Rais Sergio Mattarella: Siku ya Vijana Duniani ni fursa kwa watu wa Mungu kukutana pamoja! Rais Sergio Mattarella: Siku ya Vijana Duniani ni fursa kwa watu wa Mungu kukutana pamoja! 

Rais Mattarella: Siku ya Vijana Duniani: Cheche za matumaini!

Siku ya XXXIV ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2019. Maadhimisho haya ni fursa ya watu wa Mungu kukutana, tayari kumwilisha ndani mwao matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi; kwa kupambana kikamilifu na changamoto wanazokabiliana nazo katika hija ya maisha yao, ili kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii katika ujumla wake.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Sergio Mattarella wa Italia amemwandikia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa shukrani, kama jibu la baraka na matashi mema kutoka kwa Baba Mtakatifu, wakati akiwa njiani kuelekea nchini Panama ili kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya XXXIV ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2019. Maadhimisho haya ni fursa ya watu wa Mungu kukutana, tayari kumwilisha ndani mwao matumaini ya leo na kesho iliyo bora zaidi; kwa kupambana kikamilifu na changamoto wanazokabiliana nazo katika hija ya maisha yao, ili kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii katika ujumla wake.

Mwishoni, Rais Rais Sergio Mattarella anamtakia Baba Mtakatifu safari njema yenye matunda mengi ya amani, utulivu na mshikamano wa dhati kati ya watu wa Mataifa! Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu katika salam na matashi mema aliyomwandikia Rais Sergio Mattarella wa Italia, Jumatano tarehe 23 Januari 2019 alisema, anasukumwa kwa shahuku ya kutaka kukutana na vijana wa kizazi kipya kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanaofumbatwa katika alama ya imani na matumaini. Anamtakia Rais Mattarella heri na baraka; amani na utulivu kwa watu wa Mungu nchini Italia.

Rais Sergio Mattarella, Italia
24 January 2019, 12:49