Tafuta

Vatican News
Madaktari wasio na  mpaka wametumia picha 13 zinazowakilisha juhudi zao kwa mwaka 2018  walizotenda katika nchi 72 duniani, ni pamoja na wakimbizi,magonjwa na majanga ya asili Madaktari wasio na mpaka wametumia picha 13 zinazowakilisha juhudi zao kwa mwaka 2018 walizotenda katika nchi 72 duniani, ni pamoja na wakimbizi,magonjwa na majanga ya asili  (ANSA)

Kipeo cha kibinadamu:Juhudi za Madaktari wasio na mpka kwa 2018!

Madaktari wasio na mpaka wameonesha shughuli zao kwa kipindi cha mwaka mzima 2018 kwa njia ya picha zikionesha juhudi hizo katika nchi 72 duniani ambapo ni katika harakati za kusaidia binadamu na matatizo yake yanayosababishwa na mambo mengi kuanzia migogoro ya kivita,magonjwa na majanga ya asili

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuanzia msaada wa watu wa Yemen na Rohingya  hadi kufikia juhudi ya kukabiliana na dharura kama vile mlipuko wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, uharibifu wa mfumo wa afya huko Gaza, wimbi la wahamiaji huko Ulaya kupitia bahari ya Meditrenia. Ni picha 13 zilizo chaguliwa na Madaktari wasio na  mpaka kwa mwaka 2018 ili kusimulia  kwa dhati shughuli zao walizotenda kwa mwaka mzima  katika nchi 72 duniani na kama wajibu wao wa kukimbilia wadhaifu na waathirika kuwapatia matibabu.

Hawa ni binadamu wanaokimbia vita, vurugu maradhi na majanga ya asili

Mhusika wa Madaktari wasio na mipaka anasema kuwa, “ni watu ambao wanakimbia vita, na vurugu, ni watu wanaoshmbuliwa na maradhi, mlipuko wa magonjwa, au majanga ya asili. Na nyuma ya kila mmoja ya wagonjwa wao kuna historia moja ya aina yake”. Ni historia ya mateso na udhaifu, ni historia ya ujasiri ambo unaonesha kwa dhati katika picha zilizochaguliwa na madaktari wasio na mpaka ili kuonesha kazi yao ya ushuhuda wa kikundi kizima katika kambi zao za kusaidia maisha na kutoa faraja kwa watu wanaoteseka na wenye kuhitaji msaada.

Picha hizo ni zinaelezea hali halisi ya...

Kwa maana hiyo picha 13 zinaelezea hali halisi ya wakimbizi wa Rohingya walioko nchini Bangladesh( picha ya Pablo Tosco/Angular) ; watu wa Sudan ya Kusini (Foto di Frederic), Mlipuko wa Ebola nchini DRC(John Wessels/Msf);matokeo ya mapambao huko Mousul Iraq kati ya Isis na nguvu za kijeshi nchini Siria(picha ya Sacha Myers/Msf); matoke ya migogoro ya Yemen: shughuli za usiadizi katika Meli ya Aquarius ambayo kwa mwaka 2016 katika bahari ya Meditrane ilisaidia karibia watu 30,000 kwenue maji ya kimataida kati ya Libia, Italia na Malta: wahamiaji wakiwa katika njia ya mapambano huko Mexico; mfumo wa afya mbaya huko Gaza Palestina (picha ya Laurence Geai): kipeo cha vita huko Kasai nchini DRC (Léonard Pongo). Jamhuri ya Afrika ya Kati ( picha ya Alberto Rojas), makambi  ya wahamiaji na wakimbizi nchini Libia (picha ya Sara Creta). Na zaidi picha nyingine moja inaonyesha shughuli nyingine nchini Ukraine (picha ya Oksana Parafeniuk).

28 December 2018, 13:08