Tafuta

Vatican News
Rais Sergio Mattarella amemtumia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa heri ya mwaka mpya 2019 Rais Sergio Mattarella amemtumia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa heri ya mwaka mpya 2019 

Italia:Ujumbe wa Rais Mattarella kwa Papa Francisko!

Ujumbe wa Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia kwa Baba Mtakatifu Francisko unajikita kutazama Ujumbe wa Papa wa fursa ya Siku ya 52 ya Maadhimisho ya Kuombea Amani duniani kwa mwaka 2019. Na kwa niaba ya wazalendo wote wa Italia anamtakia Heri na Baraka ya Mwaka mpya

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mada ya siasa safi, huduma ya amani ambayo umechagua katika Siku ya 52 ya kuombea Amani duniani, inatoa fursa kwa wale wote ambao wanayo majukumu ya umma, hasa wanaojikita katika shughuli za madaraka ya serikali, kwa ngazi mahalia, kitaifa au kimataifa ili kujipanga katika kujikita daima katika huduma elekezi au iliyokusudiwa kwa ajili ya ujenzi wa wema wa wote na kuheshimu haki msingi kwa kuhamasisha mapatano kati ya watu.

Ndiyo mwanzo wa ujumbe wa Rais Sergio Matrarella wa Italia kwa Baba Mtakatifu Francisko akimtakia matashi mema ya heri ya mwaka mpya 2019. Ujumbe wa Rais unajikita kutazama juu ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa fursa ya  Siku ya 52 ya Maadhimisho ya Kuombea Amani duniani kwa mwaka 2019. Rais Mattarella anamuunga mkono ujumbe huo wa Siku ya amani  duniani na ambao anasema,  unalekeza kwa dhati namna ya kujikita kwa dhati katika sera za kisiasa na matendo halisi ya kizazi endelevu katika umma.

Rais anasema ujumbe huo unalenga mtu binafsi na kwa ujumla ili wote wawe makini kuhakikisha kwamba ni kwa jinsi gani wanatoa huduma yao mahli popote walipo lakini zaidi kuwa wadau na wajenzi wa kuishi kwa amani kati ya watu na kuwakumbusha kwa namna ya pekeee wahusika wa kisiasa kutoa mchango mkubwa kwa wazalendo wote, kwa maana bila wao haiwezekani kabisa kujenga nguvu ya pamoja na katiba hai ya kidemkorasia

Kadhalika Rais Mattarella anathibitisha ni kwa  jinsi gani nchi ya Italia inaendeleza kufuata misingi kwa ngazi ya taifa na kimataifa ili kusaidia hatua hizo za amani na wakati huo huo hata kuingilia kati kwenye dharura ya kuzuia migogoro mipya na uendeshaji wa changamoto za kidunia, ili kujenga jamii ya amani na fungamani. Hiyo pia ni mchakato mkuu kwa miaka mitatu kwa Tume ya haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuchangia mkataba unao husu uhuru na  usawa.

Amani inajengwa kutokana na kipimo cha umoja, anaendelea Rais Mattarella na kwa kuongozwa na michakato ya upamoja. Na ili iweze kuwa sawa na endelevu katika nyakati, wote wanaalikwa kuongozwa, kuwajibika katika  masuala ya  kisiasa na kudumu. Lakini wakati huo huo wasiongozwe na hofu wala kuancha kutawaliwa na mantiki ya utaifa, ubaguzi na vita na  ukatili. Kwa niaba ya wazalendo wote wa Italia na na pia yeye binafsi anamshukuru sana Baba Mtakatifu Francisko kwa ujumbe wake huo ambao amependelea kuwatumia waamini wote wa Kanisa Katoliki, wakristo wengine na kwa watu wote wenye mapenzi mema katika fursa hiyo ya Siku ya 52 ya Maombezi ya Amani kwa mwaka 2019 na amtakia heri na baraka ya mwaka mpya.

02 January 2019, 16:51