Tafuta

Vatican News
Vituo vya utafiti wa majaribio ya tiba ya virus vya Ebola vimefunguliwa huko Butembo na Katwa nchini DRC Vituo vya utafiti wa majaribio ya tiba ya virus vya Ebola vimefunguliwa huko Butembo na Katwa nchini DRC  (©mostockfootage - stock.adobe.com)

DRC:Umeanzishwa utafiti wa tiba dhidi ya virus vya Ebola huko Butembo na Katwa!

Tafiti mpya zinafanywa kuhusu uwezekano wa madawa ya kutibu Virus vya Ebola katika vituo vya WHO huko Butembo na Katwa nchini DRC

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Vituo vya tiba ya ugonjwa wa Ebola vya Madaktari wa WHO huko Katwa na Butembo kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ya DRC wanashiriki mafunzo ya majaribio ya kliniki ya kuweza kudhibiti,iliyofunguliwa kwa madawa ya nguvu dhidi ya virus vya Ebola Kaskazini ya Kivu nchini DRC. Tiba nne zilizo tathiminiwa na utafiti wa kliniki, hiyo : Remdesivir, mAb114, REGN-EB3 na ZMapp ni hatua moja  ya tiba iliyoanzishwa tangu mwanzo wa mlipuko kwa kufuata protokali za utafiti  ambazo zinaruhusu kuanzishwa kwa madawa ambayo bado hayajaorodheshwa na uchunguzi wa ugonjwa wa kifo kwa njia ya ebola (MEURI) ili kuweza kutoa uwezekano mkubwa wa kuishi.

Hatua kwa ngazi ya MEURI na ile ya jabio la kliniki ni msingi kwa sababu, hii ya mwisho itaruhusu kuzaliwa kwa data za kisayansi zilizo mwafaka katika tiba. Kwa namna ya pekee katika jaribio hilo  lengo lake ni  kugundua dawa ambayo ni mwafaka zaidi wa kudhibiti virus vya Ebola kati ya madawa manne yaliyotathinimiwa katika utafiti huo. Jaribio hili linendeshwa na Shirika la Afya ulimwenguni WHO na) Taasisi ya Kitaifa DRC ya Utafiti wa madawa (INRB) na Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Marekani (NIHUS) kwa ushirikiano na wadau wengine wa Kitaifa na Kimataifa.

Huko Butembo na Katwa ndiyo kwa sasa vituo vya utafiti wa mlipuko wa Ebola ulio tangazwa tangu tarehe 1 Agosti 2018 nchini DRC, ambapo wanasema ni janga baya sana  la pili katika historia ya magojwa. Kituo cha tiba kwa Shirika la Afya duniani huko Butembo kina uwezo wa kuwapokea wagonjwa 96 wakati kile cha Katwa kilichofunguliwa mwezi ulipota, kina uwezo wa nafasi za kulala 62. Tangu mwanzo wa shughuli hiyo WHO imekwisha walaza wagonjwa 2,100 katika vituo hivi viwili na kati ya kesi 250 zimethibitiwa kuwa ni Ebola na wagonjwa 110 wamepona.

Hata hivyo Mlipuko wa 10 wa Ebola ulioikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, umeendelea kuwa changamoto kwa serikali ya nchi hiyo, kwa mujibu wa ripoti kutoka Umoja wa Mataifa na wadau wengine wanaosaidia kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo hatari. Katika tathimini iliyotolewa mapema tarehe 1 Februari 2019  na shirika la afya ulimwenguni WHO kuhusu hali ya Ebola DRC, wamesema kwamba kwa kushirikiana na serikali ya DRC na wadau wengine wanaendelea kukabiliana na mlipuko huo licha ya changamoto za kiusalama na jamii kutokuwa na Imani. WHO inasema katika wiki za karibuni kumeripotiwa idadi kubwa ya visa vipya vya Ebola viliochangiwa na mlipuko katika eneo la Katwa ambako Umoja wa Mataifa na wadau sasa wameelekeza nguvu zao kuudhibiti wakijumuisha Benin na Oicha ili kuhakikisha mlipuko huo hausambai Zaidi.

Akizungumza mjini Geneva katika tathimini hiyo mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Daktari Motshidisho Moeti amesema licha ya kudhibiti kusambaa kwa mlipuko huo timu za wauguzi na wataalamu wa afya zitafanya juhudi kubwa kujenga Imani ya jamii na ushiriki wao katika vita dhidi ya ugonjwa huu kwenye maeneo yaliyoathirika. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ikikaribia miezi sita tangu kutangazwa kwa mlipuko wa Ebola DRC, kumekuwa na jumla ya visa 752, kati ya hivyo 698 vimethibitishwa na 54 vikidhaniwa. Kwa upande wa vifo kufikia 29 Januari mwaka 2019 ilikuwa  ni asilimia 62 ya wagonjwa wote sawa na watu 465. Hata hivyo watu wengine 259 wametibiwa kwenye vituo maalum vya Ebola na kuruhusiwa kurejea nyumbani na visa hivyo zaidi vilikuwa miongoni mwa wanawake chini ya umri wa miaka 18 na watoto 115 waliokuwa na umri wa chini ya miaka mitano. Na wakati huo mapema mwezi Januari  WHO ilikuwa imetoa ripoti ya visa vipya 118 kwenye vituo 11 vya afya maeneo ya Katwa, Beni, Butembo, Kayina, Oicha, Manguredjipa, Biena, Kyondo, Musienene, Komanda na Vuhovi.

 WHO imefanya tathimini kuhusu hatari ya mlipuko wa Ebola na kusema bado iko juu sana katika ngazi ya taifa na kikanda, lakini katika ngazi ya kimataifa hatari bado ni ndogo. Na shirika hilo limesema maeneo yaliyoathirika Zaidi ni majimbo ya Kaskazini Mashariki mwa DRC yanayopakana na Uganda, Rwanda na Sudan Kusini. Na hari ya kusambaa ni kubwa kutokana na watu kusafiri kati ya  maeneo yaliyoathirika kwenda sehemu zingine za nchi nan chi jirani. Lakini hatari pia inachochewa na kwamba nchi hiyo inakabiliwa na hali mbaya ya usalama. Pia DRC hivi sasa kuna mlipuko wa kipindupindu na tatizo la malaria.

Shirika la Afya duniania (WHO) inashauri kusiwe na vikwazo vyovyote vya usafiri kwenda DRC na hata biashara na taifa hilo kutokana na taarifa zilizopo. Pia shirika hilo lilikuwa limesema hadi sasa hakuna chanjo iliyohalalishwa na kupewa leseni ya kuwalinda watu dhidi ya virusi vya Ebola hivyo mahitaji yoyote ya vyeti vya chanjo ya Ebola sio ya msingi kwa kuzuia watu kusafiri mipakani au kutoa pasi za kusafiria kwa wasafiri wanaoondoka DRC. Hivyo WHO inaendelea kufuatilia kwa karibu na endapo itahitajika kuthibitisha safari na hatua za biashara zinazohusiana na mlipuko huo. WHO inasema hadi sasa hakuna nchi yoyote ambayo imetekeleza hatua za vikwazo vya usafiri inayoingilia safari za kimataifa za kwenda na kutoka DRC. Hata hivyo shirika hilo limewashauri wasafiri kupata ushauri wa kitabibu kabla ya kusafiri na kutekeleza masharti ya usafi.

 

18 February 2019, 15:29