Tafuta

Vatican News
Kwa sasa ni asilimia 97% ya watoto wadogo na vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ambao hawana aina yoyote ya elimu katika makambi ya wakimbizi wa Rohingya huko Bangladesh Kwa sasa ni asilimia 97% ya watoto wadogo na vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ambao hawana aina yoyote ya elimu katika makambi ya wakimbizi wa Rohingya huko Bangladesh   (ANSA)

UNICEF:Ni zaidi ya watoto wakimbizi 145,000 wa Rohingya wanarudi shuleni!

Ripoti ya Shirika la kuhudumia watoto UNICEF inasema ni zaidi ya watoto wakimbizi 145,000 wa Rohingya watakwenda shuleni.Wakati huo huo wanaripoti pia vifo vya watoto huko Sudan,na pia wanaomba serikali za Ulaya ziweze kuwa na ulinzi watoto wahamiaji

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Ripoti ya Shirika la kuhudumiwa watoto UNICEF linasema kuwa ni zaidi ya watoto wakimbizi 145,000 wa Rohingya watakwenda shuleni katika makambi ya wakimbizi  yaliyoko nchini Bangladesh. Kwa sasa ni asilimia 97% ya watoto wadogo na vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 ambao hawana aina yoyote ya elimu katika makambi ya wakimbizi. Kundi hili kwa sasa ni waathirika wa ndoa za utotoni, kazi za suruba, biashara ya binadamu, manyanyaso yakijinsia na unyonywaji. Kwa mujibu wa Unicef inasema, mara baada ya jitihada kubwa kwa upande wa jumuiya ya msaada wa kibinadamu katika ujenzi wa mtandao karibia wa vituo 1,600 vya shule katika makambi ili kutoa uhai wa mafunzo kwa vijana ambao wanakimbia vurugu na ghasia nchini Myanmara, na makini kwa sasa unaendelea kujikita katika mafunzo kwa ajili ya maelfu ya watoto ambao hawajawahi kuona shule.

Lengo lao kwa mwaka huu ni kufikia idadi kubwa zaidi ya watoto 260,000 ili wapate mafunzo kwa njia ya mtandao uliowezesha kutengeneza kwa karibu vituo 2500 vya mafunzi ambayo yataendeshwa na walimu 5000 na watu wa kujitolea wa Rohingya. Hayo yote yamethibitishwa na Eduard Beigbeder mwakilishi wa Unicef huko Bangladesh na kwamba kipeo cha wakimbizi wa Kirohingya imeweza kuwafanya kutoa jibu la haraka, japokuwa walikuwa bado hawaweza kujibu mahitaji ya haraka kwa upande wa watoto. Mwaka huu wanajaribu kuongeza huduma yao na kufikia idadi kubwa ya watoto na kwa lengo pia la kuboresha mafunzo zaidi wanayopokea.

Watoto Sudan ya Kusini wameuwawa wengi: Licha ya taarifa kuhusu vituo kujifunza, bado kuna ripoti mbaya isemayo kuwa watoto ni miongoni mwa watu waliouawa kwenye ghasia nchini Sudan, na kwa maana hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesihi mamlaka nchini humo kuhakikisha watoto wanalindwa na haki zao za msingi zinazingatiwa. UNICEF katika taarifa iliyotolewa tarehe 23 Januari  2019 mjini Amman, Yordan inasema kuwa ilitolewa taarifa ya watoto waliouawa, wengine kujueruhiwa kwenye ghasia hizo zinazoendelea za kupinga ongezeko la bei za bidhaa na ugumu wa maisha nchini humo huku watoto wengine wameshikiriwa na maaskari.

Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Geert Cappelaere amesema kwamba ingawa bado ni vigumu kwa shirika hilo kuthibitisha ripoti hizo, lakini watoto wanapaswa kulindwa wakati wote dhidi ya aina yoyote ya ghasia, ukatili na kutendewa hovyo iwe kimwili au kiakili. Amesema watoto kamwe hawapaswi  kulengwa wala kutumikishwa kama watumwa. Hata hivyo Unicef pia inathibitisha kwamba katika miezi ya hivi karibuni, Sudan imeshuhudia ongezeko kiasi kikubwa cha gharama ya maisha na uhaba wa mkate na mafuta, huku umaskini miongoni mwa watoto na kaya zao ukiongezeka na hivyo kulazimu kaya kuchukua hatua zisizo na maslahi kwa watoto kama vile kuwaondoa watoto wao shuleni. Hali hiyo ya uhaba wa bidhaa, kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia watoto limesababisha watoto wengi nchini Sudan kuhitaiji huduma ya afya na lishe. Kwa mantiki hiyo, Bwana Cappelaere ametoa wito kwa mamlaka nchini Sudan kupatia kipaumbele ulinzi wa watoto na haki zao za elimu na afya kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto.

Katika harakati za ulinzi wa watoto, pia Unicef inaomba serikali za Ulaya kulinda watoto wahamiaji:  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limeomba serikali za nchi za Ulaya kukubaliana juu ya mpango wa kikanda wa kulinda watoto wahamiaji na wakimbizi ambao wanaendelea kukumbwa na hatari kubwa na ukiukwaji mkuu wa haki za binadamu wakati wa safari za kuelekea Ulaya na ni pindi wanapowasili barani humo. Kauli hiyo ya UNICEF imo kwenye taarifa iliyotolewa tarehe 21 Januari 2019 mjini Geneva, Uswis,ambapo inaelezwa kuwa takribani watoto 400 wakimbizi na wahamiaji wamewasili kwenye fukwe za Ugiriki, Italia na Hispania wiki mbili za mwanzo za mwezi huu wa Januari.

Hii ina maana kuwa kila siku kwa wastani watoto 29 wameingia Ulaya kuanzia tarehe mosi hadi 15  Januari 2019. Watoto wanapitia machungu mengi wakati wa safari hiyo ya kuvuka bahari ya Mediteranea hasa ikizingatiwa kuwa sasa ni msimu wa baridi kali,taarifa hiyo inathbibitisha na  kunukuu ripoti za mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kati ya watu 170 wanaoohofiwa kufa maji baharini Mediteranea, miongoni mwao ni watoto na mjamzito mmoja. Taarifa imejikita kwa kina na kusema kuwa  “wiki iliyopita, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9 kutoka Iraq, aliripotiwa kufa maji kwenye bahari ya Mediteranea wakati akijaribu kufikia kisiwa cha Samos yeye na familia yake.” Kama hiyo haitoshi, mapema mwaka huu takribani watoto 6 walikwama wakiwa kwenye boti ya uokozi ya Sea Watch kwa sababu boti hiyo haikuwa na kibali cha kutia nanga na walibaki ndani ya maji kwa siku 18 hadi kibali kilipopatikana.

Afshan Khan ambaye ni  Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Ulaya, Asia ya Kati ambaye anahusika pia na masuala ya uhamiaji amesema, “kila siku watoto watyoto wako hatari ya maisha yao wakitafuta usalama na fursa za kujenga maisha yenye hadhi. Mfumo wa kikanda utasaidia kuzuia watoto hawa kukumbwa zaidi na ukatili ambao wameshakabiliana nao kwenye safari zao za kusaka maisha bora.” UNICEF inasema mipango zaidi ya uhamiaji inayopatia kipaumbele watoto inahitajika kwenye nchi zaidi za Ulaya sambamba na mipango ya kuunganisha familia.

24 January 2019, 15:29