Tafuta

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kupambana na ukimwi, wataalam wa UNICEF wanaomba watu wapime kuanzia ndani ya familia na watoto na vijana Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kupambana na ukimwi, wataalam wa UNICEF wanaomba watu wapime kuanzia ndani ya familia na watoto na vijana  

UNICEF:Siku ya kimataifa ya kupambana na ukimwi!

Tunapokaribia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi (HIV), UNICEF inasema kwamba ni karibia waathirika 700 kwa kila siku, kwa maana hiyo kila dakika mbili kijana mmoja anapata maambukizi ya virusi vya ukimwi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF iliyotolewa tarehe 29 Novemba, inasema kuwa karibia vijana 360,000 watakufa na magonjwa yatokanayo na ukimwi kati ya mwaka 2018 na 2030. Hii ina maana ya kwamba vijana 76 watakufa kila siku iwapo hatua madhubuti za kuwekeza hazitafanyika katika umakini wa mipango ya kuzuia na kutibu ugonjwa wa ukimwi.

Ripoti ya “Children, HIV and AIDS: The world in 2030”

Ripoti iliyopewa jina: “Watoto, HIV na  AIDS: dunia kwa mwaka 2030”,  inaonesha juu ya upeo wa watu na kwa mujibu wa takwimu za  matukio ya sasa, idadi ya maambukizi mapya ya HIV kati ya watoto na vijana kuanzia miaka 0 na 19, katika mwaka 2030 itafikia takribani 270,000 ambapo ni kushuka robo tatu tu, kulingana na takwimu za sasa. Aidha Ripoti hiyo inaonesha zaidi kuwa idadi ya watoto na vijana ambao wanakufa kwa sababu ya ugonjwa wa Aids utapungua kutoka visa 119,000 kufikia 56,000 kwa mwaka 2030.

Hata hivyo inathibitisha kuwa upungufu huo ni kidogo kwa namna ya pekee kati ya vijana. Kwa mujibu wa UNICEF, inasema ni karibia maambukizi ya watu 700 kila siku wanapata virus vya HIV kati ya vijana kuanzia mika 10 na 19, na kwa maana hiyo ni mmoja kila dakika mbili anapata virus. Kwa mujibu wa ripoti, hadi mwaka 2030, idadadi ya maambukizi mapya ya HIV kati ya watoto kabla ya miaka 10 ya maisha itakuwa imepungua nusu yake, wakati huo, kati ya vijana wenye umri kuanzia 10-19 itapungua kwa silimia 29% tu.

Ugumu wa kufikia malengo ya kuangamiza ukimwi 

Ripoti inaonesha matazamio ya kwamba vifo vitokanavyo na AIDS vitapungua kwa asilimia 57% kati ya watoto chini ya miaka 14, kulinganisha na asilimi 35% kati ya vijana kuanzia miaka 15 na 19. Lakini hata hivyo  Ripoti hiyo inaonesha wazi kuwa  kufuatia na mtazamo huo, dunia haipo katika mstari ulionyooka hasa kwa kutazama suala hili la kuweza kufikia malengo yaliyokubaliwa ya kuangamiza  ugonjwa wa AIDS, kati ya watoto na vijana ifikapo  mwaka 2030 . Hayo yamethibitishwa na Henrietta Fore, Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF.

Bi Fore anaongeza kusema  kuwa: mipango ya kuzuia kuambukiza virus vya HIV kwa mama kwa sasa inaendelea kutoa matunda, lakini bado kuna changamoto zaidi, kwa sababu mipango ya kutibu virus na kuzuia maambukizi kati ya vijana walio wakubwa ambayo haijaweza kwenda sambamba na matarajio hayo na  ambapo inapaswa kutafuta njia. Akiendela kusisitiza zaidi mkuu huyo wa UNICEF Fore anasema: “Hatuwezi kushinda vita hivi dhidi ya virusi vya ukimwi kama hatuharakishi mchakato wa maendeleo katika kuzuia maambukizo ya virusi kwa vizazi vijavyo”. Pia ameongeza: “Tunahitaji kudumisha hisia ya haraka ili kusaidia kufikia malengo yaliyopatikana katika miaka ya nyuma kwa wavulana na wasichana. Na ili kufanya hivyo tunahitaji kutafuta njia za ubunifu na kuzuia ili kufikia vijana walio katika mazingira magumu zaidi, haratishi na yenye wasiwasi zaidi.”

Data nyingine za Ripoti zinafafanua, milioni 3 ya watoto na vijana wenye virusi vya HIV katika dunia

Karibia milioni 1,9 ya watoto na vijana wataishi na virusi vya HIV mwaka 2030 sehemu kubwa ni Afrika ya Mashariki na Magharibi (1,1 milioni), itafuata Afrika ya Kati na Masahariki (571,000) na Amerika ya Kusini na Visiwa vya Caribbean (84,000). Kwa sasa milioni 3 ya watoto na vijana wanaishi na virus vya HIV katika dunia  na zaidi ya nusu yake wako Afrika ya Mashariki na Magharibi. Upungufu wa idadi ya vijana kati ya miaka 0-19 wanaoishi na virus kati ya mwaka 2018 na 2030 utaendana kulingana na kanda na kanda, kwa upungufu zaidi huko barani Asia ya Mashariki( karibia asilimia 50%) na Afrika ya Mashariki na Kusini ( asilimia 40%). Kinyume cha upungufu kitakuwa ni asilimia 24% tu kwa Afrika ya Kati na Mashariki na kanda ikiwa na ya pili kwa takwimu iliyo ya juu.

Vijana walio wengi hawajuhi kama wana maambukizi ya virus na  kati ya wale ambao wameambukizwa wanaendelea na tiba

Kwa mujibu wa Ripoti inasema kuwa watoto wengi na vijana hawajuhi kama wana maabukizi ya virus na kati ya wale walioambukizwa,wanaendelea na tiba,japokuwa  ni  wachache wanaoendelea  hivyo  kwa namna inayofaa. Ili kuweza kujibu suala hili la ukosefu wa kujua uhakika, Ripoti inashauri kufuata mbinu, ambayo inasaidiwa na UNICEF ambayo ni ya kupima kuanzia katika familia ili kusaidia kuwatambua wenye maambukizi na ili pia kuendeleza matibabu watoto wenye virus.  Ni vema kuelewa kwamba, huduma bora pamoja na kufanya vipimo mara kwa mara bila kusahau kuendelea kupata tiba, vinapaswa kupewa kipaumbele Kaskazini na Kusini mwa Afrika ili kukomesha maambukizi mapya kwa lengo la kupiga vita Ukimwi. Zoezi la kuhamasisha na kutoa taarifa kwa vijana wanaoishi kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika linabakia kuwa suala muhimu katika kupambana dhidi ya Ukimwi.

Mambo muhimu yapaswa kutendeka hasa kwa ajili ya utekelezaji zaidi 

Mambo muhimu yapaswa kutendeka hasa kwa ajili ya kutekeleza zaidi, kwa mfano usambazaji mkubwa wa teknolojia za uchunguzi katika vituo vya matibabu ili kuweza kuboresha utambuzi wa mapema kati ya watoto wachanga; matumizi makubwa ya majukwaa ya kidigitali ya kuweza kusambaza habari za ukimwi  kati ya vijana; huduma za kirafiki na vijana na  katika kizingatia vitendo vya kawaida kwa  vijana.

 

 

30 November 2018, 11:32