Ukuaji wa uchumi unaotegemea sana mauzo ya bidhaa nje unawezakana kabiasa kudorora kuliko matarajio kwa mwaka 2019 kwa mujibu wa Ripoti ya Banki ya Dunia Ukuaji wa uchumi unaotegemea sana mauzo ya bidhaa nje unawezakana kabiasa kudorora kuliko matarajio kwa mwaka 2019 kwa mujibu wa Ripoti ya Banki ya Dunia 

Uchumi:Benki ya Dunia yatoa ripoti ya kudorora kwa uchumi 2019

Deni la taifa kwa mujibu wa ripoti mpya ya Banki da Dunia kwa mwaka 2019 ya matarajio ya ukuaji wa uchumi duniani imesema kuongezeka kati ya asilimia 30% hadi 50% katika miaka minne iliyopita katika baadhi ya nchi zilizotajwa kukumbwa na ongezeko la deni la serikali kama vile Msumbiji, Zimbabwe na Benin

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ripoti ya matarajio ya ukuaji wa uchumi duniani iliyotolewa Jumatano 9 Januaru 2019 na Benki ya Dunia katika mantiki ya Uchumi duniani (Global Economic Prospects) imeonesha kuwa uchumi wadunia unategemea kudhoofika kwa asilimia 2.9 kwa mwaka huu wa 2019 huku biashara ya kimataifa na uwekezaji vikipungua, mvutano wa biashara ukiendelea kuongezeka na madeni ya serikali kwa nchi za kipato cha chini yakiongezeka.

Ukuaji uchumi unaotegemea sana mauzo ya bidhaa nje, unawezakana kudorora kuliko matarajio

Taarifa ya Benki ya Dunia imesema masoko kadhaa makubwa yalikuwa na shida kubwa ya kifedha mwaka jana na kwamba katika “kukabiliana na hali hii ya changamoto, ukuaji wa soko jipya na uchumi unaoendelea vinatarajiwa kubaki mahali pabaya kwa mwaka huu wa 2019. Ukuaji wa uchumi unaotegemea sana mauzo ya bidhaa nje una uwezekano mkubwa wa kudorora kuliko ilivyotarajiwa na wakati huo ukuaji wa kiuchumi katika katika nchi nyingi unatarajiwa kupungua.

Hayo yamesema na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia Kristalina Georgieva kwamba, “mwanzoni mwa mwaka 2018 uchumi wa dunia ulikuwa unaenda vizuri, lakini ulipoteza kasi mwaka ulivyoendelea na safari hiyo na  inaweza kupata misukosuko zaidi kwa mwaka huu mpya wa 2019. Ili kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi ni muhimu nchi ziwekeze katika watu, kukuza ukuaji wa pamoja na kujenga jamii sitahimilivu.

Kukua kwa deni kitaifa katika nchi zinazoendelea

Ripoti hii inasema katika miaka ya hivi karibuni nchi za kipato cha chini zimepata vyanzo vipya vya mapato na mikopo kutoka nje ya nchi kubwa za kutoa mikopo jambo ambalo limezisaidia nchi kutekeleza mahitaji ya miradi ya maendeleo lakini suala hilo limechangia katika kukua kwa deni la taifa katika nchi hizo. Deni la taifa kwa mujibu wa ripoti limeongezeka kwa kati ya asilimia 30 hadi 50 katika miaka minne iliyopita katika baadhi ya nchi zilizotajwa kukumbwa na ongezeko la deni la serikali kama vile  Msumbiji, Zimbabwe na Benin.

Benki ya Dunia inapendekeza hatua za kunusuru uchumi kuwa ni pamoja na kurasimisha sekta isiyo rasmi kwa kuweka sera ambazo zitapunguza changamoto zinazokumba sekta hiyo. Benki ya Dunia hutoa ripoti kama hii mara mbili kwa mwaka ambapo moja hutolewa mwezi Januari na nyingine mwezi Juni kama moja ya tathimini ya maendeleo ya kiuchumi na matokeo yake katika nchi wanachama.

UCHUMI DUNIANI KWA MUJIBU WA BANKI YA DUNIA

 

10 January 2019, 13:48