Ripoti ya Shirika la Afya duniani Kanda ya Ulaya inathibitisha kuwa si kweli wahamiaji na wakimbizi wanafika na magonjwa ya kuambukiza, hayo ni mawazo potofu Ripoti ya Shirika la Afya duniani Kanda ya Ulaya inathibitisha kuwa si kweli wahamiaji na wakimbizi wanafika na magonjwa ya kuambukiza, hayo ni mawazo potofu 

WHO:Wakimbizi na wahamiaji hawasababishi magonjwa ya kuambukiza huko Ulaya!

Si kweli kwamba wakimbizi na wahamiaji Ulaya husababisha magonjwa ya kuambukiza.Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Afya duniani inathibitisha kuwa kuna magonjwa kama kisukari yanatokana na ukweli wa lishe kuwa ya mashaka na fursa ya mazoezi inakuwa ni finyu. Ripoti inabaini kwa dhati kuwa wahamiaji wanafika wakiwa na afya nzuri

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Si kweli wakimbizi na wahamiaji Ulaya husababisha magonjwa ya kuambukiza. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya kwanza kabisa iliyotolewa tarehe 21 Januari 2019 na Shirika la afya ulimwenguni, WHO kanda ya Ulaya, ikilenga kubaini pengo la huduma za afya, na nini kifanyike ili kuhakikisha wakimbizi na wahamiaji wanaishi maisha yenye afya bora. Akiwasilisha ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya, Daktari Zsuzsanna Jakab amesema hali ya hatari ya kupata magonjwa inakumba wakimbizi na wahamiaji wakati huu ambapo mifumo ya sasa ya kisiasa na kijamii inahaha kukabiliana na masuala ya wakimbizi kwa njia chanya zaidi.

Wakimbizi si chanzo cha magonjwa ya kuambukiza

Akifafanua walichobaini, Daktari Jakab amesema kuwa kuna hatari ndogo sana kwa wakimbizi na wahamiaji kuambukiza wenyeji magonjwa ya kuambukiza, hii ni moja ya fikra potofu ambayo ametaka kuwaeleza. Wakati magonjwa ya kuambukiza yanahusishwa moja kwa moja na ukimbizi na  uhamiaji, kuna ongezeko la uelewa kuwa baadhi ya magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yanahitaji kushughulikiwa. Wahamiaji siyo wachukuzi kabisa wa magonjwa ya kuambukia kama vile Ebola na wala virus vya aina nyingine  hata vile vinavyojulikana kama kifua kikuu au Ukimwi zilizowahi kuthibitishwa katika raia. Kinyume chake kwa mtazamo wa vituo vya Afya,  wanasema kuwa afya za wahamiaji wanaofika ni nzuri. Kama hali nyingine ya afya inatokanayo na safari ndefu kwa ukosefu wa huduma ya hali na usafi wa kutosha. Matokeo tofauti ya hali ya wahamiaji wanafika wakiwa na wasi wasi hasa watoto wadogo ambao wanakuwa na hofu kubwa na ambao kweli wanahitaji msaada wa ushauri.

Miongoni mwa magonjwa ambayo si ya kuambukiza lakini yananyemelea zaidi wahamiaji na wakimbizi,  wansema ni kisukari ambapo kundi lililo hatarini zaidi ni kwa upande wa wanawake. Ripoti inasema kuwa magonjwa hayo kama kisukari yanatokana na ukweli kuwa lishe inakuwa ya mashaka na fursa ya mazoezi inakuwa ni finyu. Ripoti hiyo pia imebaini ukweli halisi kuhusu idadi ya wahamiaji kwenye  ukanda wa Ulaya ambapo tofauti na fikra potofu ya kwamba idadi ya wahamiaji wa kimataifa na wakimbizi kuwa ni asilimia 10 ya wakazi wote wa ukanda wa huo ambayo ni wahamiaji wa kimataifa milioni 90.7. Kati yao hao, wakimbizi ni chini  ya asilimia 7.4 na hivyo kuondoa fikra potofu ya kwamba idadi ya wahamiaji ni mara  3 au 4 zaidi ya ukweli halisi.

Hatari za watoto wakimbizi na wahamiaji

Amezungumzia pia hatari ya watoto wakimbizi kupata magonjwa kwa kuwa wanapoondolewa makwao hawafuati tena mfumo wa chanjo.  Kwa hiyo ni muhimu sana kwa nchi wanachama ambazo zinawapokea ziwapatie haraka huduma ya chanjo kwa mujibu wa ratiba ya nchi hiyo inayowapokea. Ripoti hiyo inatokana na utafiti wa nyaraka 13,000 na kile ambacho kimefikiwa na nchi za Ulaya katika kuendeleza afya ya wakimbizi na wahamiaji na iliandaliwa kwa ushirikiano na taasisi ya taifa ya afya, uhamiaji na umaskini nchini Italia, (INMP) kutoka katika mataifa 53 ambayo ni  sehemu ya kanda za uangalizi wa Shirika la  Afya Ulaya na inapanuka hadi kufika mpakani mashariki mwa Urusi na Uturuki.

25 January 2019, 14:01