Tafuta

Vatican News
Kila tarehe 11 Desemba ya kila mwaka ni Siku ya Milima duniani iliyonzishwa na Umoja wa Mataifa kunako 2002 Kila tarehe 11 Desemba ya kila mwaka ni Siku ya Milima duniani iliyonzishwa na Umoja wa Mataifa kunako 2002  (Pixabay)

Tarehe 11 Desemba ni Siku ya Milima Duniani:milima ni muhimu!

Katika Siku ya Milima duniani tarehe 11 Desemba, Umoja wa Mataifa umechagua kauli mbiu kuwa milima ni muhimu. Siku hii, ilianzishwa kunako mwaka 2002 na ili dunia iwe na uelewa zaidi juu ya faida na umuhimu wa milima kwa maana vilele ambavyo maji hutiririka ni chanzo kati ya asilimia 60 hadi 80 ya maji yote yanayopatikana duniani

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo ni siku ya milima duniani ambapo Umoja wa Mataifa unahamasisha kwa nguvu zote kwa kutumia kauli mbinu milima ni muhimu.  Siku ya Milima duniani, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kunako mwaka 2002. Kuongezeka kwa umakini na umuhimu wa milima ulisababisha Umoja wa Mataifa kutangaza Siku ya Milima Kimataifa  na ambapo katika fursa hiyo, Umoja wa Mataifa ukadhinisha ifanyike kila tarehe 11 ya mwezi Desemba na tangu mwaka 2003 siku hii imeendelea kuadhimishwa. FAO ndiyo Shirika linalojikita kuandaa maadhimisho hayo na kuwa na  kazi ya kuongoza maandalizi hayo kwa ngazi ya ulimwengu.

Kwa mfano katika upande  wa  nchi ya Italia siku hii inafikiriwa kuwa maalum kwa kuzingatia mbuga na maeneo mengi katika nchi ya Italia yanaliyozungukwa na milima. Inatosha kufikiria kati ya mbuga 24 za kitaifa, mbuga 11 zinapatikana katika Miinuka na mbuga 4 katika miinuko ya juu zaidi. Zaidi ya asilimia 42,1% ya usawa wa mbuga za Taifa imefunikwa na misitu dhidi ya wastani wa asilimia 26,3% kitaifa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa kupitia tovuti zake  maalum kwa siku hii, wanasema kuwa, ingawa milima imetajwa katika ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu,  lakini bado milima inasahaulika. Kwa kuzingatia jambo hili muhimu la milima kwa kuipatia viumbe vya dunia huduma na bidhaa pamoja na hatari ambazo zinakumbana nayo wakati huu wa mabadiliko ya tabianchi, ni vyema kuongeza hatua madhubuti ili kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wake na kuilinda.

Milima ina faida nyingi sana: asilimia kati ya 60-80 ya maji yanatokana na milima

Kuna fida nyingi za milima lakini hawali ya yote ni maji kwa kuwa milima ni vilele ambavyo kwavyo maji hutiririka kulingana na kwamba milima ni chanzo kati ya asilimia 60 hadi 80 ya maji yote yanayopatikana duniani. Pili milima ina  faida katika kupunguza majanga kwa kuwa ni kimbilio la watu wengine, pindi majanga yanapotokea. Faida ya tatu ni utalii kwa maana: takribani asilimia kati ya 15 hadi 20 ya utalii duniani hufanyika milimani kutokana na maeneo hayo kuwa na utofauti wa aina yake na  vivutio, watu wenye ufahamu tofauti na urithi.

Chakula ni miongoni mwa faida za uwepo wa milima/watu wa asili

Kadhalika chakula nacho ni miongoni mwa faida za uwepo wa milima ambapo Umoja wa Mataifa unataja  kuwa vyakula kama vile quinoa, mchele, nyanya, hata viazi, mathalani kwenye vilima vya  Usambara huko mkoani Tanga nchini Tanzania. Milima ni makazi ya watu wa asili ambao wana ufahamu wa kipekee wa kitamaduni, ufahamu ambao ni lulu katika maisha ya sasa. Kwa kuzingatia faida hizo, Umoja wa Mataifa unataka maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya milima duniani yatumike kuangazia harakati ili kuongeza ufahamu wa umuhimu wa milima kwa wanasiasa na watunga sera. Leo hii Shirika la chakula na kilimo duniani, (FAO) linatumia kampeni kupitia mtandao #Mountainsmatter ili kuchagiza uelewa wa umuhimu wa milima duniani.

 

11 December 2018, 15:28