Tafuta

Vatican News
Migogoro ya kivita nchini Yemen imesababisha njaa kwa watoto na wengine kukosa kwenda shule, hususan huko Hudaydah ambako ni watoto 60,000 hawana fursa hiyo Migogoro ya kivita nchini Yemen imesababisha njaa kwa watoto na wengine kukosa kwenda shule, hususan huko Hudaydah ambako ni watoto 60,000 hawana fursa hiyo  (AFP or licensors)

YEMEN:watoto 60,000 Hudaydah hawaendi shule sababu ya vita!

Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF anasema kuwa ni dharura viongozi wa Yemen wafanye kazi pamoja kutafuta sululu na kulipa walimu na wafanyakazi, lakini kabla ya yote, vita dhidi ya watoto nchini Yemen lazima vimalizike!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Zaidi ya watoto zaidi ya 60,000 hawasomi shule kwa sababu ya mapigano ndani na nje ya Hudaydah  nchini Yemen . Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto nchini humo UNICEF, machafuko yamelazimisha zaidi ya robo tatu ya shule kufungwa  ambapo shule 15 zipo msitari wa mbele na zingine kutokana na kusambaratishwa na vita au kutumiwa kama malazi kwa ajili ya familia za wakimbizi wa ndani.

Naye Meritxell Relano mwakilishili wa UNICEF nchini Yemen akizungumza na waandishi wa habari tarehe 30 Novemba 2018 mjini Geneva Uswis amesema hata zile shule ambazo zinaendelea na masomo imebidi zifanye hivyo kwa awamu tofauti tofauti na kupunguza muda wa kufundisha uwe saa za asubuhi pekee yake. Ameongeza kuwa “katika eneo lililoathirika vibaya na vita la Hudaydah, mtoto mmoja tu kati ya watatu ndiye anayeweza kuendelea na elimu na chini ya robo ya waalimu wote ndiyo wanaopatikana shuleni.

Changamoto nyingi zinazowakabili waalimu kote Yemen

Wafanyakazi wengi katika sekta ya elimu  nchini Yemen hawajalipwa mishahara kwa zaidi ya miaka miwili na wengi wamelazimika kufungasha virago kukimbia machafuko au kwenda kutafuta fursa nyingine ili kujipatia riziki.” Ameongeza kuwa licha ya changamoto nyingi zinazowakabili waalimu nchini kote Yemen bado wanaendelea kufundisha watoto katika njia wawezayo, dhamira yao ya kuendelea kuelimisha watoto nchini humo ni kitendo cha kishujaa. Kadhalika amesisitiza kuwa “hakuna sehemu yoyote ya maisha ya watoto ambayo haijaathiriwa na vita nchini Yemen.

Wakati vita inajeruhi na kukatili maisha ya watoto nchini Yemen, machafuko hayo pia yameathiri vibaya elimu ya watoto na matarajio ya mustakabali wao . Pande zote kinzani katika mzozo huu ni lazima zisitishe mara moja na kujizuia na operesheni zozote za kijeshi ndani na katika shule za na yemen nzima, ili kuwalinda wanafunzi, waalimu na wafanyakazi wengine katika sekta ya elimu na kutoa fursa ya elimu kwa mamilioni ya watoto nchini humo.” Kwa kuhitimisha na uchungu amesema “Ni dharura kwamba viongozi wa Yemen wafanye kazi pamoja kutafuta sululu na kulipa walimu na wafanyakazi, Lakini kabla ya yote,vita dhidi ya watoto nchini Yemen lazima vimalizike. Hivi sasa UNICEF inashughulikia program ya kuwapa waalimu fedha kidogo kila mwezi ili kuwawezesha kuendelea kufundisha hadi pale mgogoro wa mishahara utakapotatuliwa.

UNICEF ya Italia imetanga namba ya mshikamano 45525

Kutokana na hiyo UNICEF ya Italia imetanga namba ya mshikamano 45525 ikiwa ni kampeni ya kukusanya fedha kwa ajili ya kulinda milioni moja ya watoto wenye utapiamlo Yemen na dharura nyingine: Hadi tarehe 2 Desemba 2018 upo uwezekano wa kutoa euro 2 kituma kupitia  45525 kwa kutuma ujumbe  SMS au kuita kwa simu ya mkono Wind Tre, TIM, Vodafone, Poste Mobile, CoopVoce, Tiscali.

 

 

 

30 November 2018, 17:00