Tafuta

UNICEF inakadiria ifikapo mwaka ujao, zaidi ya watoto 43,000 wa chini ya umri wa miaka mitano Afrika ya Kati wanakabiliwa na tishio kubwa la kufariki dunia kutokana utapiamlo mbaya UNICEF inakadiria ifikapo mwaka ujao, zaidi ya watoto 43,000 wa chini ya umri wa miaka mitano Afrika ya Kati wanakabiliwa na tishio kubwa la kufariki dunia kutokana utapiamlo mbaya 

Mtoto 1 kati ya 4 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mkimbizi na mwathirika

Watoto milioni 1.5 ambao ni sawa na theluthi mbili ya wasichana na wavulana wanahitaji misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyokumbwa na mizozo ya wenyewe. UNICEF inakadiria ifikapo mwaka ujao, zaidi ya watoto 43,000 wa chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na kitisho kikubwa cha kufariki dunia kutokana utapia mlo wa kukithiri

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF limeonya kuwa miaka mitano baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, maisha yamekuwa magumu mno kwa watoto wa nchi hiyo. Watoto milioni 1.5 ambao ni sawa na theluthi mbili ya wasichana na wavulana wanahitaji misaada ya kibinadamu katika taifa hilo linalokumbwa na mizozo lenye idadi ya wtau milioni tano. UNICEF inakadiria ifikapo mwaka ujao, zaidi ya watoto 43,000 wa chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na kitisho kikubwa cha kufariki dunia kutokana uatapia mlo mbaya.

Mtoto mmoja kati ya wanne hana makazi nchini humo au ni mkimbizi

Mwakilishi wa shirika hilo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Christine Muhigana amesema mzozo huo unafanyika katika mojawapo ya mataifa masikini zaidi duniani na hali ya watoto ni ya kutia wasiwasi mkubwa. Mtoto mmoja kati ya wanne hana makazi nchini humo au ni mkimbizi, huku maelfu wakilazimishwa kujiunga na makundi ya waasi au wakinyanyaswa kijinsia. Kufuatia na hali hiyo, Ripoti mpya ya UNICEF  iliyopewa jina “Kipeo cha Jamhuru ya Afrika ya Kani: katika dharura iliyodharauiwa , watoto wanahitaji msaada, ulinzi na wakati endelevu”imebainisha kwa dahti kuwa  watoto milioni 1.5 ambao ni sawa na theluthi mbili ya wasichana na wavulana wanahitaji misaada ya kibinadamu katika taifa hilo linalokumbwa na mizozo lenye idadi ya watu milioni tano.Hao ni ongezeko la watoto 300,000 tangu mwaka 2016. Bilashaka katika mwaka 2019 watakuwa zaidi ya 43,000 watoto chini ya miaka mitano ambao watakabiliana na hatari kubwa ya vifo kutokana na utapiamlo wa kukithiri.

Takwimu za ripoti ya UNICEF nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Takwimu zinaonesha kuwa Mtoto mmoja kati ya wanne hana makazi nchini humo au ni mkimbizi, huku karibia watu 643,000 nusu yao ikiwa ni watoto wamerundikana nchini humo na zaidi ya 573 ,000 wamepata kikimbili katika nchi za karibu. Aidha ni maelfu ya watoto wamelazimishwa kujiunga na makundi ya waasi au wakinyanyaswa kijisnia. Idadi ya mashambulizi dhidi ya wahudumu wa kibadamu imeongezea mara dufu kutoka kesi 67 kwa mwaka 2917 kufika kesi 294 kwa miezi nane na nusu ya mwaka 2018. Afrika ya kati ni nchi ya pili yenye kipeo cha vifo vingi vya watoto wadogo na mama.

Kipeo hiki kinaendelea kujionesha katika mchakato wa dharurua ya maendeleo. Nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ni  nchi ya pili kuwa na idadi kubwa ya vifo duniani  vya watoto na mama karibu ni watoto 3 kati ya 5 ambao wanaweza kumaliza shule ya msingi,wakati nusu ya watu karibia hawana maji salama ya kunywa. Nchi ya Afrika ya kati inashika nafasi ya  188 kati ya 189 ambazo hazina maendeleo fungamani ya binadamu katika nchi zote Umoja wa Mataifa. Na hiyo ni kuonesha kipimo kulingana na maisha, umri na elimu.

Kipeo kinazidi kutokana na mapa mbano kati ya makundi yenye silaha

Kipeo cha nchi ya Afrika ya Kati kinazidi kuongezeka kutokana na mapambano kati ya makundi kadhaa ya yenye silaha  kutokana na mifugo, ardhi yenye utajiri wa madini, kama dhahabu na mengine. Mara nyingi makundi yenye silaha  yanawashambulia raia, badala ya kupigana kati yao. Na mashambulizi hayo yanaharibu vituo vya afya, wahuduma, misikiti, makanisa na baadhi ya maeneo ambayo watu wamekimbilia. Viwango vya uzito mkubwa wa utapiamlo ni zaidi ya kizingiti cha dharura

Familia zilizotishwa zimelazimika kuondoka nyumbani. Hayo yote yanasababisha ukosefu wa upatikanaji mdogo sana wa huduma za matibabu, maji salama na usafi wa mazingira, matokeo ya makazi ya kulazimishwa huleta mgogoro wa utapiamlo kwa watoto. Viwango vya utapiamlo wa kukithiri  ni zaidi ya kizingiti cha dharura katika maeneo 16 ya watu waliokimbia makazi yao kati ya  18, yaliyothibitishwa kwa miaka miwili iliyopita; kwa watoto waliolazimika kukimbilia kwenye vichaka na hali  bado ni ngumu zaidi

Misaada ya kimataifa ni chache sana

UNICEF inafanya kazi ili kufikia watoto ambao wanahitaji msaada sana, mara nyingi katika hali mbaya sana. Pamoja na mapigano makubwa na wimbi la uhamisho, UNICEF  inatoa wito kwa mwaka 2018 wa kupata dola za kimarekani milioni 56,5 , na kufikia mwezi Otoba walikuwa wamepata asilimia 44%  tu ya kiasi hicho. Kutokana na hilo ni kuonesha kuwa kwamba watoto wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameachwa kwa muda mrefu sana,  amesisistiza  Muhigana na kwamba, hawa wanahitaji tahadhari na msaada sasa na watahitaji kwa muda mrefu.

01 December 2018, 15:11