwa kuhusu faida za kuachana na mila hizo potofu.

Mchango wa jamii katika kutokomeza FGM

Viongozi hao Natalia Kanem, Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA, Henrietta H. Fore, Mkurugeniz Mkuu wa UNICEF na Phumzile Mlambo-Ngcuka, Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Wanawake duniani, wanasema ahadi za umma kutokomeza FGM na hususan za jamii nzima ni njia bora na ni mbinu inayofanya kazi kama jukumu la pamoja. Hata hivyo wamesema ahadi ya jamii lazima iende sanjari na mikakati ya kukosoa mila, vitendo na hulka ambazo zinakumbatia ukeketaji.Pia wamesema simulizi za waathirika manusura kama Mary zinasaidia kujenga uelewa na uhalisia wa athari za muda mrefu za vitendo hivyo kwa Maisha ya wanawake. Vitu vingine vinavyoweza kusaidia ni kampeni na matumizi ya mitandao ya kijamii katika kufikisha ujumbe kwamba kukomesha ukeketaji kunaboresha na kuokoa Maisha. Wamezishukuru serikali, asasi za kiraia, jamii na watu binafsi kwa juhudi zao kwani ukeketaji unapungua, hata hivyo wamesema lengo sio kuupunguza bali ni kuutokomeza kabisa ifikapo 2030.

Takwimu za waathirika na ukelezaji wa ukeketaji wanawake na wasichana

Leo hii katika dinia ni karibu miliono 200 za wanawake na vijana ambao wamekeketwa na kuwa janga kubwa dhidi ya ubinadamu. Milioni 68 ya wasichana watakeketwa kufikia mwaka 2030 iwapo hatua kali hazitachukiliwa. Zaidi ya milino 20 ya wanawake na wasichana ni katika nchi ya ( Misri, Sudan, Guinea, Djibouti, Kenya, Yemen na Nigeria, ambao wanaendesha suala hili la ukeketaji hata kwa mikono ya wahudumu wa afya. Uwepo wa wahuduma wa afya aina maana ya kuwa na uhakika, badala yake ni kuku ana kuhatarisha viungo vizima na vya kawaida ili vya mwili wa mwanamkea au msichana visifanya kazi yake vizuri.

Kwa njia ya mpango wa pamoja wa UNFPA  UNICEF kuhusiana na ukeketaji wa viungo vya wanawake

Tangu mwaka 2014 hadi 2017, idadi ya ukeketwaji wa wasichania kati ya miaka 15-19 imepungua katika nchi 10 kati ya nchi 17 zinazosaidiwa na mpango wa UNFPA na UNICEF; Tangu mwaka  2008 hadi 2017,zaidi ya watu milioni 34,6 wamethibitisha wazi kuacha tabia hii ya ukeketaji katika zaidi ya jumuiya 21,000; Kati ya mwaka  2014 na 2017 karibia wanawake na wasichana milioni  3,3 wameweza kupata huduma ya ulinzi, kuzuia na matibabu katika nchi 16 ambazo ni  (Burkina Faso, Djibouti, Misri, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Kenya, Mali, Mauritania, Nigeria, Senegal, Somalia, Sudan na Uganda). Nchi 13 kama  (Burkina Faso, Djibouti, Misri, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Kenya, Mauritania, Nigeria, Senegal e Uganda) kati ya nchi 17 zinazosaidia na Mpango wameweka sheria ya kuthibiti Ukeketaji au FGM na pia katika mtindo wa sheria hii zimeongezeka hata nchi nyingie tatu zaidi.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo suala la ukeketaji bado lipo na Kituo cha Masanga kinasaidia watoto 

Katika kilele cha siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wasichana duniani, FGM, nchini Tanzania, kuna kituo ambacho ni kimbilio kwa watoto wanaokwepa mila hiyo potofu, na ambacho kimeendelea kuwaepusha watoto wa kike na wao sasa ni mashuhuda. Kituo hicho cha Masanga, kilichopo mkoani Tarime mkoani Mara kinatoa mafunzo ya ukeketaji mbadala na tohara salama na ni kimbilio la watoto wanaokwepa mila hiyo. Mmoja wa walionufaika ni Elizabeth Magabe ambaye katika mahojiano na Bright Warren wa shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA,wafadhili wa kituo  hicho amesema alijiunga na kituo mwaka 2012 lakini, “nilikuwa naishi na wazazi wangu wote, lakini baba yangu kufariki duniani, ambaye alikuwa ndiye mtetezi wetu dhidi ya ukeketaji, hapo  ndipo tukaanza kupata changamoto. Ilipofikia mwaka 2014 wakati ukeketaji ndio umepamba moto, ndipo dada yangu mmoja akawa anatoka shule alipofika nyumbani likizo, wakamlazimisha na kumkeketa.

Kukimbilia Masanga kumeokoa maisha yake dhidi ya FGM

Uwepo wake kwenye kituo ulimnusuru na FGM na ameweza kuhitimu kidato cha nne na sasa ana  ushauri akisema: “mimi kwa sasa najiona kwenye familia yangu na kwenye jamii naonekana mwenye thamani na mimi mwenyewe ninajikubali kuwa nina thamani na ninaweza kukubalika kwa kila mtu. Pia nawashauri hata vijana kuwa mtoto wa kisasa ambaye hajakeketwa ni mtoto ambaye anaweza kuleta maendeleo makubwa sana katika jamii. Hata ukiangalia katika jamii yetu ya kikuria, wasichana ambao wamekeketwa hawaleti maendeleo yoyote yale.  Lakini kwa upande wangu wasichana ambao hatujakeketwa tuko tayari kuleta maendeleo na kufanya kitu kikubwa katika jamii  yetu.” Ni sauti ya Mmoja wa walionufaika Elizabeth Magabe ambaye katika mahojiano na Bright Warren wa shirika la idadi ya watu duniani,UNFPA ambaye mara baada ya baba kufariki dunia ndipo FGM ikawa tishio kwao lakini kwa hakika kituo cha Masanga kilimwokoa

06 February 2019, 11:29