Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi, watoto milioni moja  waliozaliwa baada ya vita nchini Siria wanateseka Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi, watoto milioni moja waliozaliwa baada ya vita nchini Siria wanateseka  

SIRIA:kwa 2019, upo uwezekano wa wakimbizi 250,000 kurudi kwao!

Shirika la kuhudumia wakimbizi (UNHCR),limesema kuwa kwa mwaka 2019 wanategea wakimbizi 250,000 wanchi ya Siria kurudi kwao, ambapo pia wanathibitisha kuwa, karibia wakimbizi 37,000 kwa mwaka 2018 wameweza kurudi nchini mwao tayari

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mwaka 2019, wakimbizi 250,000 wa Siria wanaweza kurudi katika nchi yao, iliyo haribiwa na migogoro bila ukomo tangu mwaka 2011. Hayo yametolewa na Shirika kuhudumia  wakimbizi (UNHCR), ambapo kwa mujibu wanasema karibia wakimbizi 37,000 kwa mwaka huu tayari wamekwisha rudi nchini mwao. Na namba iliyotajwa inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na jinsi ambavyo wanafanya kazi ili kuhamaisha kile kinachozuia kurudi kwao. Hayo yametamkwa na Amin Awad, Mkurugenzi wa Shirika la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa upande wa nchi za Mashariki na Afrika ya Kaskazini.

Tangu 2015-2018 milioni moja ya watoto wamezaliwa wakiwa nje ya nchi yao

Tangu mwaka 2015 hadi leo hii jumla karibia ya wakimbizi 117,000 wameweza kurudi katika nchi yao. Kwa mujibu wa dati za ofisi ya hali ya juu, inathibitisha kuwa karibia milioni 5,6 za wakimbizi wa Siria, na kati yao milioni moja waliozaliwa baada ya kukimbia nchini Siria, wanabaki bado katika mipaka ya nchi yao kama vile Uturuki, Lebanon, Yordan, Misri na Iraq. Kurudi kwao, ni kutokana na mpangilio, ambapo wao wenyewe kupenda bila kushurutishwa, vilevile hali ya usalama, hata kwa msaada wa Shirika la kuhudumia wakumbizi ( UNHCR) amesisitiza Bi Awad na kuthibitisha kuwa hakuona kulazimishwa pamoja na kwamba migogoro bado ipo. Hii pia inatokana na idadi kubwa ya vizingiti ambavyo watu wa Siria wanapaswa kukabiliana navyo kwa mfano, ukosefu wa vitambulisho, ukosefu wa hati miliki za maeneo yao, ukosefu wa huduma za afya na elimu katika maeneo ambayo wanapaswa kwenda.

Hata hivyo kwa upande wa Ofisi ya masuala ya mpango wa kibinadamu (OCHA) huko Amman wametangaza kufanya operesheni kubwa ya kupekea tani 10 za msaada wa kibinadamu kuelekea Siria, kwa ajili ya watu karibia 650,000 wenye kuhitaji msaada. Operesheni  hiyo itadumu mwezi mmoja na itafanyika kwa njia ya kupitia mpaka wa Jaber – Nassib ambao umefunguliwa wiki chache zilizopita mara baada ya kufungwa kwa miaka sasa. Umoja wa mataifa unadhibitisha kuwa karibia milioni 13 za watu wa Siria, kati ya waliorundikana ndani na wakimbizi walioko kwenye mipaka ya nchi leo hii wanahitaji msaada mkubwa.

Uzinduzi wa mpango wa kikanda kwa mwaka 2019-2020 kwa ajili ya wakimbizi wa Siria

Tarehe 11 Desemba 2018, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake, yamezindua mpango wa kikanda wa mwaka 2019-2020 kwa ajili ya kuwajengea stahamala wakimbizi wa Siria na nchi zinazowahifadhi. Mpango uliopewa jina la 3RP, ni  wenye thamani ya dola bilioni 5.5  na ambao unatarajiwa kusaidia juhudi za Uturuki, Lebanon, Jordan, Misri na Iraq  ili kukabiliana na athari mbaya za mzozo wa Siria. Taarifa ya mashirika hayo ikiwemo lile la kuhudumia wakimbizi, (UNHCR) na la mpango wa maendeleo, (UNDP) limesema nchi jirani zimekuwa na ukarimu mkubwa katika kuwahifadhi wakimbizi tangu mzozo wa Siria ulipoanza, kwa kuwawezesha kuwapa hifadhi, ulinzi, kupata huduma za umma na kuchangia katika uchumi licha ya athari hasi dhidi ya uwepo wao.

Licha ya hayo, mashirika hayo kupitia taarifa yao yamesema kuhifadhi wakimbizi hao kunazua changamoto kwani wakimbizi milioni 5.6 wamesajiliwa katika ukanda huo na watoto milioni moja wanateseka. Kutokana na kutajwa kuwa watoto wamezaliwa katika mazingira ambamo kunashuhudiwa umaskini na ukosefu wa ajira, ndoa za mapema na ajira za utotoni zinafanyika na elimu sio hakika. Mashirika hayo yametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia katika juhudi za mpango huo wa 3RP kwani jamii zinazowahifadhi watu wa Siria zinakabiliwa na changmoto za kiuchumi na kijamii. Ifikapo mwaka 2019 mpango huo wa 3RP unatarajiwa kusaidia watu milioni 9 katika nchi tano kwa misaada kwenye maeneo kama vile ulinzi kwa wakimbizi, kuwaandikisha watoto shule, kuimarisha huduma muhimu na fursa za kiuchumi hususan kwa wanawake.

Milioni 6.5 nchini Siria wana njaa kwa mujibu wa Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP)

Wakati mpango huo kukizinduliwa na  shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema kwa sasa watu milioni 6.5 nchini Siria wana njaa ambapo WFP inafikia watu milioni 3 kila mwezi ikiwemo watu milioni 3.3 wanoishi kambini nje mwa Siria. Halikadhalika WFP inasaidia watu 81,000 nchini Misri, 47,000 nchini Iraq, 880,000 nchini Jordan, 670,000 nchini Lebanon na milioni 1.5 nchini Uturuki.

SIRIA:WAKIMBIZI LAKI 6 NA NUSU KUHITAJI MSAADA
13 December 2018, 15:53