Tafuta

Vatican News
Wakimbizi wa kila taifa wanafika wakiwa na ustadi, ujuzi na utamaduni tofauti.Hivi ni vitu muhimu ambavyo vinaweza kutoa mchango madhubuti katika maendeleo ya nchi zinazowakaribisha Wakimbizi wa kila taifa wanafika wakiwa na ustadi, ujuzi na utamaduni tofauti.Hivi ni vitu muhimu ambavyo vinaweza kutoa mchango madhubuti katika maendeleo ya nchi zinazowakaribisha 

Rwanda:Kushirikisha wakimbizi ni manufaa kwa nchi!

Serikali ya Rwanda kwa ushirikiano na sekta binafsi wanasaidia wakimbizi kuanzisha biashara. Hii ni hali ya ushindi kwa pande zote kwa sababu wakimbizi wanafika wakiwa na ustadi, ujuzi na utamaduni tofauti,hivi ni vitu muhimu ambavyo vinaweza kutoa mchango madhubuti katika maendeleo ya nchi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mpango wa kujumuisha wakimbizi katika maendeleo ya kiuchumi kwenye mji mkuu wa Rwanda, Kigali, umechangia katika wakimbizi kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zimebuni ajira kwa watu 2,600 nchini humo, ikiwemo biashara ya kuuza mitungi ya gesi inayomilikiwa na mkimbizi kutoka Burundi.

Rwanda inasaidia wakimbizi kujitegemea

Akihojiwa mkimbizi kutoka Burundi wakati akiwa kwenye duka lake la kuuza mitungi ya gesi amesema alikimbilia Rwanda kunako mwaka 2015 ambapo anasema ujio wake na familia ulikabiliwa na changamoto nyingi mwanzoni kwani hali ilikuwa ngumu baada ya kujikuta mkimbizi, lakini kwa kuwa alizoea kujitegemea aligundua kuwa kuwepo Kigali, mji unaotajwa kuwa mji safi zaidi Afrika ilikuwa ni fursa ya biashara. Na Baada ya maamuzi yake mkimbizi huyo alipata mkopo kwa sababu wakimbizi wanaruhusiwa kuomba mikopo na wanalipa ushuru kwa hivyo. Faida ya kuwepo Kigali ni kwamba unaweza kufanya kazi na unaweza kufanya kazi kwa mikono binafsi wakati huo huo kwa kutangaza hata biashara binafsi!

Serikali ya Rwanda kusaidiana na sekta binafsi

Serikali ya Rwanda kwa ushirikiano na sekta binafsi wanasaidia wakimbizi kuanzisha biashara. Naye Lydia IrambonaMkurugenzi wa programu ya wakimbizi katika kampuni binafsi ya kutoa ushauri wa Inkomoko amesema: “Ni lazima kuwe na utashi wa kisiasa, kwani nchini Rwanda imekuwa rahisi kwa sababu nchi ilitia saini kuwajumuisha wakimbizi katika ukuaji wa kiuchumi na kwa sekta binafsi. Hii ni hali ya ushindi kwa pande zote kwa sababu wakimbizi hufika   na stadi, ujuzi na utamaduni tofauti na ambavyo huenda ni mchango muhimu.” Hata hivyo kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba kufikia sasa Inkomoko imewawezesha wakimbizi 809 kuanzisha biashara, ambapo wamebuni nafasi 2,600 za ajira na kuwawezesha kuchangia katika jamii zilizowakaribisha.

Milioni moja ya watu wa DRC ni wakimbizi ndani ya nchi yao

Kinyume na taarifa nzuri ya ubunifu wa biashara kwa wakimbizi nchini Rwanda ni kuhusu wakimbizi kwa mwaka 2018 nchini DRC  ambapo wanasema ni zaidi ya watu milioni moja wamefukuzwa makwao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatia mzozo unaondelea nchini humo.  Na watu waliofukuzwa makwao wako katikati ya vilima kwenye eneo la Masisi, jimbo la Kivu Kaskazini na ambapo kwa sasa hayo yamekuwa  makazi ya mapya ya raia waliofukuzwa makwao kutoka na mzozo mashariki mwa nchi hiyo. Watu wengi kwa mwaka 2018 wameshuhudia ukatili mwingi, watu wakiuwawa hovyo na waasi  au wakiporwa mali na mifugo zo, wakati huo huo wakipigwa hovyo  kikatili  watu kuwa na hatia na kuchomewa nyumba zao.

Bado hali ni nguvu ya visa vya mapigani ya wenyewe kwa wenyewe

Ingawa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimemalizika DRC, bado nchi hiyo imeendelea kukumbwa na visa vya mapigano hususan katika maeneo ya Mashariki mwa nchi. Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR mzozo unaoendelea unahatarisha watu wengi zaidi. Naye Andreas Kirchhof Afisa wa masuala ya nje wa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anasema "Kuna makumi ya maelfu ya watu ambao wanaishi kambini bila mwelekeo wowote na ambao wanataka kuanza maisha ya kawaida. Kwa sasa UNHCR inafanya kila iwezalo kusaidia wale wanaorejea nyumbani waweze kujumuika na familia na kusaidia wale ambao hawawezi kurejea kwa sasa kutokana na sababu za kiusalama". UNHCR imetoa wito kwa pande husika nchini DRC kuacha kulenga raia na wakati huohuo imeomba serikali itatue sababu za watu kufukuzwa na pia itafute suluhu kwa ajili ya waathirika.

28 December 2018, 12:50