Tafuta

 Vaa nguo ya blue kuunga mkono kampeni ya watoto, tarehe 20 Novemba wakati wa kilele cha "Siku ya watoto duniani" Vaa nguo ya blue kuunga mkono kampeni ya watoto, tarehe 20 Novemba wakati wa kilele cha "Siku ya watoto duniani" 

Unicef:20 Novemba vaa nguo ya blue kuunga mkono kampeni ya watoto!

Tarehe 20 Novemba 1989 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliweka Mkataba wa haki za watoto huku likitangaza kwa mara nyingine kwamba haki za mtoto zinahitaji ulinzi wa kipekee na muafaka na wito wa kuziboresha mara kwa mara hali za watoto ulimwenguni kote na pia kwa maendeleo yao na elimu katika hali ya amani na usalama

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuelekea kilele cha ya  Siku ya Watoto Duniani, tarehe 20 Novemba, mtoto muigizaji, Millie Bobby Brown ameungana na mabalozi wema wa shirika la kuhudumia watoto duniani, UNICEF kwa kutumia ujumbe kwa njia ya video maalum ili  kupigia chepuo ya kampeni ya kuhamasisha haki za watoto duniani

Muundo wa video ya kuhamsasha siku ya watoto duniani

Katika Video ya kuonesha ombi la kuvaa nguo ya blue, tarehe 20 Novemba katika kuunga mkono kampeni ya watoto, inasikika sauti kutoka katika video, kwa kukushirikishana na mtoto Millie mwenye umri wa miaka 14 pamoja na waigizaji wengine Nguli Orlando Boom, Liam Neeson na Lilly Singh pamoja na mwimbaji na mtunzi Dua Pipa. Rangi iliyotamalaki ni ya blue ikibeba kauli mbiu unayoongoza kampeni hiyo ya kuvaa au kuonyesha rangi ya blue kwa mazingira yoyote kama ishara ya kuandaa mazingira ya ustawi kwa watoto. Katika video hiyo anaonekana Millie ambaye amejipatia jina la Blue na akiwa amevalia nguo ya blue, yuko kwenye mazingira ya ofisi anapiga simu akitoa amri kwa makundi mbalimbali ya watoto na watu wazima wavae au wahakikishe wana rangi ya blue. Hata wapiga rangi nao na makopo yao wanaamrishwa wahakikishe wana rangi ya blue!

Baadaye inaonekana kuwa, Dawati la ufundi! Wataalamu wa mavazi...

Sasa lazima tuwashirikishe marafiki, na  anampigia simu Liam….Orlando…Lily na Du. Baadaye Millie anasema,“Katika siku ya watoto duniani, UNICEF inatoa wito kwa watoto na watu wazima duniani kote, kuwa na rangi  ya blue ili kuunga mkono haki za watoto. Kwa kuwa na rangi ya blue na kutia saini ombi letu, unaeleza dunia kuwa unaamini katika ulimwengu wenye ustawi wa watoto na kusaidia UNICEF ifanikishe ndoto hiyo.”

Ombi hilo la kutia saini linapatikana katika tovuti ya Shirika la UNICEF,  ambapo mtu yeyote mwenye umri wa zaidi ya miaka 13 anaweza kujaza na kuwasilisha rai yake juu ya kutaka kuona haki za mtoto zinazingatiwa! Haki hizo kwa mujibu wa mkataba wa haki za mtoto duniani, (CRC) ni kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa ambapo ombi hilo lenye saini litawasilishwa kwa wakuu wa nchi na serikali mwakani.Tarehe 20 Novemba 1989 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliweka Mkataba wa haki za watoto likitangaza kwa mara nyingine kwamba haki za mtoto zinahitaji ulinzi wa kipekee na muafaka na wito wa kuziboresha mara kwa mara hali za watoto ulimwenguni kote na pia kwa maendeleo yao na elimu katika hali ya amani na usalama.

15 November 2018, 15:13