UNICEF imesema watoto Sudan ya Kusini waliotenganishwa au walio pekee yao wanakabiliwa na hatari ya ukatili, unyanyasaji na kutumikishwa,kuwaunganisha na familia ni kipaumbele cha haraka UNICEF imesema watoto Sudan ya Kusini waliotenganishwa au walio pekee yao wanakabiliwa na hatari ya ukatili, unyanyasaji na kutumikishwa,kuwaunganisha na familia ni kipaumbele cha haraka 

UNICEF:miaka 5 tangu kuzuka vita Sudan Kusini,watoto 15,000 ni wapweke!

UNICEF imesema watoto waliotenganishwa au walio pekee yao kutoka Sudan ya Kusini wanakabiliwa na hatari ya ukatili,unyanyasaji na kutumikishwa na kwa mantiki hiyo kuwaunganisha na familia ni kipaumbele cha haraka

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Taarifa ya UNICEF inasema kuwa watu milioni 4 wamefukuzwa makwao, wengi wao wakiwa ni watoto ambapo Shirika la kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wameunganisha takribani watoto 6,000 na wazazi au walezi wao. UNICEF imesema watoto waliotenganishwa au walio pekee yao wanakabiliwa na hatari ya ukatili, unyanyasaji na kutumikishwa na kwa mantiki hiyo kuwaunganisha na familia ni kipaumbele cha haraka.

Shughuli za UNICEF na wadau pia ni kutafuta familia za watoto

Naye Michael Char anayefanya kazi na UNICEF nchini Sudan Kusini na anahusika na harakati za kuwakutanisha wanafamilia amesema: “Kuna kazi nyingi inafanyika katika kutafuta  na kuunganisha wanafamilia, wakati mwingine inachukua hata miaka, wakati tukimpata mtoto ambaye ametenganishwa na familia, tunaketi naye na kumuuliza maswali mengi, tunawapiga picha na kuzituma kwenye kanzidata ya taifa na ambapo sio kazi rahisi.”anathibitisha.  UNICEF inasema hata baada ya kuwakutanisha na familia nusu ya watoto hao ikiwa ni watoto 3,000 wanahitaji msaada na hivyo idadi ya watoto wanaohitaji msaada imefikia 18,000.

Ripoti mpya iliyozinduliwa tarehe 13 Desemba 2018 huko New Delhi India na Unicef

Takribani watoto milioni 30 huzaliwa wakiwa pengine njiti au wadogo kupindukia au hata wanaugua kila mwaka na hivyo kunahitajika huduma maalum ili waweze kuishi, hayo yamesema na Shirika la afya duniani, (WHO) kwa kuangziwa na ripoti mpya iliyozinduliwa tarehe 13 Desemba 2018 huko New Delhi India.  Naye  Omar Abdi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, (UNICEF) ambao ndio wametoa ripoti hiyo iliyopatiwa jina Ishi na Chanua: Kubadilisha huduma kwa watoto wazaliwao wadogo na wagonjwa; amaesema “Pindi linapokuja suala la watoto na mama zao, huduma sahihi wakati sahihi na mahali sasa zinaweza kuleta tofauti kubwa. Hata hivyo ameongeza kusema “bado  mamilioni  ya watoto wachanga wagonjwa na wanawake wanakufa kila mwaka kwa sababu tu hawapati huduma bora ambayo ni haki yao na ambayo pia ni wajibu wetu wa pamoja kuwapatia.”

Mhutasari wa ripoti:bila huduma maalum idadi kubwa ya watoto wachanga wanakufa

 Kwa muhtasari ripoti imebaini kuwa miongoni mwa watoto wachanga wanaozaliwa wakiwa  hatarini ya kufariki dunia au kupata ulemavu, ni wale ambao wanazaliwa njiti, wanapata tatizo la ubongo wakati wanazaliwa au kupata maambukizi ya bakteria na zaidi ya yote gharama za kifedha na kisaiokolojia ambazo zinakumba familia zao zinaweza kuwa na madhara makubwa katika makuzi yao na uwezo wao wa kuzungumza. Ripoti inasema kuwa bila huduma maalum idadi kubwa ya watoto wachanga wanaozaliwa na matatizo hayo hawatamaliza mwaka wa kwanza wa uhai wao ikisema mwaka 2017, “watoto wachanga milioni 2.5 walikufa, wengi wao kutokana na magonjwa yanayozuilika, takribani theluthi mbili ya idadi hiyo walizaliwa njiti.”

Huduma bora ya malezi kwa watoto wenye matatizo ya kuzaliwa njiti

Hata hivyo ripoti imesema huduma bora ya malezi kwa watoto wenye matatizo hayo itasaidia waishi bila matatizo ambapo inaelezwa hilo likifanyika, ikifika mwaka 2030, maisha ya wanawake, watoto wachanga na njiti milioni 2.9 yanaweza kuokolewa katika mataifa 81. “Kinachotakiwa ni mikakati bora. Mathalani iwapo wahudumu wa afya wanaohudumia watoto ndio hao hao wanahudumia mama zao kuanzia wakati wa uchungu, kuzaliwa na baada ya hapo, ni rahisi kubaini tatizo mapema,” imesema ripoti hiyo. Mapendekezo mengine ni huduma ya saa 24 siku saba kwa wiki kwa watoto wachanga, mafunzo kwa wauguzi ili washirikiane na familia wakati wa utoaji huduma pamoja na kutenga fedha za kutosha ikitakiwa nyongeza ya dola senti 20 kwa kila mtu ikielezwa kuwa inaweza kuokoa watoto wachanga kati ya wawili hadi watatu katika nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2030.

15 December 2018, 10:49