Kauli mbiu ya siku ya kupambana na rushwa na ufisadi duniani kwa mwaka 2018: “kukataa kushiriki katika vitendo vyote vinavyoimarisha nguvu za ufisadi na ili kupambana na umasikini Kauli mbiu ya siku ya kupambana na rushwa na ufisadi duniani kwa mwaka 2018: “kukataa kushiriki katika vitendo vyote vinavyoimarisha nguvu za ufisadi na ili kupambana na umasikini 

Tarehe 9 Desemba ni Siku ya Kupambana na ufisadi duniani!

Kila tarehe 9 Desemba ya kila mwaka ni Siku ya kupambana na ufisadi duniani. Siku ya kupambana na ufisadi kwa mwaka 2018 inaongozwa na kauli mbiu “kukataa kushiriki vitendo vyote vinavyo imarisha nguvu ya ufisadi ili kupambana na umasikini

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 9 Desemba ni siku ya kimataifa ya kutokomeza rushwa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa vitendo vya ufisadi vimeshamiri nchi zote iwe maskini au tajiri, iwe za kaskazini au kusini. Siku ya kupambana na ufisadi kwa mwaka 2018 inaongozwa na kauli mbiu: “kukataa kushiriki katika vitendo vyote vinavyoimarisha nguvu ufisadi na ili kupambana na umasikini”. Kutokana na hilo ujumbewake Bwana Guterres uliotolewa wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasema kuwa matrilioni ya dola sawa na zaidi ya asilimia tano la pato la ndani duniani huibwa au kulipwa kifisadi.

Rushwa inadidimiza utawala wa kisheria na kusaidia kuendeleza uhalifu

Bwana Guterres amefananisha rushwa na shambulizi la kimaadili duniani ambapo anasema:“Hupora  wanajamii haki  yao ya kuwa na shuIe, hospitali na huduma nyingine muhimu, hupoteza uwekezaji wa kigeni na kupora mataifa rasilimali zao za kiasili. Katika ujumbe wake Mkuu huyo anathibitisha kwamba  rushwa inadidimiza utawala wa kisheria na kusaidia kuendeleza uhalifu kama vile usafirishaji haramu wa binadamu, madawa ya kulevya na silaha. Pampja na hayo ametaja pia ukwepaji kodi na utakasishaji wa fedha kuwa vitendo vinavyochagizwa na rushwa, hivyo kukwamisha maendeleo endelevu. Akitaka kuthibitisha zaidi amenukuu Benki ya Dunia ambayo inasema kuwa sekta ya biashara na watu binafsi hulipa zaidi ya dola trilioni 1 kila mwaka kama rushwa kwani “rushwa inasababisha rushwa kuongezeka na kuchochea tabia ya ukwepaji sheria. Hata hivyo amesema mkataba wa kimataifa dhidi ya rushwa ni mbinu mahsusi na ya msingi ya kutokomeza rushwa.

Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu yanatoa mwelekeo

Bwana Guterres akitaja moja ya  maelengo ya kimataifa anasema:“Lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu pamoja na malengo yake madogo yanatoa mwelekeo wa hatua za kuchukua,” na kuongeza kusema kuwa kwa kupitia “mfumo wa kujitathmini uliowekwa na mkataba huu, tunaweza kushirikiana kujenga msingi wa kuaminiana na uwajibikaji. Tunaweza kuelimisha na kujengea uwezo raia, na kuendeleza uwazi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika  kurejesha mali zilizoporwa.”Katika msisitiza zaidi Bwana Guteress ameseama mamilioni ya watu mwaka huu duniani kote walipiga kura huku hoja ya rushwa ikiwa ndio kipaumbele kikuu hivyo basi “katika siku ya kimataifa ya kutokomeza rushwa hebu na tusimamie maadili.”

Kwa mjibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kupambana na madawa ya kulevya

Nayo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambamba na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC imeeleza bayana kuwa rushwa inadidimiza taasisi za kidemokrasia, inazororesha maendeleo ya kiuchumi na kukosesha utulivu wa serikali. Kwa mantiki hiyo ofisi hiyo  imetaka kila mtu achukue hatua kukomesha kitisho hicho. Siku hii ya kupambana na ufisadi duniani inaadhimishwa wakati ambapo maafisa wa ngazi za juu wanaosimamia vita dhidi ya tatizo hilo wanakutana kwa mara ya kwanza katika majengo ya Benki ya Dunia ili kutoa chachu kuu ya mapambano hayo. Kikao hicho kinawashirikisha pamoja wawakilishi kutoka mataifa 134.

Mkutano wa ngazi za juu kwa wanaharakati wa kupambana na vitendo vya rushwa  huko Washington

Maafisa wa ngazi za juu wanaohusika na harakati za kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa wanakutana mjini Washington kwa lengo la kutaka kuoneza kasi hususan katika mataifa masikini. Na hii ni mara ya kwanza kiasi zaidi ya maafisa 200 wanakutana chini ya mwamvuli wa wanaharakati wa kimataifa wa kupambana na rushwa. Kulingana na Rais wa Benki ya Dunia, Bwana Robert Zoellick, anasema kuwa mitandao midogo pamoja na juhudi binafsi, vyote vimechangia katika vita hivyo vinavyofanikiwa ila hatua zaidi za pamoja bado zinahitajika kwa kasi. Katika ufunguzi rasmi wa mkutano huo, Bwana Robert Zoellick amefafanua kuwa, kuna umuhimu wa kuihakikishia jamii ya wafadhili kuwa kila sarafu wanayoitoa kuchangia katika miradi ya maendeleo inatumiwa kama ilivyokusidiwa na  ili kupambana na umasikini, vilevile kuziimarisha juhudi za kuukuza uchumi huo kwa lengo la wema wa wote.

Umuhimu wa kushirikiana kuwasaka wahalifu na vitendo vya rushwa kwa njia ya Shirika la uangalizi wa visa vya ufisadi na rushwa Transparency International

Kadhalika katika hotuba yake amesisitizia umuhimu wa kushirikiana ili kuweza kuwasaka wahalifu wanaohusika na vitendo vya rushwa na ufisadi kinyume na malengo yaliyowekwa. Tendo la kukutana maafisa hawa kwa mara ya kwanza ili kuzijadili mbinu za kufanya uchunguzi wa uhalifu huo na kuweza kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wakiwemo wanaoikwamisha miradi ya benki ya dunia. Kikao hicho cha siku tatu kinafadhiliwa na serikali za Australia, Norway na Denmark. Kulingana na kiongozi huyo wa Benki ya Dunia, mafisadi wanawaibia walio masikini ila ni wasiojali wanaowawezesha kuendelea na uhalifu huo.

Hata hivyo juhudi za binafsi za kupambana na rushwa zinafaa ila mafanikio yake si makubwa wala kuwa mfumo endelevu wa kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi. Wito huo umeungwa mkono na Ufaransa ambapo mahakama yake kuu hivi karibuni ililipa idhini shirika la uangalizi wa visa vya ufisadi na rushwa Transparency International, kuchunguza jinsi viongozi watatu wa bara la Afrika walivyojipatia mali yao nchini humo. Hii ni mara ya kwanza kwa hatua kama hiyo kuchukuliwa na shirika lisilo la kiserikali baada ya serikali ya Ufaransa kuutambua mchango wake mbele ya mahakama.

 

09 December 2018, 12:09